Uchaguzi Busanda: Majigambo, Uteuzi na Kampeni kuelekea uchaguzi

Asante Nyumbu, hizi ndo habari tunataka zisikia, na hapa mwenye macho haambiwi tazama wala mwenye masikio haambiwi sikia, Chama cha mafisadi kiyama yake imewadia. Watu wana kiu ya ukombozi, yaani akitokea shujaa tu wapo tayari kusimama naye bega kwa bega!

By the way, kumbe Chama cha mafisadi at times kina tambua mchango wa kina Mwakyembe na Kilango et a.. yaani wakiwa kwenye nec yao wanawasulubu, sasa hivi ndo wanawakumbuka kwamba wakanadi mgombea wao?

Ama kweli ukiimbiwa ngombe waweza mtafuta hadi uvunguni mwa kitanda chako as if, huwa analala huko!
 
Kampeni Busanda: Moto kwa CCM, wabunge wote Mwanza waitwa kusaidia

Na Frederick Katulanda, Busanda
Source: Mwananchi

WAKATI joto la uchaguzi mdogo wa Jimbo la Busanda likizidi kuongezeka, vyama vya siasa vinavyowania kiti hicho vimebadili mbinu za kampeni, ikiwa ni pamoja na kuwaita wabunge na viongozi wake wa kitaifa ili kujiimarisha.

Kwa upande wa CCM mbali ya kumtumia aliyekuwa Makamu Mwenyekiti, John Malecela wamelazimika kumwondoa mjumbe wake wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Anthony Diallo ili kuliingiza kundi la mmoja wa wagombea aliyeshindwa kura za maoni kwa nia ya kuziba mpasuko unaokisumbua chama hicho.

Habari za ndani ya CCM zimeeleza kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya kampeni zao kupata upinzani mkali ikiwa ni pamoja na kuzomewa na watu wachache kujitokeza kwenye mikutano yao; wameamua kuunganisha makundi yanayohasimiana kwa kumuita aliyeibuka mshindi wa pili, Doanard Max ili asaidie kumnadi mgombea wao.

Diallo ametajwa kuwa hasimu mkubwa wa Max kutokana na kudaiwa kumsaidia mmoja wa wagombea kwa nia ya kumuengua (Max), jambo ambalo liligawa kura zake na kumfanya mgombea wa sasa kuibuka wa kwanza. Max alishika nafasi ya pili huku Sostenes Kulwa anayedaiwa kuungwa mkono na Diallo kuambulia nafasi ya tatu.

Sambamba na hatua hiyo, pia CCM imeamua kuwaita wabunge wake wote wa Mkoa wa Mwanza kwenda jimboni humo kusaidia kampeni za uchaguzi huo na wamepangiwa kata mbalimbali za jimbo hilo.

Mbali na wabunge hao pia CCM katika kuhakikisha inalikomboa jimbo lililoachwa na aliyekuwa mbunge wake, Kabuzi Rwilomba, imepunguza mikutano ya kampeni ya nje na kuimarisha ile ya ndani ili kuepuka kuzomewa.

Lakini Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza, Rajabu Kundya amekanusha kuondolewa kwa Diallo ili kumuita Max, bali ameondoka Busanda baada ya kutumwa Dar es salaam kwa ‘masuala mengine ya kichama'.

Kundya alisema chama chake kimewapangia kazi wabunge wake katika jimbo hilo na kufafanua kuwa kila mbunge amepangiwa kata kusimamia kampeni hadi wakati wa upigaji kura.

Hayo yakijiri, kampeni za wapinzani wa chama hicho, hasa Chadema, zinazidi kunoga na mikutano yake kupata idadi kubwa ya watu, ikilinganishwa na chama hicho kikongwe.

Kama CCM, pia inaelekea mambo ni mazito kwa chama cha CUF, kwa kuwa nacho kimeweka mkakati wa kuongeza nguvu kwenye kampeni zake kwa kuwaita wabunge wake kwa ajili ya kusaidia kumnadi mgombe wake, Oscar Ndalawah.

Katibu wa timu ya uchaguzi ya CUF, Maole Kuchilungulo aliwataja wabunge kuwa ni Magreth Sakaya, Savelina Mwijage, Nuru Bafadhiri na Zaharani Mwanakwetu, wote wakiwa wa viti maalumu. Wengine ni Omari Ally Mzee, Salum Abdallah na Mohamed Mnyaa wote wa Pemba.

Kwa mujibu wa katibu huyo, lengo la kuwaita wabunge hao ni kusimamia kampeni katika kila kata kwa kile alichosema, baada ya kubaini kuwa CCM imeleta wabunge wake na kuwatawanya kila kata kufanya hujuma ambayo hata hivyo hakuitaja.

"Awali CCM walitudharau, walijua kuwa mshindani wao ni Chadema, lakini baada ya kufanya mikutano wamegundua kuwa mgombea wetu ana nguvu zaidi ya kwao na wa Chadema; wamepanga mkakati wa kutuhujumu na baada ya kubaini hilo tumeamua kuwaita wabunge wetu ili kuja kuchuana na wenzao wa CCM katika kila kata," alieleza.

Chadema

Kwa upande wa Chadema wakiwa bado wanaendelea na kampeni za nje na zile za ndani walisema wameamua kumuita Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe kwa ajili ya kuongeza mashambulizi ya hoja na kufafanua kwa nini jimbo hilo limekuwa nyuma kimaendeleo.

Afisa Habari wa Chandema, David Kafulila alisema wao wamejipanga na kwamba kwa kuanza wameamua kumuita Kabwe ambaye atawasha moto katika kampeni hizo na baadaye kufuatiwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

"Hatuna wasiwasi, tuna mikakati mingi lakini naweza kusema tu tumeamua kumuita Zitto Kabwe ambaye sasa atakuwa akiambatana na mgombea katika mikutano hiyo kumnadi kwa wapiga kura," alieleza.

Green Guird' walilia posho

Katika hatua nyingine, Vijana 24 wa kikundi cha ulinzi cha CCM (Green Guard), wamelalamikia kupunjwa posho zao na kulipwa Sh800 kwa siku badala ya Sh2,000 walizoahidiwa.

Barua yao ya Mei 5,mwaka huu iliyoandikwa na kusainiwa na David Azaria ilieleza kuwa posho ambayo walistaili kulipwa jumla ya vijana 30 ni Sh 5,000 kwa wageni na Sh2,000 kwa wenyeji wa wilaya hiyo lakini wote wamekuwa wakilipwa Sh800 huku wakielezwa kuwa pesa hakuna.

"Maisha katika mji wa Geita ni magumu, lakini unalipwa Sh800, wanasema chakula tutakula huko. Hivi sasa hali ya maisha yetu ni ngumu sana, lakini tumejaribu kulalamika kwa Katibu wa CCM wilaya amesema tupokee na wasiotaka waondoke," alieleza mmoja wa vijana hao ambaye hakutaka kutaja jina lake.

Akijibu malalamiko hayo, Kundya alisema tatizo hilo kwa sasa limemalizika baada ya yeye kufika na watu wote waliopo katika kampeni wanalipwa kulingana na taratibu za fedha za chama.

"Tatizo hilo halipo, kuanzia nilipowasili wanalipwa kwa staili na taratibu za chama," alieleza Kundya.

Misimamizi wa uchaguzi
Vile vile CUF kimemtaka Msimamizi wa Uchaguzi kufuta zoezi la kuajiri makarani wa uchaguzi kutokana na kuchelewesha kutoa tangazo lake.

Afisa Uchaguzi wa CUF, Hussein Mmasi alisema kuwa tayari chama chake kimemlima barua msimamizi huyo kikieleza kuwa zoezi hilo limegubikwa na utata mkubwa, jambo ambalo linaonyesha wazi kuwa limefanywa makusudi kwa ajili ya kuisaidia CCM.

Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi jimboni hapa, Jackson Sombe amekiri kupokea malalamiko yao, lakini alikanusha kuwa matangazo hayo yalibandikwa siku ya mwisho.

"Nimepata malalamiko yao, lakini siwezi kubatilisha zoezi hilo, kwa sababu matangazo hayo hayakutolewa siku ya mwisho kama wanavyoeleza wao; yalibandikwa mapema kabisa, nimewaomba kwa kuwaandikia waje hapa ofisini kwangu kuhakiki majina ya makarani hao ili kama kuna mtu wana mashaka naye waseme aondolewe hawajaja," alisema Sombe.

Katika hatua nyingine, msimamizi msaidizi wa uchaguzi imevionya vyama vyote vya siasa kujiepusha na uvunjifu wa amani katika mikutano yao ili kuepuka vurugu kama za Tarime.

Sombe alisema vyama vote vinapaswa kuzingatia muda wa kuanza mikutano na kumaliza na kufuata ratiba ya mikutano ili kuepuka migongano.

"Niwaombe tu viongozi wa vyama kuzingatia haya, muda wa kufanya mikutano na kumaliza na kuwazuia wanachama wao kuwazomea wengine na kurushiana maneno," alieleza.

Uchaguzi wa Busanda unafanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Faustine Kabuzi Rwilomba. Katika uchaguzi huo vyama ambavyo vimeweka wagombea ni CCM, Chadema, CUF na UDP lakini mchuano mkali umekuwa kati ya wagombea wawili wa CCM na Chadema.
 
Ndugu kama ni kweli unataka CCM iendelee kushinda hutakiwa kumbeza RA kwani ndiyo ameshikilia ushindi wa chama chako na hauwezi kukipenda chama chako ukamchukia yeye unless uko fuse imekatika kidogo.

jamani tujiazali sana na hawa vugu vugu!
 
1.
Shalom;Ndugu kama ni kweli unataka CCM iendelee kushinda hutakiwa kumbeza RA kwani ndiyo ameshikilia ushindi wa chama chako

- Rostam hashikilii CCM, angekua basi asingetolewa hazina ya CCM tena bila ya kuambiwa mapema, na pia angeweza kumthibiti Mengi kule CC, na sasa hivi kusingekwua na tatizo kabisa na hii ishu yake na Mengi, maana angefanikiwa kuwashawishi Takukuru kumshitaki Mengi, mtu aliyeishikilia CCm kama unavyodai ameshindwa nini? Huna hoja hapo!

2. na hauwezi kukipenda chama chako ukamchukia yeye unless uko fuse imekatika kidogo. jamani tujiazali sana na hawa vugu vugu!

- Kama kawaida huwa ukishakuwa huna hoja then unaleta vituko, halafu hata unatumia jina la yesu na huu upumbavu wako, kama ni fuse tu hebu fikiria kwamba wewe ni kijibwa cha Nchimbi, na bosi wake ni RA, sasa hiyo inakuacha wewe wapi mkuu kwamba una fuse nzuri? Halafu ukija hapa JF unajifanya Chadema, si ndio vugu vugu hiyo unayoisema, umejiingiza na eti kuwekeza kwa Mwekyembe sasa umemtia kwenye matatizo maana ni wewe ndiye uliyeenda kumfahamisha Nchimbi kwamba Mwakyembe ana hii kampuni na hata kuharibu jina lake, hii ndio vugu vugu la sisi JF kujihadhari nazo. It is about time sasa ukajifunza ku-behave kulingana na umri wako, na kujua kwamba hapa JF tunajadili ishus za kulisaidia taifa ya binafsi hayana nafasi hapa!

CCM is bigger than Rostam na bosi wako Nchimbi combined.

Thank you na Respect!

Wazee wa sauti ya umeme FMES
 
FMES said:
CCM is bigger than Rostam na bosi wako Nchimbi combined.

FMES,

..haya maneno hapo juu yalipaswa kusemwa na wana-CCM wakati wa mchakato wenu wa wagombea Uraisi na Ubunge. yalipaswa kusemwa mwaka 2004 siyo 2009.

..wa-Tanzania tunapaswa kuwa makini,kuna mtandao mpya wa kifisadi unaundwa ndani ya CCM. wale mafisadi waliosaidia mwaka 2005 wanawekwa kando, wakati mafisadi wengine wakiwa-recruited kusaidia ushindi wa 2010.
 
