Kabla ya kutoa kauli yako ungefanya utafiti kwanza ili ujiridhishe kutetea mwono wako.

Kaulimbiu ya CHADEMA

Viongozi na wanachama wa CHADEMA waliamua kutoa kaulimbiu isemayo: Kashindye ashinde, Kafumu afumuliwe.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alisema umati uliohudhuria katika uzinduzi wa kampeni hizo ni kielelezo kuwa chama hicho ni makini na kinapaswa kuiongoza serikali, hivyo ni vema CCM wakajiandaa kuondoka Ikulu.

Alisema Rais Kikwete alipelekwa Ulaya kununuliwa suti, halafu akatoa maeneo kwa mwekezaji mwenye asili ya Uarabuni, wakati wananchi wake wako katika matatizo makubwa.

Alibainisha kuwa wakati wa utawala wa awamu ya pili maisha angalau yalikuwa na nafuu, lakini alipokuja Mkapa mambo yakawa mabaya zaidi

licha ya kutuambia uchumi unakua zaidi.

Amekuja mzee wa kutabasamu (JK), mambo yamekuwa mabaya zaidi, miaka 10 ya Mkapa ilikuwa nafuu zaidi kuliko miaka sita ya Kikwete.

Inakuwaje wakati wa Mwinyi mambo yalikuwa angalau kidogo, lakini kadri tunavyokwenda ndivyo mambo yanazidi kuwa mabaya zaidi tofauti na huko tulikotokea?

Kila kukicha JK anakwenda Marekani kuombaomba, wakati hapa nchini kuna rasilimali lukuki. Kila akikosolewa anasema safari hizo zina manufaa makubwa sana kwani tunafadhiliwa sana, tunapata vyandarua vya nchi, Rais wa nchi anakwenda kuomba vyandarua wakati akiwaachia Wazungu wakinufaika na fedha zinazotokana na madini! CHADEMA hatutatumia muda wetu kuomba vyandarua, bali tutatumia rasilimali zetu kununua vyandarua na mahitaji muhimu kwa jamii.

CCM ijiandae kukabidhi madaraka kwa taifa. Polisi tunawaomba mtuachie CCM tupambane nao, ukombozi wa taifa hautaletwa na rangi za bendera za vyama au uzuri wa watu, bali dhamira za kweli za viongozi wake. Hamjabebwa na watu kuja hapa kama wanavyofanya hao wenzetu, tunawashukuru, alisema Mbowe.