realMamy
JF-Expert Member
- Apr 28, 2024
- 7,450
- 19,184
Baba wengi Sasa hivi wanafanya kazi kwa bidii sana. Wanaondoka alfajiri, wanarudi usiku. Wanahangaika, wanajitaidi, ili familia isikose chochote.
Baba hawa wanajenga nyumba, wanalipia karo, wanakidhi mahitaji yote. Kwa macho ya watu huyu ni baba aliyefanikiwa.
Lakini ndani ya kuta za nyumba, picha ni tofauti. Kuna utajiri mwingi, lakini kuna upendo mdogo. Kuna kila kitu, ila kitu kimoja kimepungua - uwepo wa baba.
Mtoto ana viatu vipya, sare nzuri, mabegi ya shule ya kifahari. Lakini moyoni mwake kuna swali lisilokuwa na jibu Baba yuko wapi?
Baba amebadilika kuwa kama mashine ya kutoa pesa. Anatuma, analipa, lakini hapati muda wa kukaa mezani na familia.
Kumbuka Mtoto hatakumbuka kiasi cha pesa ulichomtumia miaka mingi baadaye. Atakumbuka kama ulimsikiliza alipokuwa na huzuni, kama ulimkumbatia kabla ya kulala.
Tunajivunia kuhudumia vizuri. Hakuna anayelala njaa. Ni kweli. Lakini chakula bila baba ni chakula tu. Nidhamu bila upendo ni amri tu. Malezi bila uwepo ni mafundisho tupu. Ubusy umewafanya kuwa watoa huduma bora, lakini wazazi dhaifu.
Tusidanganyike. Watoto wanakua kwa kuiga. Mtoto anajifunza kuwa mwanaume kwa kumuona baba. Msichana anajifunza thamani yake kwa jinsi baba anavyomtendea mama yake.
Baba asiyepatikana, anamfunza mtoto kwamba kazi ni muhimu kuliko watu. Kisha tunalia kwa nini mtoto amependa pesa kuliko mahusiano. Tulimfundisha wenyewe bila kujua.
Tumekuwa wageni katika nyumba zetu wenyewe. Tunaingia usiku kila mtu amelala. Tunaamka mapema kila mtu bado amelala.
Maisha yanapita hivi hivi, hadi siku moja tunageuka nyuma na kujiuliza: nilikuwa nikijenga nini hasa? Nyumba imesimama imara, lakini familia imetengana kimya kimya.
Baba, anza na kitu kidogo. Zima simu dakika chache. Kaa chini na mtoto wako. Muulize leo yake ilikuwaje, kisha msikilize kwa moyo wote. Weka familia kwenye ratiba yako kama unavyoweka miadi ya biashara. Maana familia ndio biashara yako kubwa zaidi.
Kumbuka hili: Mtoto anaweza kukua bila simu ya kisasa, bila gari, bila nguo za bei ghali. Lakini hawezi kukua bila baba. Uwepo wako ndio zawadi kubwa zaidi utakayompa.
Usiruhusu ubusy wako uibe kitu kisichoweza kurejeshwa - utoto wa mtoto wako na imani yake kwako.
Leo ukirudi nyumbani, kabla ya kufungua laptop au kuangalia pesa, kumbatia mtoto wako kwanza. Hapo ndipo utajiri wa kweli unapoanzia.
Baba tajiri si yule anaobakisha mali. Ni yule anaobakisha kumbukumbu nzuri mioyoni mwa watoto wake.
Asanteni.