Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Status
Not open for further replies.
Hapa aliongea pumba. Na raisi akifa, Nape anapewa nchi. Huu ni ujuha.

Licha ya matatizo makubwa tunayopata kutokana na kukosekana kwa pesa, lakini pesa za Kampeni Igunga zinapatikana.
Aibu kubwa nguvu zimeelekezwa Igunga na kusababisha hata Uwanja wa Kimataifa wa Ndege Dar kukosa umeme na ndege kutotua au kuruka. Yote hayo ni madhara ya Uchaguzi wa Igunga ambao haukuwa na budget.

Pesa inayotumika uchaguzi Igunda ni mabilioni ambayo yangeelekezwa mashuleni, ujenzi au kupunguza matatizo ya umeme ingekuwa big up.
 
kumbe huu mtindo wa magamba hawajauacha tu hadi sasa hivi...Nape mwongo kweli na propaganfad zake
 
Kaka haya maneno yako yana walakini mkubwa sana, kwa anayeelewa kusoma kwa maarifa hawezi kukuamini hata punje. Kwanza Intnal banks zipo nyingi sana; Kosa la kwanza hukusema hiyo bank kwa kuwa unaogopa hapa JF tuna wana benki hizo wengi sana, ; Pili hizo 3 billion ni utashi wa mtu kuzitoa ama kuziingiza na napenda kukuweka wazi wamba katapila la ujenzi linanunuliwa kwa zaidi ya milioni 800 ambapo kwa makandarasi wakubwa hiyo billion 3 ni pea nut tu, ; Tatu mkuu, umesema una ushahidi na kwa nini sasa huumwagi kwa kuwa hakuna anayekujua humu kwa kuwa wewe mwenyewe hujiamini, na mwisho; siku ingine usijaze JF kwa propoganda za kipuuzi mjinga wewe...
<br />
<br />
Asante sana!
Kama Watz wote wangefkiria Kimasaburi km ww ukweli kazi ya ukombozi kwa nchi ye2 inahtaj nguvu za ziada.
Sihtaji kuongea meengi ila subiri nicompile justfcation n promising kesho ntazmwaga hapa.
 
Perplex reasoning! The main theme/context is about "UCHAGUZI MDOGO" halafu unazungumzia Rais! Rais akifa (more clearly AKISHINDWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE) automatically kuna Makamu wa Rais; ana take over. Kweli viumbe wazito.

Aliyetoa hoja ya kurithi nafasi ya urais hakuwa na maana ya hoja ya msingi, ila ametolea mfano kama inavyotokea kama kiti cha rais kuwa wazi sheria ipo namna ya kujaza bila uchaguzi, na hivyo anashauri inafaa kuwepo na utaratibu kama huo inapotokea kiti kuwa wazi bungeni au madiwani. Nimemweliewa vizuri tu.
 
Bora ungesubiri uone kuliko kuleta tathmini njaa hapa.
<br />
<br />
Mbona umekuwa mkali hivyo? Tathmini japo iko qualitative zaidi lakini kuna observation imefanyika. Nakubaliana nawe kwamba ngoja tusubiri.
 
Unasema walisomba watu mbona sijaon viashiria jamani hebu sema nikasome wapi ili nijiridhishe juu ya tukio la kusomba watu toka mikoa na wilaya za jirani .
 
Tujifunze mambo ya demokrasia toka kwa waliotufundisha mataifa makubwa. Aliyoyasema Halima Mdee ni sahihi kwa vile hata mataifa makubwa inapotokea jimbo la uchaguzi kuwa wazi wana utaratibu wa kuteua mtu wa kushikilia hadi uchaguzi utakapofikia muda wake ili kuongoa gharama za uchauzi.

Obama alipochaguliwa kuwa Rais wa Marekani, nafasi yake ya Useneta ilijazwa jimboni kwake kwa kuteuliwa mwakilishi mwingine hadi uchaguzi mwingine ulipowadia. So what is wrong?
naweza kusema mlezi wetu wa kidemokrasia au mfumo wa kiuchaguzi ni uingereza,sasa jee huku uingereza hawafanyi by elections kwa kuogopa gharama?
 
Ongeza na hizi picha:

View attachment 36990
Hii chupa ya Mwenyekiti Mbowe imejazwa nini? inafanana na wiski.
Nashawishika kusema kuwa chupa ya maji imetumika kuficha kilevi!

View attachment 36991
Hwa nao vipi? Wanamuiga mwenyekiti wao?
Hivi CDM hawawezi kufanya kampeni bila ulevi wa kupindukia? Matokeo yake ni kumwagia tindikali watu wasio na hatia.

WAKATI UMEFIKA KUKOMESHA HUU UHUNI NA KUWAADHIBU KWA KUWANYIMA KURA.