Date::5/9/2009
Kampeni Busanda: Moto kwa CCM, wabunge wote Mwanza waitwa kusaidia

Na Frederick Katulanda, Busanda

Mwananchi
​

WAKATI joto la uchaguzi mdogo wa Jimbo la Busanda likizidi kuongezeka, vyama vya siasa vinavyowania kiti hicho vimebadili mbinu za kampeni, ikiwa ni pamoja na kuwaita wabunge na viongozi wake wa kitaifa ili kujiimarisha.

Kwa upande wa CCM mbali ya kumtumia aliyekuwa Makamu Mwenyekiti, John Malecela wamelazimika kumwondoa mjumbe wake wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Anthony Diallo ili kuliingiza kundi la mmoja wa wagombea aliyeshindwa kura za maoni kwa nia ya kuziba mpasuko unaokisumbua chama hicho.

Habari za ndani ya CCM zimeeleza kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya kampeni zao kupata upinzani mkali ikiwa ni pamoja na kuzomewa na watu wachache kujitokeza kwenye mikutano yao; wameamua kuunganisha makundi yanayohasimiana kwa kumuita aliyeibuka mshindi wa pili, Doanard Max ili asaidie kumnadi mgombea wao.

Diallo ametajwa kuwa hasimu mkubwa wa Max kutokana na kudaiwa kumsaidia mmoja wa wagombea kwa nia ya kumuengua (Max), jambo ambalo liligawa kura zake na kumfanya mgombea wa sasa kuibuka wa kwanza. Max alishika nafasi ya pili huku Sostenes Kulwa anayedaiwa kuungwa mkono na Diallo kuambulia nafasi ya tatu.

Sambamba na hatua hiyo, pia CCM imeamua kuwaita wabunge wake wote wa Mkoa wa Mwanza kwenda jimboni humo kusaidia kampeni za uchaguzi huo na wamepangiwa kata mbalimbali za jimbo hilo.

Mbali na wabunge hao pia CCM katika kuhakikisha inalikomboa jimbo lililoachwa na aliyekuwa mbunge wake, Kabuzi Rwilomba, imepunguza mikutano ya kampeni ya nje na kuimarisha ile ya ndani ili kuepuka kuzomewa.

Lakini Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza, Rajabu Kundya amekanusha kuondolewa kwa Diallo ili kumuita Max, bali ameondoka Busanda baada ya kutumwa Dar es salaam kwa ‘masuala mengine ya kichama'.

Kundya alisema chama chake kimewapangia kazi wabunge wake katika jimbo hilo na kufafanua kuwa kila mbunge amepangiwa kata kusimamia kampeni hadi wakati wa upigaji kura.

Hayo yakijiri, kampeni za wapinzani wa chama hicho, hasa Chadema, zinazidi kunoga na mikutano yake kupata idadi kubwa ya watu, ikilinganishwa na chama hicho kikongwe.

Kama CCM, pia inaelekea mambo ni mazito kwa chama cha CUF, kwa kuwa nacho kimeweka mkakati wa kuongeza nguvu kwenye kampeni zake kwa kuwaita wabunge wake kwa ajili ya kusaidia kumnadi mgombe wake, Oscar Ndalawah.

Katibu wa timu ya uchaguzi ya CUF, Maole Kuchilungulo aliwataja wabunge kuwa ni Magreth Sakaya, Savelina Mwijage, Nuru Bafadhiri na Zaharani Mwanakwetu, wote wakiwa wa viti maalumu. Wengine ni Omari Ally Mzee, Salum Abdallah na Mohamed Mnyaa wote wa Pemba.

Kwa mujibu wa katibu huyo, lengo la kuwaita wabunge hao ni kusimamia kampeni katika kila kata kwa kile alichosema, baada ya kubaini kuwa CCM imeleta wabunge wake na kuwatawanya kila kata kufanya hujuma ambayo hata hivyo hakuitaja.

"Awali CCM walitudharau, walijua kuwa mshindani wao ni Chadema, lakini baada ya kufanya mikutano wamegundua kuwa mgombea wetu ana nguvu zaidi ya kwao na wa Chadema; wamepanga mkakati wa kutuhujumu na baada ya kubaini hilo tumeamua kuwaita wabunge wetu ili kuja kuchuana na wenzao wa CCM katika kila kata," alieleza.

Chadema

Kwa upande wa Chadema wakiwa bado wanaendelea na kampeni za nje na zile za ndani walisema wameamua kumuita Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe kwa ajili ya kuongeza mashambulizi ya hoja na kufafanua kwa nini jimbo hilo limekuwa nyuma kimaendeleo.

Afisa Habari wa Chandema, David Kafulila alisema wao wamejipanga na kwamba kwa kuanza wameamua kumuita Kabwe ambaye atawasha moto katika kampeni hizo na baadaye kufuatiwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

"Hatuna wasiwasi, tuna mikakati mingi lakini naweza kusema tu tumeamua kumuita Zitto Kabwe ambaye sasa atakuwa akiambatana na mgombea katika mikutano hiyo kumnadi kwa wapiga kura," alieleza.

Green Guird' walilia posho

Katika hatua nyingine, Vijana 24 wa kikundi cha ulinzi cha CCM (Green Guard), wamelalamikia kupunjwa posho zao na kulipwa Sh800 kwa siku badala ya Sh2,000 walizoahidiwa.

Barua yao ya Mei 5,mwaka huu iliyoandikwa na kusainiwa na David Azaria ilieleza kuwa posho ambayo walistaili kulipwa jumla ya vijana 30 ni Sh 5,000 kwa wageni na Sh2,000 kwa wenyeji wa wilaya hiyo lakini wote wamekuwa wakilipwa Sh800 huku wakielezwa kuwa pesa hakuna.

"Maisha katika mji wa Geita ni magumu, lakini unalipwa Sh800, wanasema chakula tutakula huko. Hivi sasa hali ya maisha yetu ni ngumu sana, lakini tumejaribu kulalamika kwa Katibu wa CCM wilaya amesema tupokee na wasiotaka waondoke," alieleza mmoja wa vijana hao ambaye hakutaka kutaja jina lake.

Akijibu malalamiko hayo, Kundya alisema tatizo hilo kwa sasa limemalizika baada ya yeye kufika na watu wote waliopo katika kampeni wanalipwa kulingana na taratibu za fedha za chama.

"Tatizo hilo halipo, kuanzia nilipowasili wanalipwa kwa staili na taratibu za chama," alieleza Kundya.

Vile vile CUF kimemtaka Msimamizi wa Uchaguzi kufuta zoezi la kuajiri makarani wa uchaguzi kutokana na kuchelewesha kutoa tangazo lake.

Afisa Uchaguzi wa CUF, Hussein Mmasi alisema kuwa tayari chama chake kimemlima barua msimamizi huyo kikieleza kuwa zoezi hilo limegubikwa na utata mkubwa, jambo ambalo linaonyesha wazi kuwa limefanywa makusudi kwa ajili ya kuisaidia CCM.

Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi jimboni hapa, Jackson Sombe amekiri kupokea malalamiko yao, lakini alikanusha kuwa matangazo hayo yalibandikwa siku ya mwisho.

"Nimepata malalamiko yao, lakini siwezi kubatilisha zoezi hilo, kwa sababu matangazo hayo hayakutolewa siku ya mwisho kama wanavyoeleza wao; yalibandikwa mapema kabisa, nimewaomba kwa kuwaandikia waje hapa ofisini kwangu kuhakiki majina ya makarani hao ili kama kuna mtu wana mashaka naye waseme aondolewe hawajaja," alisema Sombe.

Katika hatua nyingine, msimamizi msaidizi wa uchaguzi imevionya vyama vyote vya siasa kujiepusha na uvunjifu wa amani katika mikutano yao ili kuepuka vurugu kama za Tarime.

Sombe alisema vyama vote vinapaswa kuzingatia muda wa kuanza mikutano na kumaliza na kufuata ratiba ya mikutano ili kuepuka migongano.

"Niwaombe tu viongozi wa vyama kuzingatia haya, muda wa kufanya mikutano na kumaliza na kuwazuia wanachama wao kuwazomea wengine na kurushiana maneno," alieleza.

Uchaguzi wa Busanda unafanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Faustine Kabuzi Rwilomba.

Katika uchaguzi huo vyama ambavyo vimeweka wagombea ni CCM, Chadema, CUF na UDP lakini mchuano mkali umekuwa kati ya wagombea wawili wa CCM na Chadema.
 
Sasa jamani tukisema mtu mzima kuvutwa sharubu?

Sasa mikutano ya ndani ina maana wanaita wananchi kwenye majengo kunadi sera zao ama? Ogopa siraha ya kuzomewa wakuu, is bigger than mabomu ya kutoa machozi!
kwi kwi.. labda wataufute super glue wawe wana wabana midomo wananchi ili wasiwazomee!
 
- Hayo ni matatizo ya ndani ya CCM na sio taifa, ndio maana Zitto anasema Dowans ni safi Dr. Slaa anasema sio safi, muwe mnakumbuka kwamba Tanzania sasa tuna demokrasia watu wana uhuru wa kufanya wanayotaka bila kuvunja sheria za jmahuri, kuunda mtandao sio kosa ila kuvunja sheria ndio kosa kisheria!

Respect.

FMES!
 
- Haya ni maneno na habari za kampeni tu ndio maana huwa hatuulizi independent source, huwa wanaanza nayo kwenye kila kampeni ya kutufanya wananchi wote tuamini kwamba watashinda, halafu wakipigwa mueleka utasikia vilio, wakuu leteni habari za kweli kutoka huko Busanda acheni hizi propaganda maana mwishoni mtaishia kulia mmeibiwa kura kumbe mlikuwa mnadanganya kuhusu hali halisi huko uwanjani!

Respect.

FMEs!
 
FMES, Hizi ni mvua za rasha rasha, subiri 2010 kama hili la kuwazomea CCM likitambaa Tanzania nzima, basi CCM watakuwa na kipindi kigumu mno na si ajabu wakapigwa na mshangao ambao wao wenyewe na wafuatiliaji wa mambo ya kisiasa Tanzania hatukuutegemea.
 
- Strong point mkuu, unajua wanatusaidia sana kutuamsha ndio maana unaona Mtandao kina Diallo wanaondolewa huko, mkuu nimeongea na wakulu wa CCM huko Busanda wanakubali kwamba huu uchaguzi hautakuwa lelemama kama ile mingine, halafu ni demokrasia at work!

FMES!
 
Kweli shughuli ndefu, mpaka umekiri? Ombeni Mungu nami naenda kuongeza nguvu.
 
- Huwa sina ushabiki wa kitoto, kwenye ukweli ninakubali na kwenye uongo ninasema sana, ukweli ni kwamba Busanda mambo ni magumu kwa pande zote mbili, na hasa CCM zaidi,ingawa anaweza kushinda anybody huwa sina taabu kukubali kupongeza aliyeshinda hata kama ni upinzani, huwa tunakuja hapa na open mind!

- Na hili ni jimbo moja tu la uchaguzi, CCM walishinda Kiteto, Tunduru, Mbeya, na Chadema wakashinda Tarime ndio maana ya demokrasia makini.

FMEs!
 
Kaka nilikuwa natania mjomba, siendi Busanda ila upinzani ukishinda nitapata faraja kwani vita ya mafisadi itapamba moto yaani itaonyesha kuwa we need real democracy. Otherwise nahisi ushabiki vile!

What do you think kaka?
 
CCM wamekanusha habari hizo za kuzomewa, kwa uhakika wanaona aibu kukubali. Kazeni mwendo wana Busanda, tutafika tu siku moja!
 
Nawawekea picha za mkutano wa jana wa Mhe.Zitto akiwahutubia wananchi wa Busanda kata ya Katoro ambapo CCM mpaka sasa pamoja na kuwa ndio makao makuu ya Jimbo wameshindwa kabisa kufanya mkutano na kueleza wao wanasimamia nini na mgombea wao ana sifa gani.

Last edited by a moderator:
Picha ziko wapi mkuu?, au ni mimi tu nashindwa kuzipata hapa JF?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…