Mbowe ana hulka fulani ya kuendesha chama kijasiriamali jasiriamali, yaani kifursa fursa.
Mwaka 2015 wakati katili Magu anagombea na Lowassa kulitokea mgawanyiko mkubwa sana. Kura zilipigwa kikanda na kikabila vibaya mno hasa kwa kanda ya kaskazini na Kanda ya Ziwa. Magu alikuwa anatumia hadi kisukuma kwenye majukwaa ya kampeni.
CHADEMA ilikuwa haiwezi kukosa viti vya ubunge mikoa ya Mwanza na Shinyanga, ila 2015 ilikosa kote isipokuwa Ukerewe na Mara.
Vivyo hivyo, CHADEMA ilizoa karibia viti vyote vya ubunge kanda ya kaskazini. Hadi majabali ya kisiasa kanda hiyo walipoteza ubunge.
Sasa ili kurudisha siasa za CHADEMA kanda ya ziwa, Mbowe akaona atafute Katibu Mkuu wa chama Msukuma ili am-neutralize "msukuma" Magu ndio akamuokota huko Mashinji. Ingawa matokeo hayakuwa kama Mbowe alivyotarajia.
Sasa leo kwakuwa Rais ni Mama Mzanzibar mvaa ushungi, kaona njia rahisi ni kumweka mbele Mmama, Mzanzibar.
Hapo hakuna demokrasia ya kura imetumika.
Siasa za Mbowe ni za kipuuzi sana. Ana misiasa ya ajabu sana kama Magufuli, na Sabaya.
Kuna kipindi alikuwa na mgogoro mkubwa sana Zitto kuhusu uenyekiti wa CHADEMA, akatafuta mzee fulani huko huko Kigoma ( anakotokea Zitto ) akamtumia kumchukulia fomu ya kugombea uenyekiti CHADEMA. Hii yote ni kuonesha kuwa licha ya kutofautiana na Zitto watu wa Kigoma wao wanampenda yeye Mbowe na CHADEMA na ndio wanaotaka Mbowe aendelee kuwa mwenyekiti wa chama. Huyo mzee haijulikani sasa hivi yuko wapi ?
Upuuzi gunia 100.