Ubunifu: vyakula vya kibongo.. Bara na Pwani .... Makabila yote, mapishi yote

Ubunifu: vyakula vya kibongo.. Bara na Pwani .... Makabila yote, mapishi yote

Chakula hiki kinaitwaje ?!
Kinapikwa na watu wa mkoa gani?
Mchanganyiko wa nini na nini?
Ukiangalia ni kama viazi vimepondwapondwa na kusongwa hivi na kuchanganywa na njegere tatizo hiyo rangi ya kijani ndio imefanya chakula kisieleweke kumechanganywa nini na nini!
Para chichi hilo😋😋😋😋
 
Inafanana na ule uzi wa vyakula ila ule ni worldwide.. Hapa kwa asilimia 100 ni vyakula tupikavyo na tulavyo kila siku
Huku hakuna chopstick, hakuna kuku kwa mrija ama kula na mikono miwili yaani visu na uma😂

TAHADHARI: KAMA UNA NJAA NA UKO MBALI NA SEHEMU YA KULA USIFUNGUE HUU UZI
Nb: Makande pia yapo😋😋😋
1740681560834.jpeg

Hii inaitwa ni ngararumo. Chakula cha asili cha mashemeji zangu wachaga. Unaanza kwa kuchemsha mahindi makavu mpaka karibu yanaiva, unaweka maharage na magadi. Chakula kinapikiwa kwenye chungu, na kikiva unaweka chungu upside down ili yale maji ya magadi yajichuje. Chakula hiki ni kizuri kwa kunywea chai asubuhi au mchana kwa watu wasio na muda wa kupika. Generation ya sasa hawakipendi sana.
 
Nimeweka vile main 😀
Arikaa Mbwanyeni! Shighirija. Uyoga unalimwa sana huko mijini ila unauziwa watu wanaomilki maSupermarkets au Hoteli kubwa-kubwa. Sisi huku vijijini tunajiokotea huko maporini msimu ukifika ila Tahadhari; watoto au wasioujua hawaruhusiwi kuokota/kuchuma uyoga wa porini. Kosa kidogo tu; mwifwa.
 
Pembeni pawe na juice ya miwa sasa😀
Hatari kabisa mpwa.
Sijui kuna siri gani kwenye huyu samaki pweza.
Halafu pilipili zao sijui mtengenezaji ni mmoja.
Ukila pweza wa Kimara na wa Mbagala au Kinondoni wote pilipili yao ina ladha moja....utamu sasa😋

Ila mie napenda pweza jamani.
Huku Dodoma hawana mwamko wa ulaji wa pweza.
Au kwa kuwa hakuna bahari🤔🤔
 
Hatari kabisa mpwa.
Sijui kuna siri gani kwenye huyu samaki pweza.
Halafu pilipili zao sijui mtengenezaji ni mmoja.
Ukila pweza wa Kimara na wa Mbagala au Kinondoni wote pilipili yao ina ladha moja....utamu sasa😋

Ila mie napenda pweza jamani.
Huku Dodoma hawana mwamko wa ulaji wa pweza.
Au kwa kuwa hakuna bahari🤔🤔
Ukila pweza wa Kimara na wa Mbagala au Kinondoni wote pilipili yao ina ladha moja....utamu sasa😋😀😀😀
 
Back
Top Bottom