Uchaguzi 2024/25 wa nini kama hakuna Katiba Mpya?

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Amekiri Freeman Mbowe kuwa wapo makamanda wengi waandamizi kwa sasa hawamwelewi.

Msimamo wetu ulikuwa mwema sana kabla ya hoja ya maridhiano. Kwamba bila katiba mpya hakuna uchaguzi.

Hivi kweli uchaguzi utakuwaje wa haki bila ya kuwapo katiba mpya yenye tume huru ndani yake?

Kwamba tumekubali kushindwa kuipata katiba mpya kwa njia zetu na sasa tunasubiri kuletewa mezani kwa utashi wa Mama Samia kama atakavyoona inafaa?

Thubutu!

Kwani tukikiwasha katiba mpya kipaumbele, haipatikani sasa? Kama haipatikani ya nini kwenda kwenye uchaguzi ambao hautakuwa wa haki, huru wala wenye kuaminika 2024/25? Vipi sasa tutayaona mawazo haya kuwa ni ya kipuuzi?

Frvd_hpWIAEHXqi.jpeg

Makamanda, kIroho safi, tukubali kutokukubaliana:

1. Kuchezeshwa ngoma ya CCM hakuwezi kuwa na maslahi sana nasi.
2. Maridhiano kuwa siri kwa agenda na content hakuwezi kuwa na afya sana nasi.
3. Kuiondoa katiba mpya katika vipaumbele vyetu hakuwezi kuwa na mstakabali mwema sana nasi.

Shime waungwana hatujachelewa na kuteleza si kuanguka.

Aluta Continua, ushindi ni dhahiri!

Ninakazia:

Tuna Imani na CHADEMA hii, wala si nyingine
 
Raia wameridhika na mahaba ya Mama. Upumbavu mtupu hii inchi maneno kidogo raia wanadanganyika na kulainika na kuacha kusimama imara kudai mambo ya msingi.
 
Umuhimu WA katiba haupo kwenye uchaguzi Tu....katiba ina Umuhimu zaidi ya hapo..
Kufikiri kuwa kazi ya katiba ni kuja kuwarahisishia wapinzani kushika nchi ni kupotoka

Haina shaka kuwa katiba mpya ni muhimu sana kwa mambo mengi.

Hata hivyo umuhimu wake kwenye chaguzi hauwezi kudogoshwa.

Uchaguzi ulio huru, wa haki na wa kuaminika si kwa ajili kuwaingiza wapinzani madarakani, bali ni wa kuwahakikishia wadau wote haki yao na hasa wananchi.

Mzigo wa kuwa na uwakilishi usiokuwa na ridhaa ya watu ndiyo sababu kuu ya matatizo yetu yote yanayotukabili. Yaani:

Dhuluma, wizi, uporaji, ufedhuli, umaskini, rushwa, kukosekana kwa uwajibikaji, maendeleo, nk.
 
Katiba mpya sio kwa ajili ya chaguzi za kushika vyeo,,
KatIba ni kwa ajili ya wananchi, siyo wanasiasa,
Anaesubiri katiba mpya ije ili imnyooshee njia ya kupata cheo, atasubiri sana,, 😂😂
 
CCM pamoja na mapungufu yake angalau ni chama cha kitaifa...

Kuamini kuwa wapinzani ni wasafi na wapewe Tu nafasi ni hatari sana...
Wakati wanafanya ufisadi na ruzuku na wanagawa viti maalum Kwa vimada wao....

Kikimbilia zoezi la katiba mpya mradi kuwaingiza madarakani wapinzani hawa ambao Wengi ni mafisadi na Wana vyama kama ofisi zao binafsi ni hatari sana...Bora mchakato uende taratibu na kipaumbele kiwe mwananchi ajue haki zake na azitumie
 
Si unawasikia wanakwambia bila katiba mpya hawashiriki uchaguzi..
Wao Umuhimu WA katiba ni uchaguzi Tu...baasi...hawataki hata wananchi WA kawaida wasiojali siasa wasikilizwe
 
Katiba:
1. Haiondoi ufisadi
2. Haiondoi umaskini
3. Haituletei viongozi wawajibikaji
4. Haiondoi CCM madarakani
5. Haizuii mfumko wa bei
6. Haiongezi mapato ya serikali ili ilete maendeleo(ijenge miundo mbinu mbali mbali)
7. Haitabadili tabia za watanzania waupende upinzani
Katiba ni dhanio tu. Ni dhahania.
Hali halisi ni watu.
Katiba haitatuletea watu tofauti na hawa tulio nao.
Katiba is not the Elephant in the Room.
 
Hawasomi alama za nyakati,, mwakani uchaguzi wa serikali za mitaa, mwaka unaofuata uchaguzi mkuu,,

Loophole pekee ni mwaka huu, leo mwaka umebaki miezi 8,,
Dalili zote zinaonyesha sidhani kama katiba mpya itapatikana kabla ya 2025,.
Na katiba itahitaji bunge likae kuweka sheria za kuendana na katiba mpya,, hiyo nayo ni process ndefu tu, ukichukulia bunge hili mojority ni ccm, na huwezi kuwaforce wapitishe sheria anazotaka labda mbowe, au henche,,
 
Mkuu kama katiba iliyopo mambo ni yale yale na waliopo ni hao hao kulikoni waiogope mpya kuliko ukoma?

