Ubunifu: vyakula vya kibongo.. Bara na Pwani .... Makabila yote, mapishi yote

Para chichi hiloπŸ˜‹πŸ˜‹πŸ˜‹πŸ˜‹
 

Hii inaitwa ni ngararumo. Chakula cha asili cha mashemeji zangu wachaga. Unaanza kwa kuchemsha mahindi makavu mpaka karibu yanaiva, unaweka maharage na magadi. Chakula kinapikiwa kwenye chungu, na kikiva unaweka chungu upside down ili yale maji ya magadi yajichuje. Chakula hiki ni kizuri kwa kunywea chai asubuhi au mchana kwa watu wasio na muda wa kupika. Generation ya sasa hawakipendi sana.
 
Nimeweka vile main πŸ˜€
Arikaa Mbwanyeni! Shighirija. Uyoga unalimwa sana huko mijini ila unauziwa watu wanaomilki maSupermarkets au Hoteli kubwa-kubwa. Sisi huku vijijini tunajiokotea huko maporini msimu ukifika ila Tahadhari; watoto au wasioujua hawaruhusiwi kuokota/kuchuma uyoga wa porini. Kosa kidogo tu; mwifwa.
 
Pembeni pawe na juice ya miwa sasaπŸ˜€
Hatari kabisa mpwa.
Sijui kuna siri gani kwenye huyu samaki pweza.
Halafu pilipili zao sijui mtengenezaji ni mmoja.
Ukila pweza wa Kimara na wa Mbagala au Kinondoni wote pilipili yao ina ladha moja....utamu sasaπŸ˜‹

Ila mie napenda pweza jamani.
Huku Dodoma hawana mwamko wa ulaji wa pweza.
Au kwa kuwa hakuna bahariπŸ€”πŸ€”
 
Ukila pweza wa Kimara na wa Mbagala au Kinondoni wote pilipili yao ina ladha moja....utamu sasaπŸ˜‹πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…