CHADEMA ‘yapeleka' mamluki wa Tarime kuifanyia fujo CCM Busanda
Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Geita; (Habarileo)
Habari zinazosomwa zaidi:
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimedaiwa kuingiza katika Jimbo la Busanda vijana takribani 70 kutoka wilayani Tarime kwa ajili ya kutisha watu na kuzomea viongozi katika mikutano ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Shutuma hizo zilitolewa jana mjini hapa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CCM, Matson Chizi kuwa vijana hao kutoka mkoani Mara, wamepelekwa katika kata kadhaa za jimbo hilo.
Kwa mujibu wa Chizi, taarifa walizonazo zinaonyesha kwamba vijana hao wapo katika kata za Nyarugusu, Bukoli, Katoro na kwamba wengine wameweka makazi katika Mji wa Geita uliopo takribani kilometa 70 kutoka jimbo la Busanda.
Alisema, moja ya matukio yaliyofanywa na vijana hao, lilitokea juzi katika mkutano wa CCM uliofanyika Nyarugusu, ambapo Chizi anadai kundi lilikaa pembezoni mwa mkutano huo wakionyesha alama ya vidole viwili.
Alisema vijana hao waliwasili wilayani Geita kabla ya kampeni kuanza. Miongoni mwa shutuma zinazotolewa ni kwamba vijana hao wamekuwa wakiwatukana wana CCM wanaopita njiani wakiwa wamevalia sare za chama.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM (Bara) John Malecela aliwataka wana CCM kutohofu chochote kwa kuwa serikali imeshaahidi kutoa ulinzi kwa vyama vyote na kuhakikisha hakuna vurugu.
Gazeti hili halikuweza kuwapata viongozi wa CHADEMA kuzungumzia shutuma hizo baada ya simu ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Wilbrod Slaa na ya Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe kuita bila kupokewa.
Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Geita, ASP Kimea alisema Jeshi hilo linafanya uchunguzi wa tuhuma hizo na akasema limejipanga vyema kukabili yeyote atakayeleta vurugu katika kampeni na kwenye uchaguzi utakaofanyika Mei 24, mwaka huu.
Hivi unajua Field Marshall kuna vitu fulani vidogo vidogo vinakupita?
Utawezaje kutamka kwamba Msekwa aliacha Ubunge halafu akaendelea kuwa spika?
Bila hata kuhitaji kuwa mtaalam wa Ibara ya 86 (1) ya Katiba au Parliamentary Standing Orders Ibara ya 7(2), hivi huwezi tu kujiuliza mwenyewe, Spika atakuwaje sio Mbunge? Utaokotaje mtu mtaani aje kugombea u-Uspika? Ataingiaje?
Sasa kama hujui vitu vidogo vidogo kama hivyo utawezaje kujua timbwili la Msekwa na Mongella?
CHADEMA yapeleka mamluki wa Tarime kuifanyia fujo CCM Busanda
Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Geita; (Habarileo)
1. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimedaiwa kuingiza katika Jimbo la Busanda vijana takribani 70 kutoka wilayani Tarime kwa ajili ya kutisha watu na kuzomea viongozi katika mikutano ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Shutuma hizo zilitolewa jana mjini hapa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CCM, Matson Chizi kuwa vijana hao kutoka mkoani Mara, wamepelekwa katika kata kadhaa za jimbo hilo.
2. Kwa mujibu wa Chizi, taarifa walizonazo zinaonyesha kwamba vijana hao wapo katika kata za Nyarugusu, Bukoli, Katoro na kwamba wengine wameweka makazi katika Mji wa Geita uliopo takribani kilometa 70 kutoka jimbo la Busanda.
3. Alisema, moja ya matukio yaliyofanywa na vijana hao, lilitokea juzi katika mkutano wa CCM uliofanyika Nyarugusu, ambapo Chizi anadai kundi lilikaa pembezoni mwa mkutano huo wakionyesha alama ya vidole viwili.
4. Alisema vijana hao waliwasili wilayani Geita kabla ya kampeni kuanza. Miongoni mwa shutuma zinazotolewa ni kwamba vijana hao wamekuwa wakiwatukana wana CCM wanaopita njiani wakiwa wamevalia sare za chama.
5. Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM (Bara) John Malecela aliwataka wana CCM kutohofu chochote kwa kuwa serikali imeshaahidi kutoa ulinzi kwa vyama vyote na kuhakikisha hakuna vurugu.
6. Gazeti hili halikuweza kuwapata viongozi wa CHADEMA kuzungumzia shutuma hizo baada ya simu ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Wilbrod Slaa na ya Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe kuita bila kupokewa.
7. Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Geita, ASP Kimea alisema Jeshi hilo linafanya uchunguzi wa tuhuma hizo na akasema limejipanga vyema kukabili yeyote atakayeleta vurugu katika kampeni na kwenye uchaguzi utakaofanyika Mei 24, mwaka huu.
- Dilunga wewe ndio unahitaji kwenda kusoma tena historia, ni kwamba Msekwa hajawahi kushindwa kura za maoni na Mama Mongella, it never happened,
- Alipogombea u-Spika na Akukweti na Sita, Msekwa hakuwa mbunge meaning kwamba angeshinda angeendelea kua Spika bila ya kuwa mbunge, sasa kasome tena hizo sheria zako zilianza kutumika lini,
- Mama Mongella amewahi kumshinda mshikaji wangu mmoja anaitwa Kamando kwenye kura za maoni sio Msekwa.
Respect.
FMES!
Waishia kuzomea na media zitashangilia, lakini mwisho wa siku CCM itashinda period!
Mtanzania,
Hiyo habari haina any other independent source except mkurugenzi wa uchaguzi wa CCM? Polisi wamesemaje? Unajua gharama ya kuwasafirisha vijana sabini kutoka Tarime na kuwatunza ugenini? Kama CHADEMA wana hela kama hizo za kuchezea ningewashauri wazitumie kwa umakini zaidi.
- Mkuu Jasusi, mbona inapokuja masuala ya Chadema na Mbowe huwa unakuwa na makengeza? Chadema wamejikita huko toka lini yaani unasema hujui kwamba wamekuwepo huko kwa muda mrefu sana, CCM ndio kwanza wameenda juzi tu!
- Halafu unasema Chadema hawana hela, hivi eti hujui kwamba huwa wanapewa hela za maalum za uchaguzi, na besides wana hela za kutosha toka kwenye ruzuku, halafu mbona habari ya kuzomewa CCM hukuuliza independent source? Wapenzi wa Chadema bwana, ndio maana wananchi huwa wanawaogopa sana, yaani in the name ya kupata power mnaweza kusema anything, Bwa! ha! ah! Acheni uchaguzi ufanyike kwa amani ni wenye sera zinazokubalika na wananchi ndio watashinda!
Respect.
FMES!
I hope waliowazomea CCM ni wananchi na wapiga kura wa hilo jimbo. Kama ni mamluki wa kupandikizwa basi tuangalie tusije tukaanza kufurahi mapema kwa kelele za watu ambao hawana sifa za kupiga kura.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimedaiwa kuingiza katika Jimbo la Busanda vijana takribani 70 kutoka wilayani Tarime kwa ajili ya kutisha watu na kuzomea viongozi katika mikutano ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Shutuma hizo zilitolewa jana mjini hapa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CCM, Matson Chizi kuwa vijana hao kutoka mkoani Mara, wamepelekwa katika kata kadhaa za jimbo hilo.
- Mkuu Mtanzania, ahsante sana kwa hii habari ambayo angalau inaweka kila kitu wazi nilichokisema, ndio uzuri wa JF huwa hatuburuzwi na uongo!
Mkuu Jasusi,Mtanzania,
Hiyo habari haina any other independent source except mkurugenzi wa uchaguzi wa CCM? Polisi wamesemaje? Unajua gharama ya kuwasafirisha vijana sabini kutoka Tarime na kuwatunza ugenini? Kama CHADEMA wana hela kama hizo za kuchezea ningewashauri wazitumie kwa umakini zaidi.
Ha ha haaa
My dear, are you there? Uchaguzi unakuja siku sio nyingi. Mgombea huyu wa CCM anayepiga magoti kuomba kura? Unaomba kura kwa kueleza sera, utafanya nini.
Anakuwa kama Hilary Clinton aliyetoa machozi ili anusuriwe?
Na hoja za waishiwa kama akina Malecela na Msekwa hazina mashiko.
FMES,
PS Habari za kuzomewa CCM hazikutolewa na CHADEMA.