- Thread starter
- #41
Sina popote ninaposema maandamano na mikutano ni machafuko maana hizo ni shughuli halali. Njia hizi zimepigwa marufuku sasa unategemea nini?
Kuitwa gaidi haikwepeki kwa watu wanaolinda madaraka haramu. Hata Mandela aliitwa gaidi huko Afrika kusini, je ni kweli alikuwa gaidi?
Umetumia neno machafuko:
"Kama watu wanaogopa kuleta machafuko ambayo ni njia sahihi na yenye matokeo ya haraka."
Ukakazia:
"Ila machafuko ndio njia yenye matokeo ya haraka."
Maneno yangu kwako ni kuwa sijui unatumia neno hilo kwa maana ipi? Kwa maana kususia jambo si machafuko.
Tudaini mabadiliko kwa amani. Kupitia mikutano, maandamano na migomo hayupo mwenye kutushtaki popote. Hayo ni kwa mujibu wa katiba na kwenye hayo tunawamudu.
Post #31 haya ni machafuko. Machafuko ni ugaidi hauna nafasi popote duniani.