Omusolopogasi
JF-Expert Member
- Aug 31, 2017
- 7,101
- 18,051
Waja JF,
Kwenye majukwaa ya kampeni za uchaguzi, Godless Lema na Halima Mdee wamekuwa wakitumia clips zenye maneno ya wapinzani wao kuonyesha jinsi walivyo vigeugeu katika maisha yao, wenye kutoa ahadi za uongo, nk. Leo wanasema hili na kesho wanasema lile na kwa hiyo wasiaminiwe na wananchi.
Kwa nini Lissu na wapinzani wengine wasitumie clip za Magufuli/Polepole nk pia kwenye majukwaa ya kampeni kuonyesha wasivyojali, wanavyobagua kwa kauli zao na matendo, wanavyodhalilisha wanawake, nk? Na pia zile ahadi uongo kama kompyuta kwa walimu wote, milioni 50 kila kijiji zinaweza kuonyeshwa kwenye majukwaa kuonyosha umma kuwa wanadili na mtu muongo. Kauli kama "Tume ikiwa huru CCM inaondoka Ikulu asubuhi na mapema" (Polepole), nk.
Kampeni za upinzani zina mambo mengi ya kuongelea na muda ni kidogo. Watumie mbinu za kisasa. Na zitumike nchi nzima. Clip za aina hii, zinaweza kutawanywa kwa wagombea ubunge na udiwani wote na kutumika katika majukwaa ya kampeni. Pia wakumbuke kuwa CHADEMA imekuwa ikisingiziwa kusema uongo katika mikutano yake. Kutumia clips za wasemaji wenyewe ni kama counterattack kwa upande wa CHADEMA. Ni vigumu mtu kukana kauli ambazo ziko kwenye clips.
Mahera na wenzie kwa hakika hawatotangaza mpinzani kushinda uchaguzi (regardless ya matokeo). Wameonyesha dalili zote za kutokufanya hivyo tangu mwanzo hado mwisho. Je, wapinzani wamejiandaeje kwa hili kama watashinda?
Nawatakia uchaguzi mwema.