Uchaguzi 2024/25 wa nini kama hakuna Katiba Mpya?

Uchaguzi 2024/25 wa nini kama hakuna Katiba Mpya?

Uchaguzi ukiwa huru na haki utaongeza uwajibikaji, sifia sifia hata kwa upumbavu inakera sana.
 
Mara nyingi siku jibu sababu Una uwezo mdogo Sana wa kuelewa na kujibu hoja bila kuweka assumptions

Tena unajibu Kwa ghadhabu hoja ambazo sijazungumza based na assumptions...tena hata unatoka nje ya mada....inaonesha akili ndogo ulivyo nayo ndo maana unajibu Kwa ghadhabu na hasira kitu hata hujaelewa....

Wapi nimesema napinga katiba mpya?unaweza weka hapa ushahidi nikisema napinga katiba mpya??

Umeelewa hata mada ?
Mada inasema katiba mpya na uchaguzi ujao WA mwaka 2025..
Mimi points zangu zote ni kutolazimisha katiba Kwa haraka sababu ya uchaguzi wa 2025..

Nikueleweshe wewe mwenye akili ndogo...mtu akisema katiba mpya isiharakishwe kuwahi uchaguzi WA mwaka 2025 Haina maana anapungua katiba mpya .. inawezekana anataka mchakato mzuri zaidi WA mda mrefu WA kutosha ipatikane katiba nzuri Kwa wote...bila kujali itapatikana kabla ya 2025 au kabla ya 2030....

Jifunze kuelewa kabla ya kushambulia watu Kwa matusi ulifikiri ndo unaongea la maana......

Maana halisi ya demokrasia ni watu kutofautiana mawazo....sasa nyinyi ambao mnafikiri Umuhimu WA katiba ni uchaguzi WA 2025 mkiona mtu ana maoni tofauti ghafla mnamshbulia Kwa matusi only mna reveal uwezo mdogo WA kuelewa hoja na jinsi mlivyo limited kwenye maono....

I hope nimekujibu na kukuonesha ustaarabu wa kujibu hoja bila matusi
The Boss " kuongelea muda kama ni kigezo cha kutoitamuka Katiba " nawe ni sawa na kuwa biased kwasabu pengine sababu ni interest zako zilizojificha ama ulizozificha. Wananchi kuhusu Katiba walishamaliza kazi kupitia Jaji Warioba, Nchi hii imekosa tu uongozi bora basi. FIKILIA KUNA UMUHIMU GANI WA KUPOTEZA PESA KUHUSU HILI LA KATIBA ILI HALI Kazi illisha ??
 
We jamaa kumbe uwezo wako ndo huu??aisee nitaacha kubishana na wewe...

Wewe ukiongea unawakilisha wananchi?Sisi tukiongea kitu hupendi hakitoki Kwa wananchi?Sisi sio wananchi? mwenye haki ya kuwasemea wananchi ni wewe?na sio wengine??...

Hizo mentality hazitawasaidia hata ikija hiyo katiba mpyaa...

Kwamba any different opinions sio ya wananchi??wewe ulitembea Tanzania nzima ukakutana na wananchi wakakupa mandate ya kuwasemea na wakasilikiza maoni yetu wengine wakakwambia sio ya kwao??aisee
Wewe ni mwananchi unaefaidika na Uwepo wa udhaifu huu, hivyo ndyo mana huwezi kukubali hoja hii kirahisi.
 
The Boss " kuongelea muda kama ni kigezo cha kutoitamuka Katiba " nawe ni sawa na kuwa biased kwasabu pengine sababu ni interest zako zilizojificha ama ulizozificha. Wananchi kuhusu Katiba walishamaliza kazi kupitia Jaji Warioba, Nchi hii imekosa tu uongozi bora basi. FIKILIA KUNA UMUHIMU GANI WA KUPOTEZA PESA KUHUSU HILI LA KATIBA ILI HALI Kazi illisha ??
Yes, sababu zake ni "interest" huyo ndumilakuwili sio wa kumuamini hata siku moja.
 
