Siku chache baada ya kuripotiwa sakata la kukatwa ovyo kwa Majina ya wagombea ndani ya CCM bila kufuata utaratibu huko Ilala mapya yaibuka.
Inaelezwa kwamba Makatibu wote wa Mikoa na Wilaya "wamepewa Maagizo" na Katibu Mkuu Chongolo kuhakikisha kila anayegombea anaambatanisha Kopi za Vyeti vyake vya taaluma (form 4, form 6 na Chuo) na Mgombea asiyeambatanisha, fomu yake isipokelewe.
Inaelezwa kwamba mpango huu una lengo la kupunguza "wapiga debe" ndani ya Chama na kuweka Wasomi wenye uwezo wa Kupambanua Mambo.
Pia hii itasaidia Mamlaka za Uteuzi Serikalini kuwateua makada wenye sifa katika nafasi nyeti serikalini.