Hahaha, hao ndio wanacdm, huyo jamaa hapo sijui amevuta ya wapi.....CCM wanagawa wali, CDM wanagawa viloba na msuba. Kweli hii ni sherehe kwa vijana wetu, unapiga konyagi/msuba kwenye mikutano ya CDM halafu unafata wali wa CCM. hii ni bora kuliko fiesta, tena mwezi mzima.
 
sio pumba....hata huko marekani hawarudii rudii chaguzi kwa staili yetu....

ni bora chama kinachoshika jimbo kifanye chaguzi ya ndani....au tuje na sysytem nyingine itakayokubalika.....

kuna system nyingi tu.....

Hiyo ni pumba mkuu wala usilete ubishi wa watumia Masaburi hapa!

Hizo ndo gharama za demokrasia! Kutuambia Marekani wanafanyaje hilo hatukuungi mkono. Kwani umeshajiridhisha Marekani wanafanyaje? Mbona huo uchaguzi wa aina hiyo huwa tunausikia na huko upo! Usilete porojo hapa.

Kama yeye Mdee anaona muda na raslimali zinapotea bure si akishauri chama chake na vyama vingine vya upinzani wasiweke wagombea, ili jamaa apite bila kupingwa! Vinginevyo na anyamaze milele!!
 
naweza kusema mlezi wetu wa kidemokrasia au mfumo wa kiuchaguzi ni uingereza,sasa jee huku uingereza hawafanyi by elections kwa kuogopa gharama?

uingereza haina rais wala makamu wa rais
system yao ya bunge linaundwa kwa viti na ndo waziri mkuu anapatikana hivyo...
sio sawa na sisi...
 
democratic system mst follow democratic principles, no shortcut, halima mdee isn't perfect she can make mistakes.

Mkiogopa cost hata katiba mpya haitakuwa na uhalali kuliko ya zamani.

Ni kweli kabisa mkuu, hatuwezi kukimbia majukumu sababu ya gharama. BTW, mtu akichaguliwa na Chama hatakuwa mwakilishi wa wananchi ila Chama. Wakati mwingine sio vizuri kucopy na kupaste watu wanavyofanya mambo, democracy zinatofautiana.
 
quote_icon.png
By The Boss
kama hujaelewa uliza uelezwa sio kuropoka non sense

hivi ni nchi zote duniani zina chaguzi ndogo?
nchi zingine wanafanyaje
???????

unafikiri demokrasia imeanzia kwetu sio?
hALIMA MDEE SI MESEMAJI WA DEMOKRASIA YA WATNZANIA
 
Wengine waondoka mkutanoni (Mwananchi)

Wakati Mkapa akiendelea kuhutubia, baadhi ya watu wakiwa kwenye makundi walianza kuondoka kwenye mkutano huo. Wengi waliohojiwa na Mwananchi Jumapili walisema hakuna jipya katika hotuba ya Mkapa na kuongeza kuwa, waliyokuwa wakiambiwa na wapinzani yalithibitishwa na Mkapa mwenyewe.

Walitoa mfano kuwa Mkapa alipoingia madarakani, makusanyo ya Serikali kwa mwezi yalikuwa ni Sh28 bilioni, lakini hadi anaondoka, makusanyo hayo yalikuwa ni Sh400 bilioni na kuongeza kuwa ni wazi Serikali ina fedha, lakini hazitumiki kwa shughuli za maendeleo.
 
Licha ya matatizo makubwa tunayopata kutokana na kukosekana kwa pesa, lakini pesa za Kampeni Igunga zinapatikana.
Aibu kubwa nguvu zimeelekezwa Igunga na kusababisha hata Uwanja wa Kimataifa wa Ndege Dar kukosa umeme na ndege kutotua au kuruka. Yote hayo ni madhara ya Uchaguzi wa Igunga ambao haukuwa na budget.

Pesa inayotumika uchaguzi Igunda ni mabilioni ambayo yangeelekezwa mashuleni, ujenzi au kupunguza matatizo ya umeme ingekuwa big up.
kwa hiyo ulitaka vyama vitumie fedha za kampeni kupeleka umeme airport?usituwekee maneno mdomoni mkuu,ni asilimia ngapi ya watanzania wanafaidika na safari za ndege?sanasana kodi zetu zinatumika vibaya kuwapeleka viongozi nje bila tija yoyote.
 
Hiyo ni pumba mkuu wala usilete ubishi wa watumia Masaburi hapa!

Hizo ndo gharama za demokrasia! Kutuambia Marekani wanafanyaje hilo hatukuungi mkono. Kwani umeshajiridhisha Marekani wanafanyaje? Mbona huo uchaguzi wa aina hiyo huwa tunausikia na huko upo! Usilete porojo hapa.

Kama yeye Mdee anaona muda na raslimali zinapotea bure si akishauri chama chake na vyama vingine vya upinzani wasiweke wagombea, ili jamaa apite bila kupingwa! Vinginevyo na anyamaze milele!!

umepewa mfano wa kiti cha senate cha obama kilivyorithiwa
marekani wana demokrasia ya miaka zaidi miaka 300.....
wewe una jeuri ya kujifanya hutaki kusikia tofauti na mawazo yako
demokrasia yenyewe huijui...
kwenye demokrasia huwezi mwambia mtu anyamaze
hili ni wazo lake ambalo wengine tunaona lina maana.....
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom