Uchaguzi bila katiba mpya wa nini?

Uchaguzi bila katiba mpya wa nini?

Wapinzani nao hawajielewi

Ova

Lawama zao kwa wananchi kuwa hawaandamani. Kwani wananchi ni nani na kipi kinaweza kufanyika bila uongozi, organization au coordination?

Iko kama Kila mtu anamtegea mwingine. Wote matunda wanataka tatizo kuyapigania.
 
Sio sahihi kumuangushia mzigo huu Mwalimu kwasababu yeye alifanya yake kwa wakat wake na katiba ya hovyo iliwekwa kipind kile ambayo ni chama kimoja na sio ya vyama vingi, na baada yake waliokua na dhamana walipaswa kulifanyia kaz na sio mstaafu aje alifanyie kaz!!
Nyerere ndiye alivifungia vyama pinzani na kuondosha Bunge kumwajibisha raisi , akaweka katiba hii inayomfanya Raisi kuwa mfalme
 
Nyerere ndiye alivifungia vyama pinzani na kuondosha Bunge kumwajibisha raisi , akaweka katiba hii inayomfanya Raisi kuwa mfalme
Lkn waliopaswa kuweka mamb saw na waliofuata haiwezekan kuendeleza kosa wakat mnaweza rekebisha, pia katiba iliyopo iliandikwa kwaajil ya chama kimoja na sio vyama vingi!!
 
ACT wanamlalamikia Nani?

Hakuna maelezo mazuri kuwahusu kuliko haya:

IMG_20221217_211317_380.jpg

NInakazia.

Cc: Abdul Nondo ACT Wazalendo
 
Sio sahihi kumuangushia mzigo huu Mwalimu kwasababu yeye alifanya yake kwa wakat wake na katiba ya hovyo iliwekwa kipind kile ambayo ni chama kimoja na sio ya vyama vingi, na baada yake waliokua na dhamana walipaswa kulifanyia kaz na sio mstaafu aje alifanyie kaz!!
Kwa nini alipiga marufuku vyama vingi wakati wa utawala wake?
 
Lkn waliopaswa kuweka mamb saw na waliofuata haiwezekan kuendeleza kosa wakat mnaweza rekebisha, pia katiba iliyopo iliandikwa kwaajil ya chama kimoja na sio vyama vingi!!

Wataweka vipi sawa na Baba ndio kawakusanya walafi na kawawekea njia ya kunywa na si kulamba asali 😛
😛
 
Huko Zanzibar mambo ndiyo kama hivi:

View attachment 2449796

Ya nini kufanya uchaguzi bila katiba mpya? Si heri kuwaacha CCM kama ndivyo waendelee tu kulamba asali kwa raha zao?

Insanity is doing the same thing over and over and expecting different results.”

Asema Einstein.

NB: Tume Huru bila Katiba Mpya ni kuendekeza ubatili ule ule.

Hakuna katiba mpya ama tume huru bila machafuko. Kenya walituonyesha ukweli huu kwa vitendo. Kinyume na hapo kutakuwa na vikao vya maridhiano, lakini hakutakuwa na uhuru wa kufanya siasa kwa wapinzani, na ukitokea uchaguzi uporaji utaendelea kuwa huu huu. CCM wanajua fika kwenye uchaguzi wa halali hawashindi. Ni sisi wenyewe kuamua kusuka ama kunyoa
 
Vitakuja wakati ambao na wao CCM wakianza kufa, Kuibiwa , kunajisiwa na kufanyiwa vitendo vyote vichafu ambavyo wao huwafanyia wenzao

Huu ndio ukweli ambao wengi wanaogopa kuusema. Kama CCM wataendelea kupora chaguzi na wanaendelea kukaa madarakani bila bugudha, tusitegemee lolote kwenye vikao vya kitapeli vya maridhiano.

Kama watu wanaogopa kuleta machafuko ambayo ni njia sahihi na yenye matokeo ya haraka. Basi tuanze kususiana kwenye shughuli za kijamii mfano misiba, sherehe, michezo, ibada nk. Njia hizi za utengano kwenye jamii ni ya amani lakini itakayotoa majibu, hata kama ni kwa kuchelewa. Mfano ukiwa kwenye nyumba ya ibada akiingia mwanaccm mnatoka mnamuachia, hakuna kwenda kununua bidhaa kwenye biashara ya mwanaccm labda iwe haikwepeki. Hakuna kuhudhuria msiba au sherehe ya mwanaccm yoyote. Na ujumbe uwe wazi, hatuwezi kushirikiana kama hamjali umuhimu wa katiba mpya. Ila machafuko ndio njia yenye matokeo ya haraka.
 
Lkn waliopaswa kuweka mamb saw na waliofuata haiwezekan kuendeleza kosa wakat mnaweza rekebisha, pia katiba iliyopo iliandikwa kwaajil ya chama kimoja na sio vyama vingi!!

Waliofuata baada ya msingi wake ndio hawa hawataki mabadiliko ya hiyo katiba. Alipokuwa madarakani aliwahi kukiri katiba hii sio ya watu wasio waadilifu. Na kabla ya kuachia uenyekiti wa CCM aliona jinsi warithi wake wasivyo na maadalili. Kibaya zaidi yeye mwenyewe akageuka kuwe muasisi wa wizi wa kura nchi hii ili CCM iendelee kubaki madarakani. Rejea uchaguzi wa 1995 huko Zanzibar.
 
Hakuna katiba mpya ama tume huru bila machafuko. Kenya walituonyesha ukweli huu kwa vitendo. Kinyume na hapo kutakuwa na vikao vya maridhiano, lakini hakutakuwa na uhuru wa kufanya siasa kwa wapinzani, na ukitokea uchaguzi uporaji utaendelea kuwa huu huu. CCM wanajua fika kwenye uchaguzi wa halali hawashindi. Ni sisi wenyewe kuamua kusuka ama kunyoa

Inategemea una tafsiri gani kuhusu machafuko.

Maandamano na mikutano ya siasa siyo machafuko. Hayo ni kwa mujibu wa katiba yatatuvusha salama.

Angalizo: wasipewe nafasi kumbatiza mtu ugaidi.
 
Waliofuata baada ya msingi wake ndio hawa hawataki mabadiliko ya hiyo katiba. Alipokuwa madarakani aliwahi kukiri katiba hii sio ya watu wasio waadilifu. Na kabla ya kuachia uenyekiti wa CCM aliona jinsi warithi wake wasivyo na maadalili. Kibaya zaidi yeye mwenyewe akageuka kuwe muasisi wa wizi wa kura nchi hii ili CCM iendelee kubaki madarakani. Rejea uchaguzi wa 1995 huko Zanzibar.

Hatupaswi kumlaumu mtu kwa hali iliyopo bali kujilaumu sisi wenyewe kwa kuwaachia watu Hawa kulamba asali kwa muda wote huu.

Anasema Messiah: "Msinililie mimi bali mjililie wenyewe."

Tuamke tuchukue hatua.
 
Inategemea una tafsiri gani kuhusu machafuko.

Maandamano na mikutano ya siasa siyo machafuko. Hayo ni kwa mujibu wa katiba yatatuvusha salama.

Angalizo: wasipewe nafasi kumbatiza mtu ugaidi.

Sina popote ninaposema maandamano na mikutano ni machafuko maana hizo ni shughuli halali. Njia hizi zimepigwa marufuku sasa unategemea nini?

Kuitwa gaidi haikwepeki kwa watu wanaolinda madaraka haramu. Hata Mandela aliitwa gaidi huko Afrika kusini, je ni kweli alikuwa gaidi?
 
Haya ni matunda ya mfumo mbovu alioujenga Nyerere
Tutaendelea kumbembesha Nyerere gunia la misumari ya kisiasa hadi lini? Je, hoja yako ni kwamba kizazi chetu hiki akili zimedumaa au vipi
 
Back
Top Bottom