Uchaguzi BAWACHA: Sharifa Suleiman aibuka kidedea Uenyekiti Taifa

Uchaguzi BAWACHA: Sharifa Suleiman aibuka kidedea Uenyekiti Taifa

Hawana bei kwenye kupigania nchi yao siyo kupigania CHADEMA.

Anyway, kama hujaliona hilo: Wamempa Mzanzibar ili apambane na Samia Mzanzibar.

Ni kama walivyowahi kuwapa wasukuma Pambalu na Mashinji ili wapambane na msukuma Magu.

Hakuna rocket science hapo wala kura zilizotumika.

Usishangae kabisa huyo dada ni mtiifu kwa ACT, huchelewi kusikia kahamia ACT mbeleni huko
 
Hawa wanafanya mzaha.Alietakiwa kuchukua mikoba ni Kiwanga au yule Mama mpiganaji kutoka Chato.
nbhy6543.jpg
765Eb.jpg
 
Kwa akili ya CHADEMA ( Mbowe ) ilivyo usishangae huyo ndio akagombea Urais 2025.
Na kwa akili za Maccm usishangae huyu mwanamke mzanzibar aliyerithi urais ndo atakuwa mgombea urais wao,
Nasema uongo!
 
Mbowe ana hulka fulani ya kuendesha chama kijasiriamali jasiriamali, yaani kifursa fursa.

Mwaka 2015 wakati katili Magu anagombea na Lowassa kulitokea mgawanyiko mkubwa sana. Kura zilipigwa kikanda na kikabila vibaya mno hasa kwa kanda ya kaskazini na Kanda ya Ziwa. Magu alikuwa anatumia hadi kisukuma kwenye majukwaa ya kampeni.

CHADEMA ilikuwa haiwezi kukosa viti vya ubunge mikoa ya Mwanza na Shinyanga, ila 2015 ilikosa kote isipokuwa Ukerewe na Mara.

Vivyo hivyo, CHADEMA ilizoa karibia viti vyote vya ubunge kanda ya kaskazini. Hadi majabali ya kisiasa kanda hiyo walipoteza ubunge.

Sasa ili kurudisha siasa za CHADEMA kanda ya ziwa, Mbowe akaona atafute Katibu Mkuu wa chama Msukuma ili am-neutralize "msukuma" Magu ndio akamuokota huko Mashinji. Ingawa matokeo hayakuwa kama Mbowe alivyotarajia.

Sasa leo kwakuwa Rais ni Mama Mzanzibar mvaa ushungi, kaona njia rahisi ni kumweka mbele Mmama, Mzanzibar.

Hapo hakuna demokrasia ya kura imetumika.

Siasa za Mbowe ni za kipuuzi sana. Ana misiasa ya ajabu sana kama Magufuli, na Sabaya.

Kuna kipindi alikuwa na mgogoro mkubwa sana Zitto kuhusu uenyekiti wa CHADEMA, akatafuta mzee fulani huko huko Kigoma ( anakotokea Zitto ) akamtumia kumchukulia fomu ya kugombea uenyekiti CHADEMA. Hii yote ni kuonesha kuwa licha ya kutofautiana na Zitto watu wa Kigoma wao wanampenda yeye Mbowe na CHADEMA na ndio wanaotaka Mbowe aendelee kuwa mwenyekiti wa chama. Huyo mzee haijulikani sasa hivi yuko wapi ?

Upuuzi gunia 100.
Mkuu vingi uliyoandika hapa umepotosha

1. 2015 ukanda uliletwa na CCM wala sio CHADEMA miaka yote mbona Mbowe hakuwahi pata wabunge wengi vile KLM au Arusha? Kma ni cha kikaskazini si wangekua wanabeba majimbo yote huko hata before 2015? Au huo uchagga umeanza alipokuja Lowassa tu?

2. Hyu mama alikua makam mwenyekiti na aligoma kwenda bungeni na kina Mdee so obvious Loyalty yake ndio imemfanya athibitishwe kuwa Mwenyekiti maana alikua ana kaimu muda wote toka January.

3. Kuhusu zitto sio kweli eti Mbowe alihitaji endorsement ya Mzee wa Kiha!! Yule mzee alikua muasisi na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee na alikua anasema wazi kabisa hamuungi mkono Zitto.

Watu ambao hampo kigoma mnadhani zitto alikuwa invicible huko si kweli. Kigoma kaskazini alikataliwa kabisa so ili kuokoa ubunge ikabidi aingie dili na CCM kwamba Serukamba aende huko kalinzi-Matyazo then yeye agombee Ujiji.

Kingine mama yake zitto alibaki CHADEMA all through na hakuwahi kuyumba hata mwanaye alipojitoa. Sasa kwa loyalty ya mama mzazi wa zitto bado Mbowe alihitaji endorsement ya mzee wa Kigoma??
 
Chama cha wachagga/kaskazini kimebakia jina tu 😄 wachagga hamuwezi uongozi mnalazimisha tu.


Sasa ndio inapotea mazima, na huko znz huenda wakabadilisha na jina, sio chadema tena.
 
Acha wivu wa kike
Aki li ndogo inakuja kutawala akili kubwa!

kweli BAWACHA walipania kuvunja genge la MBOWE na MNYIKA.

Tanzania bara ndio yenye wapiga kura wengi ndani ya BAWACHA ajabu wamempa mzanzibari SHARIFFA ambaye kule Zanzibar CHADEMA ni kama haipo wakawapiga chini wagombea wazito wa bara!
 
Mheshimiwa Susan Kiwanga na wenzake Monica Nsaro na Aisha Luja wameshindwa kurithi nafasi ya Halima Mdee ya mwenyekiti wa BAWACHA kitaifa. Kwa msingi huo, Sharifa ambaye ni kama makamu mwnyekiti wa Bawacha-Zanzibar, ndiye amechukua nafasi ya mheshimiwa Halima Mdee ya mwenyekiti wa Bawacha taifa kwa sasa.
View attachment 1789582
Pia, kamati tendaji ya BAWACHA, itajaza nafasi za katibu mkuu, naibu katibu mkuu wa Bara na Zanzibar, Katibu mwenezi taifa na makamu mwenyekiti wa bawacha Bara na zilizobakia kwa mujibu katiba,kanuni na sheria zinazoongoza Bawacha kwa ujumla.

View attachment 1789576

Kiwanga ashindwa kumrithi Mdee, Sharifa achukua mikoba

Masalu Erasto

SUSAN Kiwanga na wenzake wawili, wameshindwa kurithi nafasi ya Halima Mdee ya Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bawacha). Anaripoti Regina Mkonde,

Mbali na Kiwanga, wengine ni Monica Nsaro wa Tabora na Aisha Luja wa Singida ambao walijitosa kuchukua fomu za kuwania kukaimu nafasi hiyo iliyoachwa na Mdee.

Kiwanga ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, aliyewahi kuwa mbunge wa Mlimba, Mkoa wa Morogoro kwa pamoja, wameshindwa kushika wadhifa huo kwa mujibu wa Katiba ya Chadema.
Badala yake, Kamati tendaji ya Bawacha, inakutana kesho Jumanne tarehe 18 Mei 2021, jijini Mwanza kwa ajili ya kujaza nafasi za katibu mkuu, naibu katibu mkuu Bara, naibu katibu mkuu Zanzibar, katibu mwenezi na makamu mwenyekiti wa Bawacha-Bara.

Nafasi hizo, zinajazwa baada ya kamati kuu ya Chadema, tarehe 27 Novemba 2020, kufukuzwa uanachama, kwa tuhuma za usaliti, kughushi nyaraka za chama kisha kujipeleka bungeni Dodoma kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum.

Nafasi zingine ambazo zinajatwa ni; katibu mkuu, naibu katibu mkuu bara na Zanzibar na mratibu wa uenezi.
Sharifa Suleiman, Makamu Mwenyekiti wa Bawacha-Zanzibar

Nafasi ya mwenyekiti na makamu mwenyekiti Bara ambazo wanachama wa Chadema walijitosa kuchukua fomu, zimewekwa kando kutokana na Katiba ya Chadema, kutokuonyesha, ikiwa nafasi ya mwenyekiti itakuwa wazi, kutafanyika uchaguzi wa kuijaza.

Hoja hii imepata mashiko na kilichotokea kwa Baraza la Vijana la Chadema, (Bavicha), wakati aliyekuwa mwenyekiti wake, Patrobas Katambi alipotimkia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Novemba 2017, Patrick Ole Sosopi, aliyekuwa makamu mwenyekiti-Bara wa baraza hilo, alithibitishwa na kamati tendaji kuwa mwenyekiti.

Kwa msingi huo, Sharifa Suleiman ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Bawacha-Zanzibar, ndiye amechukua nafasi ya Mdee ya Mwenyekiti wa Bawacha.

Nafasi ya makamu mwenyekiti wa Bawacha-Bara na Zanzibar, watateuliwa miongoni mwa wajumbe wa kamati tendaji inayoundwa na wenyeviti na makatibu wa mikoa pamoja na wajumbe wa kamati kuu ambao ni wanawake.
Halima Mdee
Ndiyo maana, taarifa iliyotolewa juzi Jumamamosi na Singo Kigaila Benson, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema-Bara, kuhusu kujazwa kwa nafasi hiyo za Bawacha, hakuna wagombea wa nafasi ya mwenyekiti na makamu mwenyekiti.
Kigaila alisema, kamati kuu ya chama hicho, iliyokutana kwa njia ya mtandao, ilijadili na kuteua wagombea ambapo nafasi ya katibu mkuu walioteuliwa ni; Asia Msangi, Catherine Rugen a Esther Daffi.
Naibu katibu mkuu Bara wako watatu; Brenda Jonas, Emma Boki na Nuru Ndosi huku upande wa Zanzibar kwa nafasi hiyo akiwa mmoja, Bahati Haji.

Mratibu mwenezi wa Bawacha wako watatu ambao ni; Aisha Ame, Husna Said na Singrada Mligo.
Mbali na Mdee aliyekuwa mwenyekiti wa baraza la wanawake wa Chadema (Bawacha), wengine ni, waliokuwa wajumbe wa Kamati Kuu, Ester Bulaya na Esther Matiko, pamoja na aliyekuwa katibu mkuu wa Bawacha, Grace Tendega.

Katika orodha hiyo, wamo pia Hawa Subira Mwaifunga, aliyekuwa makamu mwenyekiti wa Bawacha (Bara); Agnesta Lambat, aliyekuwa katibu mwenezi na Asia Mwadin Mohamed, aliyekuwa naibu katibu mkuu wa Bawacha Zanzibar na Katibu Mkuu, Bawacha-Bara, Jesca Kishoa.

Pia, aliyekuwa katibu mkuu wa Baraza la Vijana (Bavicha), Nusrat Hanje na aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema mkoani Mtwara, Tunza Malapo.

Wengine waliofukuzwa Chadema, Cecilia Pareso, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Salome Makamba, Anatropia Theonest, Conchesta Lwamlaza, Felister Njau na Stella Siyao.
Suzan Kiwanga alikuwa na kiherehere utadhani keshachaguliw kushika mikoba ya BAWACHA
 
Aki li ndogo inakuja kutawala akili kubwa!

kweli BAWACHA walipania kuvunja genge la MBOWE na MNYIKA.

Tanzania bara ndio yenye wapiga kura wengi ndani ya BAWACHA ajabu wamempa mzanzibari SHARIFFA ambaye kule Zanzibar CHADEMA ni kama haipo wakawapiga chini wagombea wazito wa bara!
Ila ni sahihi ccm kumteua mama Samia kuwa mwenyekiti wa chama wakati anatoka Zanzibar yenye wapiga kura 100k tu kwa ccm ?
 
Ila ni sahihi ccm kumteua mama Samia kuwa mwenyekiti wa chama wakati anatoka Zanzibar yenye wapiga kura 100k tu kwa ccm ?


1621353394391.png


Kuna tofauti ipi ya aliyekuwa Makamu wa Rais mama Samia; kuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ? Muda ukifika tutaelewa watanzania hatua kwa hatua na kujifunza kwa wengine katika jamii.

1621353334804.png
 
Mkuu vingi uliyoandika hapa umepotosha

1. 2015 ukanda uliletwa na CCM wala sio CHADEMA miaka yote mbona Mbowe hakuwahi pata wabunge wengi vile KLM au Arusha? Kma ni cha kikaskazini si wangekua wanabeba majimbo yote huko hata before 2015? Au huo uchagga umeanza alipokuja Lowassa tu?

2. Hyu mama alikua makam mwenyekiti na aligoma kwenda bungeni na kina Mdee so obvious Loyalty yake ndio imemfanya athibitishwe kuwa Mwenyekiti maana alikua ana kaimu muda wote toka January.

3. Kuhusu zitto sio kweli eti Mbowe alihitaji endorsement ya Mzee wa Kiha!! Yule mzee alikua muasisi na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee na alikua anasema wazi kabisa hamuungi mkono Zitto.

Watu ambao hampo kigoma mnadhani zitto alikuwa invicible huko si kweli. Kigoma kaskazini alikataliwa kabisa so ili kuokoa ubunge ikabidi aingie dili na CCM kwamba Serukamba aende huko kalinzi-Matyazo then yeye agombee Ujiji.

Kingine mama yake zitto alibaki CHADEMA all through na hakuwahi kuyumba hata mwanaye alipojitoa. Sasa kwa loyalty ya mama mzazi wa zitto bado Mbowe alihitaji endorsement ya mzee wa Kigoma??
Amejaza kelele tu kwenye huu uzi, hana hoja.
 
Mbowe na genge lake ndio walimchagua Mashinji,

Katika hilo genge usimsahau Lowasa

Ni sawa, ila kutenda kosa si kosa bali kurudia Kosa. Kwa sasa wakiokota takataka nyingine tena toka ccm na kuipa madaraka, tutajuana tabia.
 
1621370275112.png

Wajumbe wa Kamati Tendaji ya Bawacha, leo Jumanne, wamemchagua, mheshimiwa Catherine Ruge, kuwa Katibu Mkuu wa Baraza hilo kwa kura 34 sawa na asilimia 52.6, akifuatiwa na Esther Daffi kura 23 na Asia Msangi kura nane.

1621370560373.png


Hivyo, anachukua nafasi ya mheshimiwa Grace Tendega aliyefukuzwa uanachama na wenzake 18.
 
Naibu Katibu Bawacha Taifa (Bara) Nuru Elias Ndosi
1621370772702.png
Matokeo ya uchaguzi nafasi ya Naibu Katibu Bawacha Taifa (Bara):-
1. EMA Theobald Boki - kura 15 2. Brenda Jonas - kura 17 3. Nuru Ndosi - kura 36
 
Back
Top Bottom