Vulmeko
JF-Expert Member
- Jul 15, 2025
- 388
- 332
Tundu Lissu ameamua kufuata ubunifu wa wanasiasa na viongozi kama Kwame Nkrumah, Nelson Mandela, Mahatma Gandhi, Muammar Gaddafi, Julius Malema, Thomas Sankara na wengine. Hao walibuni mitindo ya mavazi na mwonekano, na wafuasi wengi katika jamii zao wakawaiga. Kuna uwezekano mkubwa watu wengi wataacha kunyoa au kuchana nywele zao kwa kumuiga TL. Je, uigaji huo unaweza kuleta faida au madhara katika jamii inayomuangalia na kumfuata TL? Mimi naona madhara yafuatayo:
Watakaoiga mtindo huo wa nywele, wanaweza kuingiwa na uvivu wa kujitunza(self-neglect). Wataanza kutokunyoa au kutokuchana nywele, mwisho wataacha kuoga na kufua nguo. Hii inaweza kuwasababishia magonjwa ya ngozi.
Biashara za vinyozi, wauza mafuta ya nywele na vitana, zitakosa soko.
Hayo ni baadhi ya madhara au hasara ninazoziona, watu wakiiga mtindo wa Tundu Lissu wa kuacha kunyoa au kuchana nywele.
Wewe vipi, unaona faida au madhara?