Mheshimiwa Susan Kiwanga na wenzake Monica Nsaro na Aisha Luja wameshindwa kurithi nafasi ya Halima Mdee ya mwenyekiti wa BAWACHA kitaifa. Kwa msingi huo, Sharifa ambaye ni kama makamu mwnyekiti wa Bawacha-Zanzibar, ndiye amechukua nafasi ya mheshimiwa Halima Mdee ya mwenyekiti wa Bawacha taifa kwa sasa.
View attachment 1789582
Pia, kamati tendaji ya BAWACHA, itajaza nafasi za katibu mkuu, naibu katibu mkuu wa Bara na Zanzibar, Katibu mwenezi taifa na makamu mwenyekiti wa bawacha Bara na zilizobakia kwa mujibu katiba,kanuni na sheria zinazoongoza Bawacha kwa ujumla.
View attachment 1789576
Fuatilia habari zaidi>>> kutoka Mwanza ni Matokeo ya Uchaguzi wa Bawacha taifa Mei-2021
Mbowe ana hulka fulani ya kuendesha chama kijasiriamali jasiriamali, yaani kifursa fursa.
Mwaka 2015 wakati katili Magu anagombea na Lowassa kulitokea mgawanyiko mkubwa sana. Kura zilipigwa kikanda na kikabila vibaya mno hasa kwa kanda ya kaskazini na Kanda ya Ziwa. Magu alikuwa anatumia hadi kisukuma kwenye majukwaa ya kampeni.
CHADEMA ilikuwa haiwezi kukosa viti vya ubunge mikoa ya Mwanza na Shinyanga, ila 2015 ilikosa kote isipokuwa Ukerewe na Mara.
Vivyo hivyo, CHADEMA ilizoa karibia viti vyote vya ubunge kanda ya kaskazini. Hadi majabali ya kisiasa kanda hiyo walipoteza ubunge.
Sasa ili kurudisha siasa za CHADEMA kanda ya ziwa, Mbowe akaona atafute Katibu Mkuu wa chama Msukuma ili am-neutralize "msukuma" Magu ndio akamuokota huko Mashinji. Ingawa matokeo hayakuwa kama Mbowe alivyotarajia.
Sasa leo kwakuwa Rais ni Mama Mzanzibar mvaa ushungi, kaona njia rahisi ni kumweka mbele Mmama, Mzanzibar.
Hapo hakuna demokrasia ya kura imetumika.
Siasa za Mbowe ni za kipuuzi sana. Ana misiasa ya ajabu sana kama Magufuli, na Sabaya.
Kuna kipindi alikuwa na mgogoro mkubwa sana Zitto kuhusu uenyekiti wa CHADEMA, akatafuta mzee fulani huko huko Kigoma ( anakotokea Zitto ) akamtumia kumchukulia fomu ya kugombea uenyekiti CHADEMA. Hii yote ni kuonesha kuwa licha ya kutofautiana na Zitto watu wa Kigoma wao wanampenda yeye Mbowe na CHADEMA na ndio wanaotaka Mbowe aendelee kuwa mwenyekiti wa chama. Huyo mzee haijulikani sasa hivi yuko wapi ?
Upuuzi gunia 100.