Uchaguzi 2025, CHADEMA warudishwa uwanjani na serikali ya CCM, Je, CHADEMA watakubali au watagoma? 5 questions to answer!

Dawa ni kufanya electoral reforms; hata hivyo, CCM na Serikali yake hawatakaa wafanye hivyo kwa hiari yao!
 
Huo ni mtego mkubwa wamewekewa CHADEMA!
CHADEMA wakomae na "No Reform No Election"!
Sasa hivi NRNE inapata support kubwa ndani (tena hata ndani ya Chama tawala);na nje ya Tanzania.
Nadhani not longer time to come,DDP anaweza kuachia Nolle!
Hamna kitu
 
No. 1. Serikali haijawarudisha ila ilijisahaulisha kwamba hakuna kifungu cha ukomo wa kusaini na wanajilaumu kwanini hawakuweka ukomo.
 
Tukisema CHADEMA ndio chama kikuu cha upinzani hawataki.... ila CHADEMA wakisema no, wanaanza kutafuta namna ya kuwarudisha mchezoni....

Walipokataa kuingia bungeni 2020, walitengeneza wabunge wao 19, ili mradi CHADEMA wawepo bungeni.
 
Hakuna popote cdm walipogomea uchaguzi, bali wamegoma kusaini kanuni za uchaguzi zinazowabeba ccm. Ifahamike cdm wako tayari hata uchaguzi usogezwe mbele ili yafanyike mabadiliko ya kweli kwenye mfumo wetu wa uchaguzi. Ni kwanini ziwepo minimum reforms wakati walichokuwa wanadai ni tokea mama Samia kaingia madarakani hadi akaunda na kikosi kazi, achia mbali mikutano ya moja kwa moja ya ccm na cdm, na kote huko ilikuwa ni kupotezeana muda tu? Ama unataka kucheza na maneno ya kutufanya hatujui tutakacho ama tatizo liko wapi?
 
Mkuu hapana. Chadema iendelee kukaza kamba mpk ccm wakubali reforms zifanyike. Karibia kunakucha.
Wiki kama mbili, Kuna kaofisi flani nilisikia hii move..ila sikuamini

Sasa juzi naona inasemwa...ni kwamba miaka mitano ijayo mikopo na misaada itapungua..

Sasa na Serikali inavyopenda anasa na mikopo ..tayari wanataka kuirudisha CHADEMA kwenye game..

Na nimesikia reform zitafanyika mbili tuu... Kwenda Mahakamani kustaki matokeo ya Urais..
Na nyingine ni kuruhusu wakala wawe huru kidogo ..maana wengi hupigwa vibaya ndani ya chumba au kuzuiwa kuingia kwenye kituo mpaka saa nane mchana huku zoezi la kupiga kura likiwa limeshaanza Toka asubuhi
 
WANAWAJUA CHADEMA KUWA NI BLIND FOLDED...Watashikilia msimamo wa NO REFORM. Option ni Moja tu kwa CHADEMA: Wakatae offer na wakipotezee chama fursa au wakubali offer wachane na bango la No Reform washiriki uchaguzi
Unasema option ni moja kisha unaandika mbili ambazo zote ni fallacious.
 
Mimi nafanya uliyouliza kwenye namba 5, bila kujali lolote, wakati mwingine nia njema kwa njia mbovu sio tatizo.
 
Tuwaombe chadema waridhie kuingia kwenye uchaguzi hivyo kwa sheria zilizopo hata kama hawatashinda ukweli utajulikana, wizi wa kura utakuwa wazi na udanganyifu mwingine utaonekana
CHADEMA ibaki hapo hapo isisumbuliwe.
 
Hata mtu akivaa miwani ya dhahabu ili aelewa ulichoandika hapa hatoboi
 
Tuwaombe chadema waridhie kuingia kwenye uchaguzi hivyo kwa sheria zilizopo hata kama hawatashinda ukweli utajulikana, wizi wa kura utakuwa wazi na udanganyifu mwingine utaonekana
Hakuna ambacho hakijawahi kuonekana boss kwenye madai ya cdm. Labda useme washiriki kama fashion, lakini si kutaka proof ya uliyoyaainisha.
 
Kwani huyo wakili ndio msemaji wa tume? Tume ilisha kataa, na chama kimefungiwa, watasaini vipi
 
Kongole sana.
Umejibu maswali yote vizuri kabisa.
Mungu akubariki sana ndugu.

Kuongezea, mimi ningekuwa Rais, ningefanya hicho wanachotaka CHADEMA, kwani ni kwa faida kubwa ya nchi.
 
Chadema wamesha goma kusanitize hii process,hawashiriki period.
 
Serikali na CCM wanajua kinachopiganiwa na CHADEMA na Watanzania wote wenye mapenzi mema na nchi yao.
Kukaa tena kuzungumza juu ya nini tena!!??
Reforms zinazotakiwa zipo mezani zinajulikana kitambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…