Katiba mpya sio kwa ajili ya chaguzi za kushika vyeo,,
KatIba ni kwa ajili ya wananchi, siyo wanasiasa,
Anaesubiri katiba mpya ije ili imnyooshee njia ya kupata cheo, atasubiri sana,, [emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23]
 
Mkisusia Uchaguzi ACT anashiriki na kuchukua viti.
 
Amekiri Freeman Mbowe kuwa wapo makamanda wengi waandamizi kwa sasa hawamwelewi.

Msimamo wetu ulikuwa mwema sana kabla ya hoja ya maridhiano. Kwamba bila katiba mpya hakuna uchaguzi.

Hivi kweli uchaguzi utakuwaje wa haki bila ya kuwapo katiba mpya yenye tume huru ndani yake?

Kwamba tumekubali kushindwa kuipata katiba mpya kwa njia zetu na sasa tunasubiri kuletewa mezani kwa utashi wa Mama Samia kama atakavyoona inafaa?

Thubutu!

Kwani tukikiwasha katiba mpya kipaumbele, haipatikani sasa? Kama haipatikani ya nini kwenda kwenye uchaguzi ambao hautakuwa wa haki, huru wala wenye kuaminika 2024/25? Vipi sasa tutayaona mawazo haya kuwa ni ya kipuuzi?

View attachment 2560606

Makamanda, kIroho safi, tukubali kutokukubaliana:

1. Kuchezeshwa ngoma ya CCM hakuwezi kuwa na maslahi sana nasi.
2. Maridhiano kuwa siri kwa agenda na content hakuwezi kuwa na afya sana nasi.
3. Kuiondoa katiba mpya katika vipaumbele vyetu hakuwezi kuwa na mstakabali mwema sana nasi.

Shime waungwana hatujachelewa na kuteleza si kuanguka.

Aluta Continua, ushindi ni dhahiri!

Ninakazia:

Tuna Imani na CHADEMA hii, wala si nyingine
Katiba mpya siyo sera ya chadema ni sera ya watz wote ttzo ni kwamba watz wengi wanaifahamu zaidi simba na yanga kuliko siasa za nchi yao
 
Katiba mpya siyo sera ya chadema ni sera ya watz wote ttzo ni kwamba watz wengi wanaifahamu zaidi simba na yanga kuliko siasa za nchi yao

Katiba Mpya haiwezi kuwa sera ya chama chochote. Ila ilikuwa kipaumbele cha kuvutia hadi siku za karibuni.

Hili la kuwatupia watz ni visingizio tu ndugu. Katika uzi huu:

Bei za vitu kushuka Kenya, sisi tunakwama wapi?

Angalia hoja za huyu Allen Kilewella kama na majibu aliyopewa. Hapa chini ni moja ya majibu kwake. Katokomea kusikojulikana:

brazaj mfano wako wa maandamano ya Kenya kumhushisha Laila unakosea sana. Ukijikumbusha vita ya Mau Mau utaona kwamba wala si suala la Laila Wakenya kuwa vile.

Lakini pia unajua ushawishi wa Laila Nairobi unatokana na nini. Tafuta kwa karibu habari za Kibera ujielimishe. Mbona siyo Kenya Nzima walioandamana??

Maandamano huratibiwa kwa watu waliotayari kuandamana ila huwezi kuratibu maandamano kwa watu wasio tayari kuandamana. Watanzania ni waoga wa kuandama dhidi ya serikali. Kenya hata bila ya Raila wataandamana tu maslahi yao yanapotishiwa!!

Nimejibu hoja zako mbili zile, nikidhani na ya Liz Truss iko hapa kumbe sivyo. Kwa vile uliileta nitaitembelea pia.

Nitategemea tuwe na forum moja kama ni nia ya majadiliano ya dhati, siyo hii ya kuruka ruka. Hii itafaa kwa flow nzuri na inapobidi inaweza kuwa muhimu kutoa maelezo marefu labda pamoja na references kadha wa kadha. (Ni maoni yangu tu.)

--------

Nikikurejea sasa kwenye post hii ambapo nitalazimika kuzijibu hoja zako kirefu, nikiweka references kadhaa zilizo relevant.

(a) Kwamba watanzania ni waoga:

1. Hoja hii itakuwa ni matusi ya wazi kwa watanzania waliokuwa JKNIA LIssu #1 na hata LIssu Kiluvya alipokuwapo pia Askofu Mwamakula. Wakati huo madarakani akiwapo jiwe kweli kweli pamoja na washirika wake.

Ninaamini kamanda LIssu hawezi kukubaliana na hoja yako hiyo isiyokuwa na afya wala ukweli wowote.

2. Hoja hii ni matusi kwa wazanzibari na wahanga wa risasi za moto kutoka kwa wanaosemekana kuwa askari wa kukodiwa kutokea nchi jirani:

Hiyo ikiwa ni ACT chini ya Maalim Seif (rip).

Ninaamini Maalim Seif akiwa hai angeipinga hoja (mufilisi) yako hiyo.
3. Kumbuka mauaji kwenye maandamano Zanzibar, 27/1/2000, CUF chini ya Maalim Seif.
4. Nani asiyeujua uliokuwa moto wa Chadema chini ya Dkt. Slaa na harakati zilizokuwapo? Nani asiyeujua uliokuwa moto wa wazanzibari chini ya Maalim Seif?
5. Nk nk.

Kuhusiana na hoja yako hiyo, hapa chini ni uzi wenye maelezo ya kina, kama nia yako ni kujadiliana kupata ufumbuzi wa mikwamo yetu yenye kushangaza.

Upinzani - walio waoga (cowards) si Wafuasi

Watanzania walioangaziwa hapo juu ni hawa hawa waliopo leo. Kumbe nini kimebadilika kuwaita wewe leo kuwa ni waoga ndugu?

(b) Kushindwa kutambua umuhimu wa Raila kwenye mapambano haya:

1. Raila hana njaa wala hao viongozi wenziwe. Kwa nini kama Raila si muhimu, maandamano Kenya hayakutokea kabla ya Raila kuyaitisha au hayakuendelea baada ya yeye kuyasitisha ikiwa kumbe kila mmoja alitokea huko kwenye maandamano kivyake vyake (na njaa yake) kama mvua?

2. Hapa zingatia kuwa Zanzibar wameandamana na CUF chini ya Maalim si vingine. Pia wameandamana na ACT chini ya Maalim si vingine. Kenya wanaandamana na Raila, siyo Karua wala Musyoka, na huo ndiyo ulio ukweli. Labda kama unadhani CUF waliandamana na Lipumba au ACT waliandamana na Zitto.

Kujaribu kuukimbia ukweli huo labda kama unataka kujitoa ufahamu tu au kutaka kuacha kujitendea haki wewe mwenyewe.

Harakati za ukombozi kama hizi, ambako maandamano ni silaha pekee hayajaacha kuwa na icons. Wamekuwapokina Mandela, Nyerere, Tutu, Mtikila, Malema nk. Hii kote duniani kama tunavyo wasikia kina Dalai Lama, Aung San Suu Kyi, nk.

Uzi huu hapa hapa chini una maelezo ya kina kuhusiana na hoja yako hii:

Tusilaumiane: Wako wapi kina Nyerere, Maalim Seif, Mtikila, Julius Malema au kina Tutu

(c) Maandamano huratibiwa:

Hakuna mahali popote nilipotumia neno kuratibiwa. Hivyo sijui ni kwa mantiki ipi unalitumia. Hilo ninakiachia mwenyewe.

(d) Kumhusu Liz Truss:

Nimemtumia huyu kuonyesha jinsi demokrasia isivyodanganya. Nikionyesha kuwa tuweke misingi huru, ya haki na demokrasia katika kupata viongozi wetu kulingana na agenda na malengo yetu.

Kwamba mtu anaweza kutokuwa anatufaa, huyo tutamtoa au kudumu naye kwa wakati wowote kulingana na outputs zake.

Kwamba kiongozi ni lazima awe na uungwaji mkono wa kutosha. Ambapo akipoteza huo anatoka au tutamtoa bika kusubiri.

(e) Siyo Kenya yote inayoandamana:

Haikuihitaji Kenya yote kuandamana kumfikisha Ruto na genge lake alipofikishwa. Hayo yako kwenye mada:

"Hakuna mahali popote Kenya (au kwingine) wanakodai kuwa hizi ni harakati za wajaluo au kuwa hata ni za kikabila, isipokuwa Tanzania. Maana kamili ya kuwa mtanzania ni mjuaji mno!"

Bado Raila hana watu wa kufikia 5,000 anaoambatana nao Nairobi, kuitia jamba jamba ya kutosha serikali ya Kenya.

"Inafahamika kuwa hata huko walamba asali, wahuni na hata vijana wa hovyo wapo. Kwamba yaliyoko kwetu na kwao yapo. Hata hivyo ujasiri wa viongozi wao wenye misimamo isiyotetereka ni jambo la kupigiwa mfano sana."

NInasimama na hoja yangu kuwa kuhamasisha na kuongoza maandamano ni wajibu wa viongozi wa harakati za ukombozi.

Kiongozi asiyeliweza hilo ni vyema akang'atuka mwenyewe au akang'atuliwa.

Hatuna upungufu wa watu wenye kuwa na ari, dhamira, kujitoa, nk, kuyafanikisha majukumu yoyote tunayojipangia kidemokrasia katika vyama.
 
Tatizo liko kwetu wananchi sisi ndio tunataka katiba kabla ya uchaguzi sio vyama vya siasa.
 
Tatizo liko kwetu wananchi sisi ndio tunataka katiba kabla ya uchaguzi sio vyama vya siasa.

Kwa hiyo vyama vya siasa havitaki katiba mpya siyo?

Kumbe nani wa kumwongoza nani kwenye madai haya? Kwamba itokee kama mvua siyo?

"Shikamoo Raila Amolo Odinga na Azimio la Umoja."

Kwa hakika Ruto na Kenya Kwanza watajuta kuzaliwa si Samia wala CCM.

Cc: Kalamu
 
Kwa hiyo vyama vya siasa havitaki katiba mpya siyo?

Kumbe nani wa kumwongoza nani kwenye madai haya? Kwamba itokee kama mvua siyo?

"Shikamoo Raila Amolo Odinga na Azimio la Umoja."

Kwa hakika Ruto ba Kenya Kwanza watajuta kuzaliwa si Samia wala CCM.

Cc: Kalamu
ccm wanaogopa katiba mpya kwasabu wanajua bila wizi wa kura awatoboi ndichanza cha kupiga Dana Dana.

Vyama vya upinza vikovingi uwezi sikia wakidai katiba mpya kwasabu chakupoteza awana.

Chadema waongoze maandamani ya kuilazimisha sereka kuandaa katiba mpya kabla ya uchaguzi 2025 ccm lazima watoke.
 
Uzi huu unajielekeza:

Tudai uchaguzi wa haki badala ya kudai kuibiwa baada ya chaguzi

Vyama vya siasa vina maslahi makubwa ya moja kwa moja na katiba mpya isipokuwa CCM.

"Chadema waanze na free and fair primaries. Viongozi wanofaa na wenye ushawishi wapewe chama."

Chadema inao ubavu wa kuongoza harakati za kudai katiba mpya.

Wanachama 8m+ wasiokuwa na influence Kwa maamuzi ya nchi wa nini?
 
Kwa hiyo vyama vya siasa havitaki katiba mpya siyo?

Kumbe nani wa kumwongoza nani kwenye madai haya? Kwamba itokee kama mvua siyo?

"Shikamoo Raila Amolo Odinga na Azimio la Umoja."

Kwa hakika Ruto ba Kenya Kwanza watajuta kuzaliwa si Samia wala CCM.

Cc: Kalamu
Umemjibu vyema huyo anayedhani wananchi wanaoihitaji Katiba Mpya wataamuka tu siku moja na kujipanga kuidai bila ya uwepo wa uongozi na uratibu wa juhudi zao hizo.
Hawa watu wengine wanajiwekea tu mabandiko humu bila ya kufikiri maana ya wanachokibandika.

Kuhusu ya Raila (Azimio la Umoja) na Ruto (Kenya Kwanza), habari zao wote ninazo vizuri sana. Namsikitikia tu Mzee Odinga kwa juhudi kubwa alizokwisha fanya miaka yote hii bila ya mafanikio ya kuchukua uongozi wa nchi hiyo. Ambalo nalijua na lipo wazi kabisa, alipokonywa ushindi wazi kabisa aliposhindana na Kibaki na kusababisha matatizo yaliyowapeleka ICC akina Uhuru na Ruto.
Amehangaika sana Raila kuutafuta uongozi wa nchi hiyo, lakini mbali ya uonevu anaofanyiwa mara kadhaa, kuna mambo anayoyafanya yeye mwenyewe yanayosababisha kazi yake kuwa ngumu sana na kutokuwa na mafanikio anayoyatafuta. Haya yote niyasemayo yana ushahidi na mifano mingi tu ya kui'support'.

Lakini nikuombe radhi, nisingependa kuingia kwenye mjadala huo wa mambo ya majirani zetu. Tuweke mawazo yetu kwenye haya yetu makubwa yanayotukabili hapa wenyewe chini ya hiki chama cha CCM.

Kama kuna mifano mizuri unayoiona tunaweza kuichukua toka huko kwingine na kuitumia hapa itusaidie kuwadhibiti hawa wahuni wa CCM, hayo ndiyo mambo tunayoweza kuyajadili na kuona ni namna gani yanavyoweza kutusaidia katika adhma yetu hii.
 
"Chadema waanze na free and fair primaries. Viongozi wanofaa na wenye ushawishi wapewe chama."
Hili ni moja ya mambo muhimu sana ndani ya chama, ambayo sasa hivi yangekuwa yanafanyiwa kazi toka ngazi za chini kabisa za chama huko mashinani. Huko ndiko kunakotakiwa kuwekewa mkazo wote kichama..
Wizi wa kura kwa mabavu unaofanywa na CCM huanzia huko huko; kwa hiyo CHADEMA nao wanatakiwa kuimarisha matawi yao, wakatae na kuzuia wizi huo tokea huko huko vijijini.
Haya ndiyo tunayowasisitizia CHADEMA mara kwa mara humu wayatambue na wachukue hatua ya kuyazuia.

Wanachama 8m+ wasiokuwa na influence Kwa maamuzi ya nchi wa nini?
Wao wanasema, 'kidigitali' wanao takribani milioni 15!
Kama ni kweli, hawa ni watu wengi sana wanaoweza kukataa uhujumu wa aina yoyote ile unaolenga kuvuruga kura zao. Kinachokosekana hapo ni uongozi wa kuwaongoza jinsi ya kukataa kunyanyaswa. Ni wajibu wa CHADEMA kuwapa elimu hawa wanachama wao na kuweka mikakati inayoeleweka ni namna gani wanavoweza kukataa kujhujumiwa, hata bila ya wao kuvunja sheria za nchi.

Pili, hawa wananchama, milioni 15, kama kweli wapo, na wengine wengi ambao ni wapenzi tu wa chama hicho, na hata sisi tulio nje kabisa ya hizi siasa, lakini tunapigania maslahi ya nchi yetu yanayovurugwa na CCM; tukielezwa na kuonyeshwa mipango madhubuti iliyo nayo CHADEMA, na kuhitaji michango ya fedha, hata ttukichanga Tsh 1,000/ tu kwa kila mmoja wetu, hiyo ni pesa ya kutosha kabisa kukabiliana na CCM ambao hutumia pesa toka kwa mafisadi kuwachangia ili waendelee kukaa madarakani.

Hili nalo CHADEMA wanatakiwa walisimamie tokea sasa na wananchi wajue mipango ya namna hii ipo ili na wao washiriki kikamilifu.
 
Umemjibu vyema huyo anayedhani wananchi wanaoihitaji Katiba Mpya wataamuka tu siku moja na kujipanga kuidai bila ya uwepo wa uongozi na uratibu wa juhudi zao hizo.
Hawa watu wengine wanajiwekea tu mabandiko humu bila ya kufikiri maana ya wanachokibandika.

Kuhusu ya Raila (Azimio la Umoja) na Ruto (Kenya Kwanza), habari zao wote ninazo vizuri sana. Namsikitikia tu Mzee Odinga kwa juhudi kubwa alizokwisha fanya miaka yote hii bila ya mafanikio ya kuchukua uongozi wa nchi hiyo. Ambalo nalijua na lipo wazi kabisa, alipokonywa ushindi wazi kabisa aliposhindana na Kibaki na kusababisha matatizo yaliyowapeleka ICC akina Uhuru na Ruto.
Amehangaika sana Raila kuutafuta uongozi wa nchi hiyo, lakini mbali ya uonevu anaofanyiwa mara kadhaa, kuna mambo anayoyafanya yeye mwenyewe yanayosababisha kazi yake kuwa ngumu sana na kutokuwa na mafanikio anayoyatafuta. Haya yote niyasemayo yana ushahidi na mifano mingi tu ya kui'support'.

Lakini nikuombe radhi, nisingependa kuingia kwenye mjadala huo wa mambo ya majirani zetu. Tuweke mawazo yetu kwenye haya yetu makubwa yanayotukabili hapa wenyewe chini ya hiki chama cha CCM.

Kama kuna mifano mizuri unayoiona tunaweza kuichukua toka huko kwingine na kuitumia hapa itusaidie kuwadhibiti hawa wahuni wa CCM, hayo ndiyo mambo tunayoweza kuyajadili na kuona ni namna gani yanavyoweza kutusaidia katika adhma yetu hii.

Kujifunza kutokea kokote hakuna maana ya kuchukua 100% za popote. Kutofautiana kwenye miscellaneous hakuwezi kutuondoa kutoka kwenye yaliyo ya msingi.

"Msingi wa hoja CCM atolewe madarakani sasa ndani ya sheria zilizopo."

Ni wazi kuwa sheria zilizopo haziruhusu wizi wa chaguzi. Pia sheria zilizopo zinaruhusu kuzuia jinai ikiwamo zinazohusu chaguzi.

Tupambane na watu hawa Kwa namna zote ziwezekanazo. Tuwa infiltrate watu hawa.

"Infiltration haiwezi kuwa wao kwetu tu."

Pana haja ya kuyaweka bayana yote yanayotakikana na kuyapigania kutokea ndani na nje chama.

Huu unapaswa kuwa muda wa kuambiana ukweli bila kujali nani anataka au hataki kusikia Nini.

Tusisitize agenda na malengo kuwa ndiyo kuwa ni ya kudumu. Si maadui wala marafiki.

Tuwekeze kwenye kutafuta mashirikiano na wengine vikiwamo vyama vya siasa na taasisi za kidini.

Chadema ni yetu, sote tuliomo. Kama ilivyo, Kwa wengine popote waliko.
 
Back
Top Bottom