Uchaguzi 2020 Uchaguzi 2020 Zanzibar: Prof. Mbarawa vs Dr. Mwinyi, nani namba zinambeba?

Uchaguzi 2020 Uchaguzi 2020 Zanzibar: Prof. Mbarawa vs Dr. Mwinyi, nani namba zinambeba?

Prof Makame Mbarawa atakuwa Rais kwa sababu moja kuu anatokea Pemba ambako hawajawahi kutoa Rais wa SMZ. Hivyo Mbarawa atawaongezea CCM ushindi kuleni Kisiwani Pemba!
hivi wewe nae ni Mtanzania? Aisee tuna kazi kubwa sana. Yaani hujawahi kujua DrShein ni Mpemba
 
Umetumwa? Mitihani ya chuo umemaliza? Acha upuuzi dogo. Pigania maisha yako.
Hahahahaaaaaaa, mkuu vipi? Kiongozi kaamua walau kufanya kautafiti kuona mtandaoni hawa wawili wakishindanandani ya CCM nani atapendekezwa. Lakini bado akishapita kuna uchaguzi kati ya CCM na upinzani. Hivyo wewe mpe jibu kwanza la swali lake!!!
 
Mmmmmmmm ni shida yaani mna waza kutuletea mizimwi yenu tena.
 
Inabidi Rais wa Zanzibar sasa sera iliopo lazima apikwe bara ndio awe Rais wa Zanzibar wazanzibar hawawezi kutoa Rais wao wenyewe. Watu wa bara mnawachagulia Rais
 
Kuna MTU anasema Pemba haijawahi kutoa raid Wa Zanzibar ,hivi Dk Shein sio mpemba? Tusiandike vitu kama hatunahakika navyo ili mradi usomeke
 
Inabidi Rais wa Zanzibar sasa sera iliopo lazima apikwe bara ndio awe Rais wa Zanzibar wazanzibar hawawezi kutoa Rais wao wenyewe. Watu wa bara mnawachagulia Rais
inaonekana huwajui wazanzibari walau kidogo
 
Kama tunavyojua kuwa 2020 Dr Shein atakuwa anafikia muhula wake wa mwisho wa uongozi visiwani Zbar, kinyang'anyiro cha kumpata mrithi wake kinaweza kikatawaliwa na 'wababe' hawa wawili yani Dr Mwinyi na Prof Mbarawa.

Sasa nimekuja kwenu wachambuzi wa maswala ya siasa mtoe uchambuzi wenu kuwa nani namba zinambeba na nani kati ya hawa wawili anaweza kuibuka kidedea?

Karibuni.
Mwinyi kiongozi wa tofauti hufanya kazi zake bila kukurupuka ni kiongozi wa mfano
 
Prof Makame Mbarawa atakuwa Rais kwa sababu moja kuu anatokea Pemba ambako hawajawahi kutoa Rais wa SMZ. Hivyo Mbarawa atawaongezea CCM ushindi kuleni Kisiwani Pemba!
Kwani shein anatokea wapi?!
 
Mwinyi kaandaliwa kuja kuwa rais visiwani

Ndio maana alihama toka mbunge wa jimbo la mkuranga na kuhamia kohani unguja.

Ulishwahi muona sijui mwinyi akijisumbua kuhangaika kuchukua fomu za uteuzi wa urais wa SMZ ama SMT...???
Jibu ni moja tu nalo ni kuwa yeye habahatishi anandaliwa na system na ndio system itamwambia lini na wakati gani achukue fomu na akishachukua fomu ni moja kwa moja "tunachukua tunaweka waaaaahh"
 
Mwinyi kaandaliwa kuja kuwa rais visiwani

Ndio maana alihama toka mbunge wa jimbo la kisarawe na kuhamia kohani unguja.

Ulishwahi muona sijui mwinyi akijisumbua kuhangaika kuchukua fomu za uteuzi wa urais wa SMZ ama SMT...???
Jibu ni moja tu nalo ni kuwa yeye habahatishi anandaliwa na system na ndio system itamwambia lini na wakati gani achukue fomu na akishachukua fomu ni moja kwa moja "tunachukua tunaweka waaaaahh"
hivi hii Wizara yake yupo tangu lini? panga pangua ikipita ametulia palepale.
 
hivi hii Wizara yake yupo tangu lini? panga pangua ikipita ametulia palepale.
Tangu enzi ya mkapa
Mwinyi kaishi kwenye wizara 3 tu

Afya-naibu waziri wa anna abdallah enzi ya mkapa.
Muungano- enzi ya jk
Ulinzi-jk
Afya tena-jk
Ulinzi tena-jk
Ulinzi tena-jpm

Yaani wizara ya ulinzi ndio nyumbani kwake na akiaminika hapo kwa kuwa ni "mtoto wa nyumbani"kutoka uzao wa dola.

Hadi hapo tu hujui tu wala kushtuka kuwa huyu bwana anaandaliwa kuwa mtawala.....!!
 
Mimi sitaki Mzanzibari awe Rais Tanganyika, kama Wazanzibari wasivyotaka Mtanganyika awe rais Zanzibar.
 
Prof Makame Mbarawa atakuwa Rais kwa sababu moja kuu anatokea Pemba ambako hawajawahi kutoa Rais wa SMZ. Hivyo Mbarawa atawaongezea CCM ushindi kuleni Kisiwani Pemba!
Kwa pemba hata akae nani ndugu ccm hawana kura watabaki kutumia nguvu nyingi na kujaza malor watu ili waende kwenye zogo lkn kwa kura hasa ccm kwa pemba noooo.
 
Back
Top Bottom