Ukweli wa mambo ni kuwa tuna katiba ya hovyo sana yenye mambo kama haya:

1. Katiba iliyopo haiwawajibishi baadhi ya watendaji wakuu kwa kuikiuka, na hii ni kwa mujibu wa katiba yenyewe?
2. kwa katiba iliyopo pana watu hata kama wakiiba, wakipora, wakiuwa, wakidhulumu nk hiyo ni halali kwa mujibu wa katiba yenyewe?
3. katiba iliyopo inawapa baadhi ya watu mamlaka ya kujifanyia lolote bila kuhojiwa au hata kuwajibishwa tu?
4. Katiba iliyopo haitoi haki sawa kwa watu wote ndani ya nchi?
5. Kuna mianya mingi katika katiba hii ambayo inaweza kuifanya mihimili mingine hata kupoteza uhuru wake wa kiutendaji kwa mujibu wa katiba yenyewe?
6. Kuna utitiri wa nafasi za uongozi wasio na tija wala ridhaa ya wananchi ambao pia ni mzigo mkubwa kwa mlipa kodi?
7. Kuna rundo kubwa la vigogo wasio na tija na wasiolipa kodi wanaopata uhalali tokea katika katiba yenyewe?
8. Nk, nk.

Linganisha na orodha yako kufahamu kuwa matatizo yetu yote yanatokana na katiba hii iliyopo.
 
😂😂,Niki sumup,, unamaanisha Rais hashitakiwi,,,
 
CCM pamoja na mapungufu yake angalau ni chama cha kitaifa...

Kuamini kuwa wapinzani ni wasafi na wapewe Tu nafasi ni hatari sana...
Wakati wanafanya ufisadi na ruzuku na wanagawa viti maalum Kwa vimada wao....

Kikimbilia zoezi la katiba mpya mradi kuwaingiza madarakani wapinzani hawa ambao Wengi ni mafisadi na Wana vyama kama ofisi zao binafsi ni hatari sana...Bora mchakato uende taratibu na kipaumbele kiwe mwananchi ajue haki zake na azitumie

Mkuu wenye nchi wananchi na msema ukweli ni sanduku la kura.

Kama wananchi wameamua kuwapa au kuwanyima wao kwa sababu zao kwa nini usingependa lifanyike hili kwa uwazi, ukweli na kuaminika na wadau wote?

Kulikoni wewe kujivika umalaika (unilaratelly) wa kuamua kufaa au kutokufaa kwa awaye yote bila ya kuiweka CV yako hadharani japo tujiridhishe?

"Watanzania wa leo si wajinga ki hivyo." --- JPM
 
😂😂,Niki sumup,, unamaanisha Rais hashitakiwi,,,

Hilo ni moja tu. Kwani wasioshtakiwa ni huyo tu mjomba?

Zingatia pia yako mengi, orodha inaendelea. Hata point #8 nayo hukuiona pale?

Tafadhali ondoa miwani ya mbao uliyovaa.
 
Mkuu wenye nchi wananchi na msema ukweli ni sanduku la kura.

Kama wananchi wameamua kuwapa au kuwanyima wao kwa sababu zao kwa nini usingependa lifanyike hili kwa uwazi, ukweli na kuaminika na wadau wote?

Kulikoni wewe kujivika umalaika (unilaratelly) wa kuamua kufaa au kutokufaa kwa awaye yote bila ya kuiweka CV yako hadharani japo tujiridhishe?

"Watanzania wa leo si wajinga ki hivyo." --- JPM
Ndio maana watanzania walishakataa kuandamana,, hawaoni sababu ya kuacha kutafuta mkaye wa kila siku, wakaandamane kutwa ili Lema aje kuwa waziri wa fedha awape bodaboda wote kazi TRA🤷
 
Hata Ruto, Gachagua na genge lao la Kenya Kwanza waliamini wakenya watamsusa Raila:

Raila aridhia: Maandamano sasa mara 2 kwa wiki

Kwa taarifa yenu kaeni hivyo hivyo, tena kwa kutulia tuli!
 
Hawasomi alama za nyakati,, mwakani uchaguzi wa serikali za mitaa, mwaka unaofuata uchaguzi mkuu,,

Loophole pekee ni mwaka huu, leo mwaka umebaki miezi 8,,
Dalili zote zinaonyesha sidhani kama katiba mpya itapatikana kabla ya 2025,.
Na katiba itahitaji bunge likae kuweka sheria za kuendana na katiba mpya,, hiyo nayo ni process ndefu tu, ukichukulia bunge hili mojority ni ccm, na huwezi kuwaforce wapitishe sheria anazotaka labda mbowe, au henche,,

Usiyesoma alama za nyakati mbona ni wewe?

Kwa taarifa yako uamuzi wote wanao wananchi. Wenye wananchi. Lolote wanaloweza amua popote na siku yote ndilo linalosimama.

Habari ndiyo hiyo.
 
Si unawasikia wanakwambia bila katiba mpya hawashiriki uchaguzi..
Wao Umuhimu WA katiba ni uchaguzi Tu...baasi...hawataki hata wananchi WA kawaida wasiojali siasa wasikilizwe

Si unawasikia?! - kwani nyie nani na mnaowasikia nao nani? Ni hii timu yenye ID bandia?

Wao umuhimu wa katiba tu?! -- wanani hao?

Wananchi wasiojali siasa wamekutuma kuwasemea hayo?

Wekeni japo utambulisho wenu tuwajue?

Mbona kujimililikisha nchi ki aina aina ndugu?

Hii nchi si yenu peke yenu.
 
Usiyesoma alama za nyakati mbona ni wewe?

Kwa taarifa yako uamuzi wote wanao wananchi. Wenye wananchi. Lolote wanaloweza amua popote na siku yote ndilo linalosimama.

Habari ndiyo hiyo.
Hakuna haja ya kubishana sana,, mda utaamua nani yuko right.. 🤷
 
Back
Top Bottom