Uchaguzi CHADEMA: Anthony Komu ataka Mbowe apishe uenyekiti

Naelewa tumetoka mbali juu ya jambo hili la Mbowe.

Hii sababu ya Rais Magufuli kung'ang'ania kuwepo kwenye madaraka kwa kisingizio cha Mbowe..., hapana. Hahitaji sababu hafifu kama hiyo ku'justify' hatua hiyo, sote tunaelewa vizuri uwezo na nguvu zake, na 'ushawishi' wake.

Mimi nawasihi CHADEMA wafanye maamuzi yao kwa uangalifu mkubwa kwa manufaa ya chama chao. Kama wanaona Mbowe ndio kiongozi wanyemtaka na wnahakikisha wanachama wao wanatoa ridhaa yao kwa uhuru na utashi wao; hiyo inatosha kuninyamazisha hata kama naona kua uwezekana wa kuwepo na hatari ya kufanya hivyo.

Mimi ningependa CHADEMA waamue wenyewe kwa utashi wao wenyewe, wanataka nani awaongoze. Ningekuwa nashiriki kura hiyo, ingenilazimu nijiridhishe kuwa kuendelea kuwepo kwa Mbowe hakuepukiki.
 
Kwa hiyo asipogombea hiyo kesi itawekwa pembeni na chama chake kitaondolewa pingamizi zote zinazokikwamisha kumudu mapambano? Kwa maneno mengine kitabebwa na chama tawala ili kiendelee na mapambano. Wanachotakiwa kufanya ni kumtema Mbowe tu!
Sijasema kuwa "asipogombea kesi itawekwa pembeni", na kwamba "chama chake kiaondolewa pingamizi zote"
Sijasema "chama chake kitabebwa na chama tawala"

Na wala sijamwomba popote asigombee uenyekiti wa CHADEMA.

Kwa kifupi ni kwamba, huna uwezo kabisa wa kunibebea akili yangu na kuwasilisha hapa ninayoyaeleza.
Unachoweza kufanya ni kupotosha, kupindisha, au kutoelewa kabisa nilichowasilisha.
 
Ni kweli mkuu hapa kuna hatari ya kupasua chama vipande2
Hili CCM wamelitafuta muda mrefu sana bila ya mafanikio kutokana na umahiri na uimara wa Mh. Mbowe. Inawezekana wakawa wameona mwanya safari hii. Acha tusubiri, huenda tutayaona mengi katika muda mfupi wa wiki zijazo.
 
Mbowe awaachie Damu changa hawa malaya wa kisiasa?
 
Hamna anayepindisha uliyoandika. Ni kweli kabisa siwezi kukubebea akili zako. Kwa kujua hivyo basi unatakiwa kuwa makini na unachokiandika ili ujumbe unaotaka kutuma ueleweke vizuri. Sisi wengine tunasoma kinachoandikwa na kutafsiri tunavyokiona. Badala ya kulalamika mno, ungesema tu hatukukuelewa, halafu ukatueleza ulichokusudia. Kwa jinsi ulivyoandika, bado nasimama kwenye tafsiri yangu. Sina sababu ya kupotosha au kupindisha ulichoandika.

Amandla.......
 
Inaonekana km mbowe kaishiwa pumzi
 
Hao wote ni wanasoccos wenzio! Ngoja nimwite mwingine huyu hapa technically unaitwa huku kuwa wewe ni mwana Lumumba eti kwa kumshauri dikteta Mbowe kukiacha chama cha saccos ili vijana wagombee!!!
Ndio kimetuweka mjini ,Pesa baba so saccos ndio mpango wenyewe.
 
Yaani mtu aliyekuja chamani kwa mafuriko ya mzee Lowasa miaka minne iliyopita apewe kuongoza cdm, kwa kweli hamtakuwa serious.
 
MwambaTuvushe ---- Mbowe hakuna kutoka kwenye Uwenyekiti ...Ukiona CCM hawakutaki basi jua umewakamatia pabaya...Hawa kina Komu ni watu wenye pricetag wananunulika ndio maana clips zake zilivuja.
CDM-CECIL DAVID MWAMBE
 
Sijawahi kumsikia Bungeni. Labda ni mpiga makofi kama wale mbogamboga.
Nje ya Bunge sijawahi kumsikia kwa lolote. Atakuwa katumwa na Jiwe.
Sisemi lazima awe Mbowe, lakini huyo Mnyasa vyema akagombee Malawi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…