Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Status
Not open for further replies.
udini huu...ngoja tuone utatufikisha wapi, kama vp waombe nyumba za wakristo, kwani wakristo hawana nyumba huko igunga??

sidhani kama ni udini nafikiri ni umbumbu zaidi wa siasa za vyama vingi na ccm imekuwa ikitumia mwanya huo kuwatisha wahusika ili wasishirikiane na upinzani kwa kuwatisha kufunga biashara zao au kuwatisha kuwadai kodi zao za miaka yote ambazo wamekuwa hawalipi na vitu kama hivyo.

kwa watu tunaofuatilia vizuri mfumo wa vyama vingi ulivyoanza Tanzania ni kwamba vitu hivi havikuanza leo kwani huko miaka ya nyuma wagombea wa urais wa vyama vya upinzani walipokuwa safarini mikoani walinyimwa hadi mafuta kwenye baadhi ya vituo kwa sababu ya wahusika
kutishwa au kwa humbumbu wao kisiasa. ktk issue hii ya nyumba inaonekana wazi kuwa ni vitisho kwani kama walikuwa hawawataki chadema wangeshakataa pesa toka mwanzo lakini kupokea pesa na baadaye ghafla kuzikataa hiyo inaonhyesha wazi kuwa ni mchezo mchafu wa CCM.
 
kaka english yako du wengine sisi ni product ya shule za kata hatujakusoma kabisa

kwa misingi hiyo mwita25 ana tatizo kwenye effective communication ,
haina maana kumwaga maneno watu wasiyoyaelewa au kuyaelewa kwa taabu,
mwita25 hana point kwa hiyo ndiyo njia rahisi kufisha udhaifu wake
 
CCM haifai imezeeka ni kikongwe anayejikojolea hapo hapo bila kujali wajukuu
 
Kwani mwandishi akiandika taarifa za uongo katika tukio kama hili adhabu yake ni nini?
 



Matomaso kama nyie mnatakiwa mwangalie kwa macho, umeona wa magamba wenzio wanavyo ufyata kwa pipoz pawa
 
Gazeti la mwananchi la leo lina picha ya watoto mbele kabisa wanasema CCM wahaha kutafuta watu wakuhudhuria mkutano niambie kuna mwananchi mbili japo contents wameandika hayo ukitafakari utajua wanapigwa vijembe kwa kuonyesha picha ya vitoto vya igunga
 

You keep on dreaming!!.. Dreamer!!!... By the time you come back to your senses... It'll be over.... and you'll be baffled!!!...
 
ccm wanazindua kampeni huku taifa linaoboleza. Labda meli iliyozama haina uhusiano na Igunga, pamoja na uccm yenyewe.
 

Mkuu unanishambulia bure, sina nia mbaya nimeleta habari hapa JF watu ambao hawajasoma wajue ni nini kinaendelea na namna ya kukabiliana nacho.

Fuatilia vizuri post zangu hapa JF
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]Makada wa CCM wasaka wapambe mitaani Igunga
[/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"]Friday, 09 September 2011 21:57
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]0diggsdigg

NI KWA AJILI YA KUSHIRIKI MKUTANO WA UZINDUZI LEO, ROSTAM HAKIJAELEWEKA
Mwandishi Wetu, Igunga
JIMBO la Igunga jana lilikumbwa na kitimtim cha maandamano ya wanachama na wapenzi wa CCM waliokuwa wakipita katika mitaa mbalimbali kuhamasisha wakazi wa hapa kujitokeza kwa wingi leo kwenye ufunguzi wa kampeni za chama hicho zitakazozinduliwa na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa.Kadhalika, mji huo ambao umeingia kwenye pilikapilika za uchaguzi mdogo wa ubunge, umeshuhudia vigogo wa CCM wakiongozwa na Mkapa wakihamia kwa muda mjini humo, kuhudhuria uzinduzi wa kampeni za chama hicho ambao unafanyika baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Mbunge wake, Rostam Aziz (CCM).

Rostam licha ya kuachia nafasi hiyo huku akiwashutumu baadhi ya vigogo kuhusika na kile alichokiita siasa chafu, ametajwa kuwa miongoni mwa watakaoshiriki katika uzinduzi wa kampeni hizo. Hata hivyo, hadi jana jioni kada huyo wa CCM hakuwa ameonekana mjini humo hivyo kuzua wasiwasi kuhusu ushiriki wake.

Vigogo wa CCM waliowasili hapa ni Makamu Mwenyekiti (Tanzania Bara), Pius Msekwa, Katibu Mkuu, Willson Mukama. Mwingine ni Mtunza Hazina, Mwigulu Nchemba ambaye pia ndiye Mratibu wa Kampeni za chama hicho katika uchaguzi huo na viongozi wengine wa wilaya zote za Mkoa wa Tabora.

Awali, kulikuwa na taarifa kwamba Mukama na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wasingekwenda Igunga kwa kile kilichodaiwa kwamba walikuwa hawatakiwi kutokana na kusimamia kidete suala la kujivua gamba ambalo lilimng'oa Rostam.

Jana, makada wa CCM walizua kitimtim ambacho kilianzia kwenye ofisi za chama hicho za wilaya na baadaye kuzunguka mitaa mbalimbali na kadri muda ulivyokuwa unasonga, idadi yao iliongezeka na kuwa shamrashamra za aina yake.

Maandamano hayo yaliandamana na nyimbo za kukisifu chama hicho tawala, viongozi wake pamoja na mgombea wa chama hicho jimboni humo, Dk Dalaly Peter Kafumu.

Kinamama na vijana hawakusita kuonyesha hisia zao pale waliposerebuka mitaani kucheza nyimbo za kukisifu chama hicho ambazo ziliandamana na majigambo ya ushindi kwenye uchaguzi huo utakaofanyika Oktoba 2, mwaka huu.

Chadema juzi kilizindua kampeni zake na leo ni zamu ya CCM. Mwenyekiti Mstaafu wa chama hicho, Mkapa, atakuwa mgeni rasmi kwenye shamrashamra hizo za kupuliza kipenga cha kuanza kumnadi Dk Kafumu.

Mkapa aliwasili hapa juzi na kulakiwa na wanachama wa CCM waliofurika kwa wingi kumlaki. Ilibidi asimamishe gari lake na kuupungua mkono umati wa watu uliofika kumlaki huku akitabasamu na baadhi ya wafuasi wa chama hicho kumsabahi kwa salamu aliyokuwa akiitumia mara kwa mara alipokuwa rais ya "mambo!"

CCM itazindua kampeni hizo katika Viwanja vya Sokoine, mjini hapa na tayari kuna kila dalili za kampeni hizo kuvunja rekodi kutokana na maandalizi yaliyofanyika jana.

Waswahili husema, "Nyota njema huonekana asubuhi" na ndivyo CCM kilivyofanya jana kwa kutikisa jimbo hili kwa maandamano yaliyovuta umati mkubwa wa watu.

Hali hiyo ni tofauti na wakati mgombea wa CCM aliporejesha fomu kimyakimya kutokana na kuwa katika maombolezo ya kifo cha mtoto aliyegongwa na gari na kufariki dunia alipokuwa katika eneo ambalo wanaCCM walikuwa wamekusanyika kumsindikiza Dk Kafumu kwenda kuchukua fomu.

Maandamano ya CCM jana yalikuwa na vimbwanga kadhaa, miongoni vikiwa ni wafuasi hao walioonyesha kuwa na shauku kubwa ya kukipigia debe chama hicho kuingia kwenye tafrani ya kugombea bendera.

Tukio hilo lilitokea kwenye Ofisi ya CCM Wilaya ya Igunga, pamoja na wingi wa bendera ndogondogo za chama hicho zilizomwagwa mbele ya ofisi hiyo, baadhi walikosa.

Baadhi ya wafuasi wa CCM ambao wanakaa maeneo ya mbali na eneo la uzinduzi walianza kufika kwa wingi hapa jana tayari kwa uzinduzi huo.

Kutokana na jimbo hili kutokuwa na magari ya kutosha ambayo ni rasmi kwa abiria, wengi wa wapenzi wa CCM walioingia hapa, walitumia gari aina ya Land Rover ambayo huweza kupita hata kwenye barabara korofi.

