Nina maswali matano juu ya sakata hili? Wala Sina maelezo mengi. Kwa ufupi, Serikali imetoa tangazo rasmi kwamba CHADEMA wanaweza kusaini kanuni za Uchaguzi hata sasa na kuingia kwenye Uchaguzi wa 2025.
Soma, Pia:
Wakili Ado November: CHADEMA bado wanayo nafasi kutia saini kanuni za maadili
Nina maswali 5 ambayo sijapata jibu!!
1. Kwa nini Serikali imebadilisha msimamo wake sasa? Why now? Taarifa iliyotoka mwanzoni kutoka ofisi ya Msajili ni kwamba CHADEMA hawataruhusiwa kushiriki uchaguzi wo wote hata wa marudio hadi 2030. Nini kimetokea na kubadilisha msimamo huu wa awali? Nikapata swali lingine!
2. Je, Chadema watashiriki au hawatashiriki? Je, CHADEMA Wakigoma kushiriki Uchaguzi 2025, Serikali na CCM wataendelea kulegeza kamba na kufanya Reforms kidogo au watagoma na kuendelea na uchaguzi? Duuh! Nikapata swali lingine la 3 tena!
3. Je, CCM Wakiendelea bila Chadema nini kitatokea ukizingatia kwamba
Wanaotukopesha madola mengi sana ndo hao hao wanataka tuwe na Demokrasia kwa maana kwamba CHADEMA washiriki? Je, vyama hivi vidogo vitaufanya uchaguzi kuwa halali mbele ya macho ya kimataifa? Kumbe maswali hayaishi. Nikajiuliza swali la Nne!
4. Je, Uchaguzi ukifanyika na tukaamua kujitegemea kama Taifa huru (Sovereign state) bila kujali kama ulaya na Marekani wanataka au hawataki, Je, tunaweza kukaa bila wao au bila kukopa cho chote kutoka kwao kwa miaka mitano ijayo? Tunaweza kukabiliano na vikwazo vyao? Kumbuka marejesho yetu kwa mwezi ni Zaidi ya nusu ya makusanya ya Mwezi. Je, tunaweza kukaa bila kukopa kutoka kwao kwa miaka 5 ijayo? Swali la tano likaja, Kama Hilo haiwezekani!
5. Je, Tukiamua kujitegemea kwa Mbinde na kuamua kuitengeneza marafiki wapya (new alliance) na Waarabu, China na Urusi, Je, Hawa jamaa wanaweza wakatufikisha? Wanauwezo huo!? Nilipofika hapa sasa Kichwa kimeuma kwa sababu Kuna swali la Ziada! Nikakumbuka na waraka wa katoliki wa Juzi!
6 Je, Kwa nini wakatholiki wamekataa Viongozi wa vyama vya siasa, Chama tawala na Serikali kusimamia madhabahuni? Kwa nini sasa!? Kwa nini Leo?! What is in Between the line?
Je, nao wanashinikiza Reform za Lissu, Lema na Heche kwa njia hiyo!?
Je, Kuna madhehebu mengine ya Kikristo na kiislamu yenye msimamo huo hata kama hawajatoa waraka wao? Hata Mimi sijui!! Nini kifanyike?
Narudi kwako, Wewe unayetaka kucoment ndo ungekuwa Rais ungeamua kupatana na Chadema au ungefanyaje katika mazingira kama haya??
Unamwita Lissu na kukaa naye meza Moja au unakomaa mazingira kama haya?
Kwa heshima na unyenyekevu na uzalendo kwa Taifa langu nawasilisha kwa AJILI ya mjadala.