Uchaguzi 2025, CHADEMA warudishwa uwanjani na serikali ya CCM, Je, CHADEMA watakubali au watagoma? 5 questions to answer!

Mkuu hongera sana kwa weledi wa kujibu hoja hongera sana...nimesoma nikiwa natembea barabarani nusura nigongwe na pikipiki hongera sana

Jamii forum inapaswa kuwa hivi
Asante ndugu yangu- pamoja- Tanzania i yetu sote, natamani sana CCM walitambue hili jambo kwamba hata kama ni cdm au Act, au cuf , sote ni Watanzania... hatupaswi kutengana kwa itikadi ya vyama. Yeyote atakaye shinda, kutokana na uchaguzu huru na haki- atangazwe na apewe ushirkiano.. ni hayo tu ndiyo yaliyo matamanio yangu.
 
Nilicomment hili mahala nikaishia tukanwa.

CHADEMA ilianzisha slogan kwabkutisha, matokeo yake wananchi wameikubali, sasa watarudi vipi kuwaaambia wananchi wanashiriki uchaguzi wakati hamna reforms zozote?
Hilo baba la kushiriki uchaguzi usio na reform halipo CCM wasahau TUNDU ANTIPAS LISSU na JOHN HECHE hawa watu ni tofauti na MBOWE na kundi lake,CCM watambue kwamba watanzania wamechoshwa na uchaguzi wa MAIGIZO tena wenye UCHAFU mwingi.NO REFORMS NO ELECTION NI GARI KUBWA LENYE UWEZO NA DAWA PEKEE KWA TAIFA LILILOKWAMA KIUONGOZI KAMA TANZANIA.
 
Pointi zako nzuri, ila ulipomwingiza JK tu, naona kumbe hujui kinafanyika nini na kiko nyuma ya nani. JK anataka mundelezo (continuity), hawazi kuwa hivyo bila ya puppet Samia. Wakati wa JPM JK alikuwa zizini kabanwa
 
Point of correction, No reforms No Election siyo ya Lissu, bali ya Chadema. Inaungwa mkono na binadamu yeyote anayependa ushindani wa haki.
 
We jamaa ni mjinga Rudi shule
 
Mazingira kama haya ndipo bwana AM alikuwa anapiga mpunga. Tayari angeshajaa bei na kujazwa kitita.
Chadema shikilieni hapo hapo.
 
Katibu mkuu hatambuliki na mahakama imepiga marufuku shughuli za chama sasa tunashiriki vipi huo uchaguzi
 
Aosee patamu hapo ni
no reforms no election dawa imeanza kufanya kazi
 
Bagonza ana kanisa gani acha upotoshaji wewe chawa
 
Bila reforms na kurekebisha kanuni za uchaguzi hao washindi wa Chadema hawawezi kitangazwa
 
Mamamammamaee Mahakama imewasaidia sana CCM na Serekali yake. Kwanza kuzuia mikutano na shughuli zote za chadema. Lissu kuwekwa mahabusu kwa kesi ya mchongo.
Wallah hawa wawili wangekuwa nje ccm ingeshatepeta kitambo kabisa. Maana spana zilivyokuwa zinapigwa lilikuwa jambo la muda tu.
 
Huyu kalala na kismati gin. Hana habari na tanzania ya leo.
 
Msajili wa vyama vya siasa alikataa kuitambua chadema, kwa kukataa kutambua uongozi halali wa chama hicho.

Kisha akaifutia ruzuku kwa kutokutambua uongozi mpya.

Mahakama imewazuia kushiriki siasa zote za majukwaani na online.

Sasa kwa akili yao nani anatakiwa aka sign hizo form za kushiriki uchaguzi ikiwa huwatambui viongozi wa chama, na hawaruhusiwi kushiriki siasa?

Je msajili atautambua uongozi wa chadema uliopo?

je mahakama itatoa zuio la kutokushiriki siasa?

Je msajili ata irejesha ruzuku?

Na vipi Tume imesahau kaulimbiu ya chama? kuhusu NO REFORMS NO ELECTION au wanajitia wazimu?
 
Aweda habari za siku nyingi, mimi nachangia hiyo namba 6 kwenye kipengere cha No Reforms, Ni hivi, No Reforms No Election ni mpango wa kila Mwananchi, hata wassira amenaswa mahali akizungumzia hilo.

Kwahiyo hilo si suala la Chadema au Wakatoliki tu, ni suala la Nchi nzima

Hata hivyo ccm inayoendeshwa na kikundi nje ya mfumo halali haitakubali reforms, hii ni kwa sababu katika uchaguzi huru na wa haki Samia hatopata hata 25% ya kura zote, hili Mamluki na Chawa wake wanalifahamu

Kwa kifupi ni kwamba, Chadema haitashiri huu uchaguzi ili kuepusha viongozi wake na wanachama kuuawa kama walivyouawa miaka yote.

CHADEMA ITAZUIA UCHAGUZI HUU
 
Yaani ni hivi - bila CDM kushiriki uchaguzi CCM waelewe atakayeshinda atatambulika hadi pale Lumumba tu.
Bila Reforms hakuna kitu kinaitwa uchaguzi wa October 25.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…