KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Naelewa tumetoka mbali juu ya jambo hili la Mbowe.Ninashukuru kalamu1 kwa kuliona hili kwa uhalisia wake. Hii hatari nimeshaiona iwapo Mbowe ataendelea kuwa mwenyekiti huu unajisi wa box la kura utatumika kipropaganda kuwa watu haiwachagui cdm maana haina demokrasia. Pia hatari nyingine kubwa kabisa ninavyoona, cdm ndio chama kinachopendwa kiukweli kwa ushawishi wa kisiasa, iwapo Mbowe ataendelea kuwa mwenyekiti bila sisi kukataa kwa nguvu zetu, hiyo itatumika kama kinga ya kumuongezea Magufuli muda wa kuendelea kukaa madarakani, maana watakaopinga Magufuli kuendelea kukaa madarakani ni cdm kuanzia wanachama wake mpaka mashabiki. Je iwapo Mbowe ataendelea kuwa mwenyekiti hiyo nguvu tutaitoa wapi? Faida za Mbowe kuendelea kuwa madarakani ni ndogo kuliko hasara zake. Katika hili nimesema msimamo wangu utakuwa wazi kama nilivyopinga Lowassa kupewa tiketi ya kugombea urais, na sasa karudi zake ccm.
Hii sababu ya Rais Magufuli kung'ang'ania kuwepo kwenye madaraka kwa kisingizio cha Mbowe..., hapana. Hahitaji sababu hafifu kama hiyo ku'justify' hatua hiyo, sote tunaelewa vizuri uwezo na nguvu zake, na 'ushawishi' wake.
Mimi nawasihi CHADEMA wafanye maamuzi yao kwa uangalifu mkubwa kwa manufaa ya chama chao. Kama wanaona Mbowe ndio kiongozi wanyemtaka na wnahakikisha wanachama wao wanatoa ridhaa yao kwa uhuru na utashi wao; hiyo inatosha kuninyamazisha hata kama naona kua uwezekana wa kuwepo na hatari ya kufanya hivyo.
Mimi ningependa CHADEMA waamue wenyewe kwa utashi wao wenyewe, wanataka nani awaongoze. Ningekuwa nashiriki kura hiyo, ingenilazimu nijiridhishe kuwa kuendelea kuwepo kwa Mbowe hakuepukiki.