Mungi
JF Gold Member
- Sep 23, 2010
- 16,973
- 9,572
Gazeti la mwananchi limeeleza kwa kirefu leo kuhusu maandalizi makubwa yaliyofanywa na ccm jana kuhusu kufanikisha uzinduzi wa mgombea wao leo.Waandishi wa gazeti hilo wameenda mbali zaidi na kutabiri mkutano wa ccm leo utavunja rekodi ya mikutano yote kuwahi kufanywa ktk uwanja wa sokoine.Kama vile haitoshi waandishi wa gazeti pendwa la mwananchi pia wamerudia taarifa ya mapokezi ya mkapa juzi ambapo wamesema alilakiwa na umati mkubwa wa watu kuwahi kushuhudiwa.Source habari kuu Mwananchi leo.
CCM kuvunja rekodi ya CHADEMA ni kitu kilichotarajiwa, kuna habari tulizipata tokea juzi kuwa yapo Malori zaidi ya 100 yameandaliwa kuwabeba watu kutoka nzega, singida na iramba.
Taarifa zimetanabaisha kuwa ugawaji wa khanga, T-shirt na kofia kama kawaida, watakao toka nje ya Igunga watapewa posho za kuhudhuria. kweli pesa za walipa kodi zina kazi nyingi sana.