Nape aliwahi kuliambia gazeti hili kwamba kampeni hizo zinaratibiwa na CCM Wilaya ya Igunga na kwamba viongozi wowote wa kitaifa watakaopata fursa ya kwenda, watakuwa wamefanya hivyo kwa mapenzi yao na siyo kuagizwa kwenda kufanya kampeni.

Kuna tetesi pia kuwa Rostam atakuwa miongoni mwa wanachama wa CCM watakaompigia debe Dk Kafumu ambaye anapambana na Joseph Kashindye wa Chadema, John Maguma wa SAU na Leonard Mahona wa CUF.

Nape akitangaza uteuzi wa Dk Kafumua alisema katika kufanikisha kampeni za CCM, wanachama waliowania kuteuliwa katika nafasi hiyo na kushindwa wameahidi kuwa watashiriki kikamilifu katika kampeni hizo ili kumnadi mgombea huyo wa chama hicho.

Dk Slaa amfuata Dk Kafumu alikozaliwa
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa jana alitinga kijiji anachotokea Dk Kafumu na kuwaeleza wananchi wa eneo hilo kuwa mgombea huyo hawezi kuwaletea maendeleo kwa kuwa amekuwa ni tatizo ndani ya Serikali.

Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni za mgombea wa Chadema, uliofanyika katika Uwanja wa Mnadani katika Kijiji cha Lugubu, Dk Slaa alisema hivi sasa Watanzania wanahitaji ukombozi kwa kuwa hali zao ni mbaya.

"Nawaambieni Kafumu amekuja kujenga nyumba hapa kwa sababu za uchaguzi tu na wala halali hapa, nawaombeni mumchague Kashindye ambaye mmekuwa naye kwa muda mrefu ili awasaidie kuondokana na umasikini huu uliokithiri," alisema Dk Slaa.
Alisema kuwa wananchi wa Igunga wamekuwa na mbunge wa CCM aliyeachia ngazi kwa miaka zaidi ya miaka 15 lakini hajawasaidia kitu zaidi ya kuwadanganya kila wakati wa uchaguzi ili aweze kutimiza matakwa yake.

"Wananchi mmeliwa sana na CCM sijui kama mnajua maana ya mbunge, Rostam amekuwa hapa kwa zaidi ya miaka 15 je, amekuja kuwaona baada ya kumchagua? Wakati wa kudanganywa umekwisha na msikubali Serikali ya CCM ambayo inawagawia kanga za uongo na baadaye kuwatelekeza," alisema.

Mbunge wa Meatu (Chadema), Sylivester Kasulumbai alisema kuna tatizo kubwa ambalo limeletwa na CCM ambalo ni ufisadi huku akikifananisha chama hicho na fisi ambaye akiwekwa buchani haachi hata kipande cha mfupa.

"Matatizo yapo lakini hayakuletwa na Mungu ni kutokana na kumweka fisi kwenye bucha ambaye haachi hata mfupa, nawaombeni CCM isiwafanye tena hivyo na wala isiwageuze wananchi kama kuku wa kienyeji," alisema Kasulumbai.

Kwa upande wake, Kashindye aliwaomba wananchi wa eneo hilo kumchagua ili waweze kuleta maendeleo kwa pamoja: "Nawaombeni mnichague tuachane na unyonyaji kwani bila CCM maendeleo yanawezekana."
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


 
Guys, hasidi haachi asili yake. Magamba ni kawaida yao kukodisha watu wa kuhudhuria kampeni zao, ni jambo tunalolijua wote.
 
Andika vizuri ueleweke unaandika kisharobaro hii ni Jf, usidhani upo Facebook hapa

Hili ndilo tatizo la kufunguliwa account ya jf na chama check sasa hata jina lenyew limeanza na heruf ndogo.inadhirisha utumiaji wenu wa ubongo ni le ge le ge!
 
na Gazeti hilo la mwananchi haikuishia kusema tu makada wa ccm wasaka wapambe mitaani kwa ajili ya kushiriki Uzinduzi wake wa Kampeni, baadhi ya makada hao ni hawa katika picha hii
 
na hapa ndio walikua wakitafuta wakuwasikiliza mitaani, watu hawaendi , mpaka wahakikishiwe kutakua na Ze Komedi, hahahaaaah

 
weka picha za hayo malori yakishusha watu.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…