Uchaguzi CCM: Marufuku kuchukua fomu kama huna Cheti cha Taaluma

Uchaguzi CCM: Marufuku kuchukua fomu kama huna Cheti cha Taaluma

Status
Not open for further replies.
Katibu hana mamlaka hayo, mnajaza uchafu tu JF.

Mkutano mkuu wa ccm uliokutana Dodoma ndio uliopitisha kanuni za uchaguzi, hizi zingine ni porojo tu.

Wewe unadhani mikataba yote ya hovyo nchi hii waliingia walioishia darasa la saba au secondary school?
Waliingia wajaza matumbo km akina February -1. Kuna kuwa na elimu ukaendeshwa na tumbo au kutokuwa na elimu ukaendeshwa na ukosefu wa utashi kuelewa jambo.
 
Hivi unafahamu Sugu ni form four lakini anawazidi kwa mbali sana wasomi bingwa kama kina Dr Mwakyembe?

Tanzania hatuhitaji vyeti bali tunahitaji watu wenye akili kichwani vyeti ni nyongeza tu ya maarifa.

Degree na intelligent ni vitu viwili tofauti kabisa.
Km ulishindwa shule usipambe ujinga. Mjinga ni mjinga tu, Sugu anamzidi lipi Dr. Mwakyembe? Kuifanya Mbeya isitulie? Vurugu? Namshangaa sana mtu anayeshabikia ujinga kisa tu umeshindwa shule. Hovyo kabisaaaa!!!!
 
Kwa hiyo akina Namba 3 (Mkoa), Gachuma (Mkoa), Ochele (Wilaya) na Ngitu (Wilaya) kule Mara itakuwaje maanake ccm ina watu wengi sampuli hiyo ambao wao kuwa kwao kwenye siasa ni mkakati maalumu wa kujitafutia maisha.
 
Sifa za dc,rpc,rc,kc sijui ni kushiriki kwa dhati kwenye kuhakikisha rais na chama kinaibuka kidedea kwa kishindo katika chaguzi, baaasi!
 
Ndo ishakula kwao hivyo. Watafute chaka jingine la kujifichia ila sio ndani ya Chama 😂
Halafu inakuaje CCM imejaza watu wa dizaini hii jamani??
 
Sifa za dc,rpc,rc,kc sijui ni kushiriki kwa dhati kwenye kuhakikisha rais na chama kinaibuka kidedea kwa kishindo katika chaguzi, baaasi!
Makada watiifu. Kipimo cha RC & DC ni kumsifia Rais mbele ya Camera
 
Mama ameona mbali sana. Baada ya Miaka 10 CCM itaendeshwa kisomi mno. Naona pia huu ni mwanzo wa kufuta wabunge wa darasa la 4B huko mbeleni
Kwani serikali haina Wasomi? Mbona imejaa mapropesa na madagtari lakini inaendeshwa utadhani genge la Nyanya la Mama Kuruthumu?

Sent from my M2003J15SC using JamiiForums mobile app
 
Kwani serikali haina Wasomi? Mbona imejaa mapropesa na madagtari lakini inaendeshwa utadhani genge la Nyanya la Mama Kuruthumu?

Sent from my M2003J15SC using JamiiForums mobile app
Kwa sababu wenye Ilani inayotekelezwa ndio hao waliokuwa na elimu ya kujua kusoma na kuandika tu. Unategemea nini??
Mama amekuja kurekebisha hili
 
Siku chache baada ya kuripotiwa sakata la kukatwa ovyo kwa Majina ya wagombea ndani ya CCM bila kufuata utaratibu huko Ilala mapya yaibuka.

Inaelezwa kwamba Makatibu wote wa Mikoa na Wilaya "wamepewa Maagizo" na Katibu Mkuu Chongolo kuhakikisha kila anayegombea anaambatanisha Kopi za Vyeti vyake vya taaluma (form 4, form 6 na Chuo) na Mgombea asiyeambatanisha, fomu yake isipokelewe.

Inaelezwa kwamba mpango huu una lengo la kupunguza "wapiga debe" ndani ya Chama na kuweka Wasomi wenye uwezo wa Kupambanua Mambo.

Pia hii itasaidia Mamlaka za Uteuzi Serikalini kuwateua makada wenye sifa katika nafasi nyeti serikalini.
Ccm ni maviii
 
Msukuma na Lusinde watanyang'anywa nyadhifa zao?
 
Najaribu kuwafikiria hawa vijana wanaomaliza form 4 miaka hii nabaki najiuliza kuwa hawa ndio wana uelewa kuliko mie na darasa la saba langu?
 
Labda kwa DSM.

Vijijini watakosa wagombea!

Isitoshe vyeti havimfanyi mtu asiwe "mpiga debe".

Kuna chawa wana hadi PhD.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom