Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 59,804
- 134,593
duh...hii sasa italeta wivu ndani ya upinzani. CUF wangekaa pembeni tu sasa, wabaki washabiki tu!Kabla ya kuwasili helikopita hiyo, mamia ya wakazi wa eneo hilo walikuwa wamejitokeza kwa wingi kuhudhuria mkutano wa kampeni za Chama cha Wananchi (CUF), lakini baada ya kutua, mkutano huo ulishindwa kuendelea baada ya waliokuwa wamekusanyika kwa ajili ya kusikiliza sera za chama hicho kukimbilia katika mkutano wa CHADEMA.
Napenda kuwaambia ndugu zangu, leo nimewaita hapa kutaka kuwaambia kwamba, tuna kazi moja tu ya kuhakikisha mnachagua CCM katika uchaguzi ujao, sasa nawaambia kama hamtafanya hivyo, tutahakikisha tunawanyanganya leseni kwani CCM ndiyo yenye serikali, alisema Ngeleja.
Unaonekana wewe upo chama kimoja na mafisadi,
Wewe mwenyewe umeshindwa kujiandaa vyema kuleta habari iliyokamilika. Huenda walitakiwa kujulikana mapema nao waanze kupewa chumvi na magodoro.
watu wako makini wakiwajua mapema wanaanza kuwasumbua narushwa ndo mana wanawataja dakika ya mwisho.
Hongera mkuu kwa kuliona hilo, nafikiri ndicho walichokuwa wanakitafuta hicho kuwajua mapema ili wawape ahadi kubwa na kuruhusu wizi wa kura huyo ndio CCM kubwa la maadui kwenye picha ya kihindi.
Hatua ya Ngeleja kukimbiwa na wachimbaji hao ilitokana na kauli yake kuwa, kama watashindwa kuichagua CCM watanyag'anywa leseni na kufutiwa usajili wa vitalu vyao.
Katika mkutano huo ambao ulifanyika katika Shule ya Msingi Mwenge, Ngeleja alisema CCM ndiyo yenye wezo wa kuchukua hatua zozote zinazostahili kuwaendeleza wachimbaji, wakiwamo wa migodi mikubwa kama vile Mererani, North Mara na Geita Gold Mine.
"Napenda kuwaambia ndugu zangu, leo nimewaita hapa kutaka kuwaambia kwamba, tuna kazi moja tu ya kuhakikisha mnachagua CCM katika uchaguzi ujao, sasa nawaambia kama hamtafanya hivyo, tutahakikisha tunawanyang'anya leseni kwani CCM ndiyo yenye serikali," alisema Ngeleja.
Alisema wachimbaji wadogo wadogo wamekuwa na tabia ya kupinga sera za CCM eti kwa madai kuwa imekuwa ikiwakandamiza, jambo ambalo halina ukweli wowote.
Katika hali inayoonekana kuwa vitisho, Ngeleja alisema kama CCM itashindwa kwenye uchaguzi huo, wachimbaji hao watashukiwa kwa nguvu zote na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kuona kama kweli wanalipa kodi ya serikali.
"Moja ya mkakati ambao tumeandaa ni kwamba kama CCM haitashinda, TRA itakuja hapa kwa ajili ya kuhakiki kama kweli mnalipa kodi ya mapato, ikiwa ni kinyume chake mtashughulikiwa kwa mujibu wa sheria ya serikali," alisema Ngeleja.
Kauli hiyo ilionekana kuwaudhi wachimbaji hao ambao walianza kuondoka mmoja mmoja ndani ya ukumbi na kumwacha Ngeleja na viongozi wa CCM aliokuwa ameambatana nao kwenye kikao hicho.
Huo ni mtazamo wako; nimeamua kusema ukweli ili ijulikane kwa watu wote kuwa Upinzani ukipigwa bao kusiwe na visingizio tuliibiwa kura au mengineyo wkt mazingira ya kuibiwa tuliyataka wenyewe
Mimi si mwandishi wa habari; nimeandika vile nilivyoipata hiyo habari kutoka ktk chombo cha habari (TBC Taifa) wakati msimamizi anahojiwa na mwandishi wa habari. Jadili somo husika usinijadili mimi bainafsi, nimefikisha ujumbe kwa wadau wa siasa. Kama unaona huelewi kitu kaa kimya hujalazimishwa.
Kujulikana mapema kwa wasimamizi ni jambo muhimu sana ni ktk mikakati ya kujihakikishia maandalizi ya kulinda kura za chama chako. Ukiweka msimizi asiye muaminifu ni tatizo la chama husika kilichomuweka msimamizi huyo bomu asiyejua thamani ya ushindi kwa chama chake na kwa wapenda maendeleo wote kwa ujumla; si la chama cha mafisadi. Tunajua mafisadi kazi yao ni kufisidi; kwa hiyo lazima tutarajie watatafuta upenyo ili wapitishe ufisadi wao kwa huyo msimamizi ili lengo lifanikiwe nalo ni kuiba kura au kuweka kura zilizokwishapigwa.
Vile vile tujue uchaguzi una sheria na taratibu zake; kama wakichelewa kupelekwa ndio tumeliwa sisi; hizo kampeni na mengineyo yote itakuwa ni big zero
Muhimu kila chama hasa wapinzani kujenga msingi madhubuti kwa wanachama wao hasa UAMINIFU KTK CHAMA NA MAISHA YA KILA SIKU KWA UJUMLA, tuwaeleshe wanachama wetu thamani yao ktk chama na wao wanatakiwa wakithamini chama; na jengine wawajulishe umuhimu wa kuwa na uaminifu kwao wenyewe na kwa chama chao.
Kama mtu anajua thamani yake, utu wake na thamani ya chama chake kwake binafsi na jamii kwa ujumla, hata FISADI AJE NA MILIONI NGAPI HATAPOTEZA UAMINIFU WAKE KWA MAMBO YA KUPITA
AMANDLA!!!
Ymeashaanza. technicalities kama hizi (kupeleka majina wiki moja kabla...) zinafanana na yale mambo yaliyotokea Mbeya. Ebu nikalale mie
Si kwamba napingana na sheria, hapana. Kinachonichosha ni kuona yaliyotokea Mbeya Vijijini yanaweza pia kutoka na Busanda. lawama of course zitakuwa juu ya watakaoshindwa kufuata matakwa ya sheria na kanuniSio kweli; hii sheria ipo miaka mingi tu. Sina hakika ni viongozi wa vyama kutokujua taratibu nzima za uchaguzi au ni kutokufuatilia taratibu na sheria za uchaguzi; kuanzia mchakato wa kutafuta wagombea hadi ktk kumpata mshindi wa uchaguzi.
Mimi ntajuaje hakuna kina "mashibya" wakati mwandishi kasema "mashibya"? Na wale wanaosema Busanda hakuna kina "mashibya" wameuliza majina ya kila mkazi wa eneo hilo, wahamiaji, na wageni wengine ambao si wa asili wa miji hiyo? ubishi mwingine!
Yamebaki masaa 48 muhimu kwa Chadema kuunganisha nguvu na CUF kuichukua Busanda. Kuna watu wa aina yangu, type ya kina Tomaso wa Biblia, hatuwezi kuamini kinachotarajiwa kutokea Busanda mpaka tukashuhudie kwa macho, Kesho natia timu Busanda kushuhudia na kuwajulisha.
Mpaka sasa, barua imekuja too late na there is too little to do.Busanda ni CCM asilimia 40% hiyo asilimia 60% CUF watagawana na Chadema na mshindi atabaki CCM.
Haya ni matokeo ya ubinafsi wa viongozi wetu kwa kila mmoja kujiuliza kwa nini nisiwe mimi?, Busanda hiyoo....CCM.
Haina maana mimi ni mshabiki wa CCM, mimi ni mshabiki wa ukweli na hali halisi.
Hako kabarua hakana mpya yoyote!
Mkuu AljuniorTz habari yako hukuifanyia utafiti wa kutosha tayari wasimamizo wapo tena wamejiandaa vy akutosha kulinda hizo kura zetu za za ushindi.Watu wapo hatua moja mbele yako mkuu.
Ni kweli sikufanya utafiti wa kutosha; ila nimetoa taarifa nikiwa mpenda mageuzi ya kweli ktk nchi yangu hasa baada ya kupata taarifa kutoka kwa msimamizi wa uchaguzi. Sipendi tuwe ni wababaishaji ktk kuyaendea hayo mageuzi ya kweli, halafu baadae tuwe tunalalamika...
hujaelewa hoja yake, umekurupuka kupondo...usiwe mvivu wa kusoma.Unaonekana wewe upo chama kimoja na mafisadi,