Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Status
Not open for further replies.
Hahhahaaaa unajifanya hujaskia eeeeh, haya anasema hivi mlichezeana rough wenyewe, dogo kapewa pesa kwa ajili ya kung'oa mabango ya CDM sh.150,000Ts akawazidi wenzie, jamaa wakaamua kumfanyizia na kwamba hakuna mtu wa CDM aliyehusika, hapo pia hujaelewa? njoo na jipya tena kama unalo
ANASEMAJE mbona sion na kusikia chochote?
 
Yaani hizi picha mbili zimenichekesh mpaka basi, huu ndiyo haswaa uungwaji mkono wa CCM!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

kweli hii kali. wanatumia njaa iliyoko ndani ya jamii kuomba kura. Hapo wanaoneshwa kidogo alafu wanaambiwa walipiga kura kwa sisiemu watakula zaidi loh!!!
 
SIKU moja baada ya uzinduzi wa kampeni za CCM, juzi kutikisa mjini hapa, baadhi ya makada wa vyama vya upinzani wamekiri kwamba ni vigumu upinzani kushinda kiti hicho cha ubunge. Kampeni hizo zilizozinduliwa na Rais mstaafu Benjamin Mkapa na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi, zimeibua hisia za wananchi, kutokana na mambo mbalimbali yaliyowagusa. Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, mmoja wa makada wa CHADEMA alisema kuwa walidhani uzinduzi wa CCM ungedoda, lakini imekuwa kinyume cha matarajio yao. Alisema idadi ya watu waliohudhuria katika mkutano huo, uliwavunja nguvu za kuendelea kufanya kampeni, kwani imeonyesha dhahiri jimbo hilo bado ni mali ya CCM. "Sikufichi, pamoja na kwamba mimi naichukia CCM, lakini kwenye hili la uzinduzi halina ubishi, jamaa bado wanakubalika na kweli hapa upinzani tunasindikiza tu, kwani wale watu sio mchezo," alieleza.

Alieleza kwamba pamoja na kwamba uzinduzi uliofanywa na CHADEMA Septemba 8, ulikuwa na watu, lakini ule wa CCM ulifunika mara tatu zaidi, jambo linaloonekana dhahiri kwamba upinzani una kazi ngumu. "Tutajitahidi kuendelea kufanya kampeni, lakini mpaka sasa kama hatutumii hisia za uchama, lazima ukiri kwamba jimbo hili ni la CCM, na ni ndoto kwenda upinzani," alisisitiza. Akijibu swali juu ya kwa nini, hawakuiunga mkono CUF kutokana na mgombea wake kuwa na mtaji mkubwa kisiasa, alisema hakuna msimamo wa pamoja juu ya vyama vya upinzani, ndiyo maana kila chama kimeamua kusimamisha mgombea wake. "Kweli mgombea wa CUF ana mtaji mkubwa kuliko wa kwetu (CHADEMA), na kama tungeungana ni wazi tungewaangusha CCM, lakini bado vyama vya upinzani hatujawa na sauti moja," alikiri.

Source: Gazeti la Uhuru, Jumatatu, Septemba 12, 2011

Katika hali ambayo inadhihirisha kukata tamaa kwa upinzani, juzi akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro, alikiri kwamba sio rahisi kuiondoa CCM madarakani, kupitia siasa za mapambio zinazofanywa na baadhi ya vyama vya upinzani.

Mtatiro alikiri kwamba CCM bado ni chama imara, kina nguvu na miundombinu mingi ya ushindi, hivyo bila kutafuta mwafaka wa pamoja wa upinzani haitakuwa na maana.

"Wenzetu CHADEMA mwaka jana hawakusimamisha mgombea na sisi mgombea wetu alipata kura 11,000 tulidhani wangetuunga mkono, badala yake wamekuja kugawa kura Igunga,
"
alieleza.

Baadhi ya wananchi walisema kwamba uzinduzi uliofanywa na CCM na kueleza sera zake, kumewafanya wananchi kuendelea kuwa na matumaini na chama hicho.

"Unajua wapinzani ni watu wa ajabu sana, kila kitu kwao tatizo, hawajui hata historia ya jimbo hili, lilikuwa mwisho kwa maendeleo mkoani Tabora, lakini leo ni wa kwanza, lakini wanasema hakuna kitu kilichofanyika," alieleza Juma Herman.

Herman alisema kwamba wananchi wamekuwa wakitaka kusikia sera za vyama, lakini wanachukizwa na sera za kutukana viongozi wa kitaifa na kupakana tope, kitu ambacho hakiwasaidii wananchi.

"Hivi mtu akisema huyu mbaya, mwananchi anajua ubaya wake nini... ni bora wakaeleza sera na namna ya kuwasaidia wananchi, lakini wao matusi na maandamano, ambayo hayana faida kwetu," alieleza.

Alisema CCM itaendelea kuongoza jimbo hilo na kushika dola kutokana na mikakati yake imara ya kuwaondolea wananchi umasikini na kuwahimiza katika kufanya kazi kuliko kuandamana.

Katika uzinduzi wa kampeni hizo, Mkapa aliwataka wananchi kuwapuuza CHADEMA kutokana na kukosa sera nzuri za kuendeleza nchi zaidi ya kuandamana bila kutoa sera mbadala.

Katika hatua nyingine, baadhi ya vijana wamelaani kitendo kilichofanywa na wafuasi wa CHADEMA cha kummwagia tindikali kijana mwenzao.

Jacob Maduhu (25) alisema kwamba kitendo hicho kimewasikitisha vijana na imekuwa matusi kwao kutokana na chama hicho kujitangaza kwamba ni mkombozi wa vijana.

"Hivi mkombozi wa vijana anaweza kuwaua vijana, hapana hiki ni chama cha mauaji, huwezi kumuharibia maisha kijana unayetaka kumkomboa kwa kumwagia tindikali," alisema Mahudu.

Naye Salma Hamisi alisema kwamba amekuwa haelewi maana ya nguvu ya umma inayohubiriwa na chama hicho, kumbe maana yake ni kuangamiza umma kwa tindikali.

"Kila siku utasikia nguvu ya umma, hawaelezi sera zao, wao ni fujo na maandamano na kuwapiga wanaopingana nao, hizi ni siasa za wapi, maana waasisi wa taifa walitujengea siasa nzuri, sasa hizi za kumwagiana tindikali si zitatumaliza?" aliuliza.
Chanzo tafwadhali au ni UHURU PUBLICATION!
 
biashara kama hiyo ni ya CCM muda ukifika watasemana wenyewe kwa wenyewe, tunamtaka na aliyetoa hizo hela awekwe hadharani.

siasa uchwara zinaendelea Igunga, naogopa asijetajwa yule aliyeachana na siasa 'uchwara' kuhusika
 
Regia bana,

"M. Mchemba" anasema waliofanya kitendo hicho ni CDM 'people's power'

Anayesema ni CCM ni huyo kijana mwingine anajiita mwana CCM. Je tutaamini vipi ni mwana CCM kweli na nyie CDM hamjampa pesa aseme hivo?
Hiyo video nyie wenyewe ndo mmeiandaa.

Utata unabaki pale pale.
 
Kamanda Regia mbona kila Mtanzania alijua tangu siku ya pili yake tu kwamba ni wale vijana wa USALAMA WA CCM ndio waliohusika na huo mchezo wa tindikali Igunga kama ilivyowahi kutokea miaka fulani Dar.
 
Jana nilimwambia Member anayekuja kwa jina la Mbopo kuwa hii kesi imewakalia vibaya ni muda tu unasubiriwa ili wahusika watajwe ndiyo maana waliamua kukodi ndege ya private kumpeleka mbali Muhimbili ili kumtenga na wezake wa karibu na kumfundisha jinsi ya kujibu, lakini nawaambia ukweli utawekwa wazi, Mwigulu katoa hela kwa makundi mawili tofauti halafu kesho yake anapanda jukwaani kulalamika shame on you muuaji mkubwa.
 
Nape umekwisha ulitoa pesa ili kucha picha za CHADEMA vijana wako wazidiana kete wakamwangiana tindikali ukaenda kwenye mitandao ya kijamii kusema kuwa nai CHADEMA ndiyo wamefanya kazi hiyo sasa njoo na jingine....tunajua njia ya kubandua picha za chama pinzani huwa mnaitumia sana...
 
Mkutano wa ccm watu wengi walienda kutizama Ze Comedy siyo hotuba ya ufunguzi ya Rais Mstaafu kwani hana jipya la kuwaeleza watanzani yeye mwenyewe ni Fisadi Mkubwa,Ingekua siyo kinga aliyonayo alitakiwa ashtakiwa kwenye kesi ya akina Mramba. Ipo siku watakamatwa wote na kushitakiwa na siyo mbali baada ya uchaguzi wa 2015, watakoma!
 
Regia bana,

"M. Mchemba" anasema waliofanya kitendo hicho ni CDM 'people's power'

Anayesema ni CCM ni huyo kijana mwingine anajiita mwana CCM. Je tutaamini vipi ni mwana CCM kweli na nyie CDM hamjampa pesa aseme hivo?
Hiyo video nyie wenyewe ndo mmeiandaa.

Utata unabaki pale pale.
Unategemea atasema nini wakati yeye ndiye mwenye dili na mtoa pesa wamemtia kilema cha maisha kijana wa watu kwa tamaa za ubunge najua akipona atayasema yote, CCM wanarudia yale yale ya Kubenea ila uharamia huu utalipwa hapahapa.
 
ha ha ha nadhani gazeti la uhuru la leo litakuwa limeshaujua ukweli..naomba kesho lisahihishe habari wa liochapa leo..magamba bwana ufisadi mpaka kwa wananchi wa kawaida
 
Hawa CCM si waliwahi hata kumwaga "unga unga" bungeni! Pamoja na kuonekana na kamera za ukumbi wa bunge bado wakabisha. Kwa hiyo hawa watu kudhuriana ni kawaida yao.

Wapi Papaa Kolimba? Wapi Mamaa Mbatia? Wapi
 
msosi+ze komedi+ wanatarabu mlitegemea nini?? Chadema watu walifuata sera na si chakula kama ambavyo magamba wamefanya
 
Siasa chafu za kufanyia jaribio la tindikali kwenye mwili wa huyu kijana masikini mwenzetu wa Igunga si nzuri.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom