Uchaguzi 2025, CHADEMA warudishwa uwanjani na serikali ya CCM, Je, CHADEMA watakubali au watagoma? 5 questions to answer!

Uchaguzi 2025, CHADEMA warudishwa uwanjani na serikali ya CCM, Je, CHADEMA watakubali au watagoma? 5 questions to answer!

Nina maswali matano juu ya sakata hili? Wala Sina maelezo mengi. Kwa ufupi, Serikali imetoa tangazo rasmi kwamba CHADEMA wanaweza kusaini kanuni za Uchaguzi hata sasa na kuingia kwenye Uchaguzi wa 2025.

Soma, Pia: Wakili Ado November: CHADEMA bado wanayo nafasi kutia saini kanuni za maadili

Nina maswali 5 ambayo sijapata jibu!!

1. Kwa nini Serikali imebadilisha msimamo wake sasa? Why now? Taarifa iliyotoka mwanzoni kutoka ofisi ya Msajili ni kwamba CHADEMA hawataruhusiwa kushiriki uchaguzi wo wote hata wa marudio hadi 2030. Nini kimetokea na kubadilisha msimamo huu wa awali? Nikapata swali lingine!

2. Je, Chadema watashiriki au hawatashiriki? Je, CHADEMA Wakigoma kushiriki Uchaguzi 2025, Serikali na CCM wataendelea kulegeza kamba na kufanya Reforms kidogo au watagoma na kuendelea na uchaguzi? Duuh! Nikapata swali lingine la 3 tena!

3. Je, CCM Wakiendelea bila Chadema nini kitatokea ukizingatia kwamba
Wanaotukopesha madola mengi sana ndo hao hao wanataka tuwe na Demokrasia kwa maana kwamba CHADEMA washiriki? Je, vyama hivi vidogo vitaufanya uchaguzi kuwa halali mbele ya macho ya kimataifa? Kumbe maswali hayaishi. Nikajiuliza swali la Nne!

4. Je, Uchaguzi ukifanyika na tukaamua kujitegemea kama Taifa huru (Sovereign state) bila kujali kama ulaya na Marekani wanataka au hawataki, Je, tunaweza kukaa bila wao au bila kukopa cho chote kutoka kwao kwa miaka mitano ijayo? Tunaweza kukabiliano na vikwazo vyao? Kumbuka marejesho yetu kwa mwezi ni Zaidi ya nusu ya makusanya ya Mwezi. Je, tunaweza kukaa bila kukopa kutoka kwao kwa miaka 5 ijayo? Swali la tano likaja, Kama Hilo haiwezekani!

5. Je, Tukiamua kujitegemea kwa Mbinde na kuamua kuitengeneza marafiki wapya (new alliance) na Waarabu, China na Urusi, Je, Hawa jamaa wanaweza wakatufikisha? Wanauwezo huo!? Nilipofika hapa sasa Kichwa kimeuma kwa sababu Kuna swali la Ziada! Nikakumbuka na waraka wa katoliki wa Juzi!

6 Je, Kwa nini wakatholiki wamekataa Viongozi wa vyama vya siasa, Chama tawala na Serikali kusimamia madhabahuni? Kwa nini sasa!? Kwa nini Leo?! What is in Between the line?
Je, nao wanashinikiza Reform za Lissu, Lema na Heche kwa njia hiyo!?

Je, Kuna madhehebu mengine ya Kikristo na kiislamu yenye msimamo huo hata kama hawajatoa waraka wao? Hata Mimi sijui!! Nini kifanyike?

Narudi kwako, Wewe unayetaka kucoment ndo ungekuwa Rais ungeamua kupatana na Chadema au ungefanyaje katika mazingira kama haya??

Unamwita Lissu na kukaa naye meza Moja au unakomaa mazingira kama haya?

Kwa heshima na unyenyekevu na uzalendo kwa Taifa langu nawasilisha kwa AJILI ya mjadala.
Dawa ni kufanya electoral reforms; hata hivyo, CCM na Serikali yake hawatakaa wafanye hivyo kwa hiari yao!
 
Huo ni mtego mkubwa wamewekewa CHADEMA!
CHADEMA wakomae na "No Reform No Election"!
Sasa hivi NRNE inapata support kubwa ndani (tena hata ndani ya Chama tawala);na nje ya Tanzania.
Nadhani not longer time to come,DDP anaweza kuachia Nolle!
Hamna kitu
 
No. 1. Serikali haijawarudisha ila ilijisahaulisha kwamba hakuna kifungu cha ukomo wa kusaini na wanajilaumu kwanini hawakuweka ukomo.
 
Tukisema CHADEMA ndio chama kikuu cha upinzani hawataki.... ila CHADEMA wakisema no, wanaanza kutafuta namna ya kuwarudisha mchezoni....

Walipokataa kuingia bungeni 2020, walitengeneza wabunge wao 19, ili mradi CHADEMA wawepo bungeni.
 
Kinachotakiwa na CDM ni nini haswa? Ni reforms, au ni kugomea uchaguzi? Kama ni reforms, kuna shida gani waka kaa mezani na kukubaliana reforms za muhimu kuwawezesha wao kushiriki uchaguzi? Migogoro yote duniani huisha kwa kuzungumza, kama hamtaki mazungumzo tunakuwa na wasiwasi mnachotaka ni nini?
Hakuna popote cdm walipogomea uchaguzi, bali wamegoma kusaini kanuni za uchaguzi zinazowabeba ccm. Ifahamike cdm wako tayari hata uchaguzi usogezwe mbele ili yafanyike mabadiliko ya kweli kwenye mfumo wetu wa uchaguzi. Ni kwanini ziwepo minimum reforms wakati walichokuwa wanadai ni tokea mama Samia kaingia madarakani hadi akaunda na kikosi kazi, achia mbali mikutano ya moja kwa moja ya ccm na cdm, na kote huko ilikuwa ni kupotezeana muda tu? Ama unataka kucheza na maneno ya kutufanya hatujui tutakacho ama tatizo liko wapi?
 
Mkuu hapana. Chadema iendelee kukaza kamba mpk ccm wakubali reforms zifanyike. Karibia kunakucha.
Wiki kama mbili, Kuna kaofisi flani nilisikia hii move..ila sikuamini

Sasa juzi naona inasemwa...ni kwamba miaka mitano ijayo mikopo na misaada itapungua..

Sasa na Serikali inavyopenda anasa na mikopo ..tayari wanataka kuirudisha CHADEMA kwenye game..

Na nimesikia reform zitafanyika mbili tuu... Kwenda Mahakamani kustaki matokeo ya Urais..
Na nyingine ni kuruhusu wakala wawe huru kidogo ..maana wengi hupigwa vibaya ndani ya chumba au kuzuiwa kuingia kwenye kituo mpaka saa nane mchana huku zoezi la kupiga kura likiwa limeshaanza Toka asubuhi
 
WANAWAJUA CHADEMA KUWA NI BLIND FOLDED...Watashikilia msimamo wa NO REFORM. Option ni Moja tu kwa CHADEMA: Wakatae offer na wakipotezee chama fursa au wakubali offer wachane na bango la No Reform washiriki uchaguzi
Unasema option ni moja kisha unaandika mbili ambazo zote ni fallacious.
 
Nina maswali matano juu ya sakata hili? Wala Sina maelezo mengi. Kwa ufupi, Serikali imetoa tangazo rasmi kwamba CHADEMA wanaweza kusaini kanuni za Uchaguzi hata sasa na kuingia kwenye Uchaguzi wa 2025.

Soma, Pia: Wakili Ado November: CHADEMA bado wanayo nafasi kutia saini kanuni za maadili

Nina maswali 5 ambayo sijapata jibu!!

1. Kwa nini Serikali imebadilisha msimamo wake sasa? Why now? Taarifa iliyotoka mwanzoni kutoka ofisi ya Msajili ni kwamba CHADEMA hawataruhusiwa kushiriki uchaguzi wo wote hata wa marudio hadi 2030. Nini kimetokea na kubadilisha msimamo huu wa awali? Nikapata swali lingine!

2. Je, Chadema watashiriki au hawatashiriki? Je, CHADEMA Wakigoma kushiriki Uchaguzi 2025, Serikali na CCM wataendelea kulegeza kamba na kufanya Reforms kidogo au watagoma na kuendelea na uchaguzi? Duuh! Nikapata swali lingine la 3 tena!

3. Je, CCM Wakiendelea bila Chadema nini kitatokea ukizingatia kwamba
Wanaotukopesha madola mengi sana ndo hao hao wanataka tuwe na Demokrasia kwa maana kwamba CHADEMA washiriki? Je, vyama hivi vidogo vitaufanya uchaguzi kuwa halali mbele ya macho ya kimataifa? Kumbe maswali hayaishi. Nikajiuliza swali la Nne!

4. Je, Uchaguzi ukifanyika na tukaamua kujitegemea kama Taifa huru (Sovereign state) bila kujali kama ulaya na Marekani wanataka au hawataki, Je, tunaweza kukaa bila wao au bila kukopa cho chote kutoka kwao kwa miaka mitano ijayo? Tunaweza kukabiliano na vikwazo vyao? Kumbuka marejesho yetu kwa mwezi ni Zaidi ya nusu ya makusanya ya Mwezi. Je, tunaweza kukaa bila kukopa kutoka kwao kwa miaka 5 ijayo? Swali la tano likaja, Kama Hilo haiwezekani!

5. Je, Tukiamua kujitegemea kwa Mbinde na kuamua kuitengeneza marafiki wapya (new alliance) na Waarabu, China na Urusi, Je, Hawa jamaa wanaweza wakatufikisha? Wanauwezo huo!? Nilipofika hapa sasa Kichwa kimeuma kwa sababu Kuna swali la Ziada! Nikakumbuka na waraka wa katoliki wa Juzi!

6 Je, Kwa nini wakatholiki wamekataa Viongozi wa vyama vya siasa, Chama tawala na Serikali kusimamia madhabahuni? Kwa nini sasa!? Kwa nini Leo?! What is in Between the line?
Je, nao wanashinikiza Reform za Lissu, Lema na Heche kwa njia hiyo!?

Je, Kuna madhehebu mengine ya Kikristo na kiislamu yenye msimamo huo hata kama hawajatoa waraka wao? Hata Mimi sijui!! Nini kifanyike?

Narudi kwako, Wewe unayetaka kucoment ndo ungekuwa Rais ungeamua kupatana na Chadema au ungefanyaje katika mazingira kama haya??

Unamwita Lissu na kukaa naye meza Moja au unakomaa mazingira kama haya?

Kwa heshima na unyenyekevu na uzalendo kwa Taifa langu nawasilisha kwa AJILI ya mjadala.
Mimi nafanya uliyouliza kwenye namba 5, bila kujali lolote, wakati mwingine nia njema kwa njia mbovu sio tatizo.
 
Tuwaombe chadema waridhie kuingia kwenye uchaguzi hivyo kwa sheria zilizopo hata kama hawatashinda ukweli utajulikana, wizi wa kura utakuwa wazi na udanganyifu mwingine utaonekana
CHADEMA ibaki hapo hapo isisumbuliwe.
 
Hujafanya homework yako, nadhani watu hawajaelewaaana ya Tume Huru. CHADEMA walishafutwa na Mwenyekiti alisema kama hawaridhiki waende Mahakamani. Ni nani kasema CHADEMA eamerudishwa? Kuhusu Wakatoliki, mlrngwa ni Katibu Mkuu wao, kada wa CHADEMA, Padre Kitima aliyejeruhiwa majuzijuzi kisiasa. Usisahau Kuna watu Wana makanisa "yao" kwa mfano Askofu Bagonza na Askofu Gwajima. Ukieazuia eatanaki na nini? Nyerere naMkapa naMagufuli wote ni Wakatoliki Wala hawashabikia sana Dini yao. Mara nyingi Viongozi la Dr Mpango au hata Rais Samia HUKARIBISHWA huwa hawajipeleki. Mlrngwa ni Kitima.
Hata mtu akivaa miwani ya dhahabu ili aelewa ulichoandika hapa hatoboi
 
Tuwaombe chadema waridhie kuingia kwenye uchaguzi hivyo kwa sheria zilizopo hata kama hawatashinda ukweli utajulikana, wizi wa kura utakuwa wazi na udanganyifu mwingine utaonekana
Hakuna ambacho hakijawahi kuonekana boss kwenye madai ya cdm. Labda useme washiriki kama fashion, lakini si kutaka proof ya uliyoyaainisha.
 
Kwani huyo wakili ndio msemaji wa tume? Tume ilisha kataa, na chama kimefungiwa, watasaini vipi
 
Asante kwa maswali yako mazito na yenye uzito mkubwa kwa hatma ya taifa letu.
Lakini hebu tuwe wakweli, huu mchezo wa serikali si jambo la kushangaza—ni mkakati wa kisiasa uliojaa unafiki, ujanja wa kimkakati, na hofu ya madhara ya kimataifa. Hebu tuchambue hoja kwa hoja Kama ambavyo umeukiza.

1. Kwa nini Serikali imebadilisha msimamo sasa?

Kwa sababu wamebanwa. Serikali haijabadilika kwa hiari, bali ni kwa shinikizo la ndani na nje ya nchi. Taarifa ya awali kwamba CHADEMA haitaruhusiwa hadi 2030 ilikuwa ni mbinu ya kuua upinzani kisiasa. Lakini baada ya kelele za ndani na mashinikizo kutoka jumuiya ya kimataifa, wameamua “kugeuza gia angani” ili kujionyesha mbele ya wahisani kuwa kuna demokrasia. Huu ni ujanja ujanja wa kisiasa wa kuokoa sura save face mbele ya wafadhili, siyo nia njema ya kuijenga nchi.

2. Je, CHADEMA washiriki au wasishiriki?

Swali hili linaumiza kichwa, lakini ukweli ni huu: Iwapo CHADEMA watashiriki bila reforms za msingi—hasa katiba mpya, tume huru ya uchaguzi, na uhuru wa vyombo vya habari—basi watakuwa wanalegitimize uchaguzi feki. Lakini wakigoma kushiriki, serikali itakuwa kwenye presha kubwa ya kimataifa. Hivyo, serikali inaweza kutumia mbinu za “kuwalambisha asali Kama wanalambishika” CHADEMA ili warudi mezani bila kuleta mabadiliko yoyote ya kweli. Ni mtego.
Kumbukuka mikutano ya wazee- Warioba, Butiku na Yule sura ya Gombe- Warioba alisema Chadema wakubari kurudi Kwa minimum reform- substantial reforms zifanyike baada ya uchaguzi. Inavyooneka , hiki ndicho Kinacho enda kutoea, hayo makesi yanayo washugulisha Chadema yatafufwa muda si mrefu. “Uchaguzi ni vita ya hoja” - kikwete. Kama hawataki hoja zijadiliwe, uchaguzi usio na hoja zilizo shiba upande wa pili, huo uchaguzi wanautaka wa nini ? Au ni kupoteza tu mali fedha za walipa kodi?

3. Je, uchaguzi bila CHADEMA ni halali kimataifa?
Hapana! Vyama vidogo haviwezi kufunika pengo la CHADEMA. Wafadhili hawadanganyiki. Uchaguzi usio na upinzani madhubuti hauna mashiko mbele ya macho ya mataifa makubwa. Hivyo, uchaguzi wa namna hiyo hautakuwa “free and fair”, bali ni “free for CCM only”. Ni propaganda tupu, na dunia itauona kama mchezo wa kuigiza.

4. Je, Tanzania inaweza kuishi bila misaada na mikopo ya Ulaya/Marekani?

Tuseme ukweli mchungu: Hatuwezi - period! Kumbuka Kwa sasa, Bajeti yetu ina zaidi ya 40% inayotegemea misaada na mikopo. Mwezi mmoja tu bila fedha za nje, serikali itaanza kukopa mishahara benki. Kama tungekuwa na uchumi wa ndani ulio huru na wenye tija, tungesema ndiyo. Lakini kwa sasa, ni ndoto ya mchana. Hatuna uhuru wa kiuchumi, hivyo kupingana na mataifa ya magharibi ni kujifukuzia adhabu za kiuchumi, hali ambayo itaua maisha ya wananchi wa kawaida.

5. Je, tukikimbilia China, Urusi na Waarabu, wataweza kutubeba?

Tujitazame kwenye kioo: China na Urusi wana maslahi yao binafsi. Hawana historia ya kusaidia mataifa masikini bila faida. Na pia, hawataki kukosoa udikteta. Kwa hiyo, tutakimbilia kule si kwa sababu wanatupenda, bali kwa sababu hawatuulizi kuhusu haki za binadamu. Hii si suluhisho la muda mrefu. Ni kama mtu aliyeachwa na mke wake anaamua kuoa kahaba kwa sababu “ Kahaba haulizi sana maswali”yeye ni fedha tu na muda mchache baada ya hapo - analivua na kulitupa gaguro lake ili akupozee maumivu lakini baada ya hapo ni kulio tupu - ni majuto moyoni, Mara kaswende, wasiwasi Kama umeukwaa ukimwi, gono, UTI etc.

6. Waraka wa Kanisa Katoliki: Kwa nini sasa?
Kwa sababu wameona udhalimu umepita kiasi. Madhabahu ni mahali pa haki na ukweli. Huwezi kuwa fisadi, dhalimu, muongo na mtesaji wa wanyonge, halafu ukapanda madhabahuni eti kutoa ushuhuda!

Ukweli ni kwamba, Kanisa Katoliki limechoshwa na unafiki. Wameamua kusema ukweli hata kama utauma. Naamini kuna madhehebu mengine pia yameanza kuona haya ya udhalimu, hata kama bado hawajatoa waraka rasmi.

Mimi ningefanyaje kama ningekuwa Rais?

Haraka sana,ningewaita hao CHADEMA, ACT, na wadau wengine mezani mara moja- Kama kikwete alivyo Fanta huko zamani. Nisingengoja hata dakika moja. Ningeanzisha maridhiano ya kweli, si ya maigizo. Ningeanza mchakato wa katiba mpya, tume huru ya uchaguzi, na uhuru wa bunge na mahakama. Kwa sababu haki haijengwi kwa mabavu bali kwa kusikiliza wote—hasa wale wanaopinga.

Maswali yako ni mazuri ya kizalendo. Lakini majibu hayaonyeshi udhaifu wa serikali tu, bali pia ukosefu wa ujasiri wa kisiasa katika kukubali ukweli na kushirikiana kwa ajili ya mustakabali wa taifa letu.

Ukomavu wa demokrasia si kuruhusu uchaguzi pekee, bali kuhakikisha kila mwananchi anaweza kushiriki kwa usawa, haki na amani.

#TaifaKwanza
#ReformZaKweliSiyoDanganyaToto
#DemokrasiaSiyoNeemaYaWachache
Kongole sana.
Umejibu maswali yote vizuri kabisa.
Mungu akubariki sana ndugu.

Kuongezea, mimi ningekuwa Rais, ningefanya hicho wanachotaka CHADEMA, kwani ni kwa faida kubwa ya nchi.
 
Ni kweli hoja ya msingi ni kama reforms zimefanyika au la, lakini pia ni muhimu kujadili namna ya kushinikiza mabadiliko hayo. Kukataa kushiriki uchaguzi bila kushiriki kabisa kwenye mchakato wa kudai reforms kunaweza kuacha nafasi kwa mfumo uleule kuendelea. Mkakati wa pamoja wa kisiasa, kushiriki majadiliano na kushinikiza kwa hoja ni njia bora ya kufanikisha mageuzi ya kweli.
Chadema wamesha goma kusanitize hii process,hawashiriki period.
 
Kinachotakiwa na CDM ni nini haswa? Ni reforms, au ni kugomea uchaguzi? Kama ni reforms, kuna shida gani waka kaa mezani na kukubaliana reforms za muhimu kuwawezesha wao kushiriki uchaguzi? Migogoro yote duniani huisha kwa kuzungumza, kama hamtaki mazungumzo tunakuwa na wasiwasi mnachotaka ni nini?
Serikali na CCM wanajua kinachopiganiwa na CHADEMA na Watanzania wote wenye mapenzi mema na nchi yao.
Kukaa tena kuzungumza juu ya nini tena!!??
Reforms zinazotakiwa zipo mezani zinajulikana kitambo.
 
Back
Top Bottom