Uchaguzi bila katiba mpya wa nini?

Uchaguzi bila katiba mpya wa nini?

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Huko Zanzibar mambo ndiyo kama hivi:

Ya nini kufanya uchaguzi bila katiba mpya? Si heri kuwaacha CCM kama ndivyo waendelee tu kulamba asali kwa raha zao?

Insanity is doing the same thing over and over and expecting different results.”

Asema Einstein.

NB: Tume Huru bila Katiba Mpya ni kuendekeza ubatili ule ule.

===

ACT Wazalendo walalamikia uchaguzi mdogo wa jimbo la Amani, lililopo Mkoa wa Mjini Magharibi kuwa umegubikwa na udanganyifu.

Kiongozi wa ACT amesema wapiga kura hewa ambao ni watu wa nje ya jimbo la Amani na marehemu wamepiga kura katika jimbo hilo huku wapiga kura halali wakizuiwa kupiga kura katika jimbo hilo.
 
Huwezi pata katiba mpya kwa hii siasa majitaka..inabd kuwe na vyombo huru
 
Sitokuja kupiga tena kura chini ya hii Katiba mbovu ya ccm ya mwaka 1977! Enough is enough.

Nakumbuka nilipiga kura kwa mara ya mwisho 2015. Na kamwe sijutii! No Katiba Mpya ya Wananchi, no kupiga kura.

CCM wanaowapinga wasipopiga kura huhesabu ushindi wa kishindo.

Tunahitaji Movement ya kudai katiba mpya. Hii haiwezi kuja kama mvua. Hiyo inahitaji uongozi, mkakati na agenda moja ya wazi - Katiba mpya.
 
Haya ni matunda ya mfumo mbovu alioujenga Nyerere
Sio sahihi kumuangushia mzigo huu Mwalimu kwasababu yeye alifanya yake kwa wakat wake na katiba ya hovyo iliwekwa kipind kile ambayo ni chama kimoja na sio ya vyama vingi, na baada yake waliokua na dhamana walipaswa kulifanyia kaz na sio mstaafu aje alifanyie kaz!!
 
CCM hawataki hilo litokee. Lengo lao kuendelea kulamba asali wao na familia zao.

Madiliko ya katiba hayawezi kuja au kuwa kwa hisani ya CCM.
Ni kweli unachosemq mabadiliko ya katiba kwa serikali ya CCM ni ndoto
 
Ni kweli unachosemq mabadiliko ya katiba kwa serikali ya CCM ni ndoto

Movement iliyodhamiria kudai katiba mpya kama agenda pekee ndicho kinaweza kuwalazimisha kufanya tunachotaka. Hawa si wa kuwaomba kuwarai au kuwalilia.
 
Movement iliyodhamiria kudai katiba mpya kama agenda pekee ndicho kinaweza kuwalazimisha kufanya tunachotaka. Hawa si wa kuwaomba kuwarai au kuwalilia.
Izo movement pia znapigwa vita sana..hakuna uhuru wa kujieleza na vyombo kama mahakama havifanyi kazi kwa uhuru na transparency
 
Izo movement pia znapigwa vita sana..hakuna uhuru wa kujieleza na vyombo kama mahakama havifanyi kazi kwa uhuru na transparency

Movement si ruksa yao. Tukisubiri ruksa kutoka kwa walamba asali Ili kuwatatiza wao kulamba asali mbona tutasubiri milele?
 
Kumlaumu marehemu kwenye hili rojo tulilomo ni kujilisha upepo tu.

Kwani @ACT na wenzao kwenye hizi chaguzi wanategemea nini? Kwa nini tusiunganishe nguvu kudai katiba mpya kwanza?
ACT wako busy kuzunguka baadhi ya maeneo kutafta maon kuwa wajitoe au wasijitoe kwenye serikali yao ya umoja wa kitaifa huko zanzibar wakiambiwa na chadema wapiganie katiba mpya wao macho yao yako kwenye serikali fake ya umoja wa kitaifa.
 
Haieleweki ACT wanataka nini. Kwa hakika hawa wanatuchelewesha sana:

IMG_20221217_174044_120.jpg

Cc: Abdul Nondo ACT Wazalendo
 
Back
Top Bottom