Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Status
Not open for further replies.
Moderators wa JF, Max na wenzako acheni kuihujumu CCM kwa kupotosha suala la tindikali. sisi tukiweka ushahidi humu au post zinazoeleza ukweli moderator hazipandishi. Na huu ni mkakati wa CDM kutengeneza hizi video na sehemu wanayotengenezea ni kwenye guest moja inaitwa MISANA LODGE. mtaumbuka siku si nyingi.
 
NINACHOFAHAMU wajinga na wezi bado wanaiunga mkono CCM.
NISICHOFAMU wajinga na wezi nchini wako wangapi.

Mkuu nadhani ni jazba tu na uelewa wako mdogo kudhani kuwa wana CCM ni wajinga.
Wako watu makini, wenye kila sifa nzuri tu ambayo hutokaa ufikie lakini ni wana CCM
Nadhani tunajidanganya sana kudhani CCM wote wabaya na CDM/wapinzani ndo wazuri.
Niliwahi kuwa na mawazo kama yako lakini nimewafuatilia wana siasa wetu na naconclude hivi.
TZ haitapona kwa kubadilisha vyama, bali kupata mtu (Rais) makini mwenye uwezo na nia dhabiti na si bla bla na majungu tu.
Mtu huyo aweza toka CCM, CDM au popote tu.
Time will tel.

Note: Mi si mwana chama wa chama chochote, ni mpiga kura tu kwa mtu makini regardless chama chake.
 
<br />
<br />
Mimi tangu nipo mtoto nimekua nawaamini sana walemavu ni watu waaminifu sana lakini dada yangu Regia kama umejiingiza kwenye propaganda hizi za Chadema unaondoa hata uaminifu tulio nao kwa walemavu!

Watu kama nyinyi mnanikera sana majibu yenu mnapoambiwa ukweli. Huyu Mwangulu mropokaji hapo juu anaongelea mambo ya kuota, lakini kijana mwenyewe ni mwana Igunga inaonyesha ni kiasi gani kimemuuma mpaka akaamua kuwa muwazi. Na kama amejitokeza na kusema yote hayo inamaana anajua vitu vingi na hayupo mwenyewe. Tuungana wote na kutokomeza huu mchezo wa ccm kutoa watu kafara, kunaendelea kuupalilia kesho watakuvuna wewe.

Hata Pilato alisema sioni kosa la mtu huyu, mnamsulubisha kwa kosa gani wakati ni nyinyi wenyewe mnavunja sheria zenu wenyewe. Lakini walijua ukweli uliokuwa unasemwa ndio maana wakasema ni lazima mtu mmoja afe kwa ajili ya watu. Sasa wengine wanatafuta sababu za kipumbavu ili wapate madaraka. Na Tanzania tutathaminiana endapo tutashirikiana kutokomeza hii hali ambayo ilishaonekana ni kawaida huko ccm.

Mimi ninajiuliza lakini sipati jibu hawa chadema walijua je kuwa kuna watu wa ccm anatoa mabango yao usiku huo wa saa 5 usiku, na nyinyi watu wa ccm kwa nini msingefanya hiyo kazi mchana watu wakawaona. Nisingependa kumsema huyu kijana lakini majibu ya hawa watu wa ccm ndio yanafanya mpaka watu wanatoa lugha ambazo hatarajii.
 
Hawa CCM si waliwahi hata kumwaga "unga unga" bungeni! Pamoja na kuonekana na kamera za ukumbi wa bunge bado wakabisha. Kwa hiyo hawa watu kudhuriana ni kawaida yao.

Wapi Papaa Kolimba? Wapi Mamaa Mbatia? Wapi

daah! Huogopi? Watakukolimba!! Umenikumbusha mengi kati ya mabaya niliyoshuhudia katka miongo hii mitatu!, nyaraka zilizo kwenye shelf moja pale ofisi ya ...... zinatisha!
 
Mkuu naomba unikosoe kwa hoja lakini usiuhusishe ulemavu wangu..Jenga hoja lakini si vema kushambulia mumble ya watu,hakuna mtu aliyemuomba MUNGU kuwa jinsi alivyo,awe mbaya,mzuri,mwenye ulemavu au kutokuwa na ulemavu..

Hakuna uhusiano wa ulemavu na kuwa muaminifu au kutokuwa mwaminifu...Haya mengine ni tabia na ulemavu ni hali.

Usicheze na MUNGU,Mshukuru MUNGU kama huna ulemavu wa aina yeyote ile.

MUNGU akubariki sana na nakuombea MUNGU asikupe ulemavu ama wewe au yeyote yule katika familia yako..

Mimi kwa haraka namuona anayehusisha ulimavu wa viungo na Hoja ambayo inatakiwa ijibiwe kwa hoja, ni Lazima atakuwa Mlemavu wa akili!! Na ikumbukwe katika hii dunia hakuna ulemavu mbaya kama ulemavu wa akili!! Duh Maskini hadi mtu anajua Kutumia mtandao wa Jamii huku ana ulemavu wa AKILI!! NA MUNGU AMSAMEHE NA KUMREHEMU!! DADA REGIA KANYAGA TWENDE!! HAJUA HUYU BWANA/BIBI KESHO ANAWEZA KUPANDA BUS AU HATA HILO GARI LAKE (KAMA ANALO) AKAJIKUTA KATIKA HUO ULEMAVU WAKE WA AKILI AKIONGEZEA ULEMAVU WA KIUNGO? Hujafa hujaumbika ndugu!!!!!
 
<br />
<br />
Mimi tangu nipo mtoto nimekua nawaamini sana walemavu ni watu waaminifu sana lakini dada yangu Regia kama umejiingiza kwenye propaganda hizi za Chadema unaondoa hata uaminifu tulio nao kwa walemavu!

Watu kama nyinyi mnanikera sana majibu yenu mnapoambiwa ukweli. Huyu Mwangulu mropokaji hapo juu anaongelea mambo ya kuota, lakini kijana mwenyewe ni mwana Igunga inaonyesha ni kiasi gani kimemuuma mpaka akaamua kuwa muwazi. Na kama amejitokeza na kusema yote hayo inamaana anajua vitu vingi na hayupo mwenyewe. Tuungana wote na kutokomeza huu mchezo wa ccm kutoa watu kafara, kunaendelea kuupalilia kesho watakuvuna wewe.

Hata Pilato alisema sioni kosa la mtu huyu, mnamsulubisha kwa kosa gani wakati ni nyinyi wenyewe mnavunja sheria zenu wenyewe. Lakini walijua ukweli uliokuwa unasemwa ndio maana wakasema ni lazima mtu mmoja afe kwa ajili ya watu. Sasa wengine wanatafuta sababu za kipumbavu ili wapate madaraka. Na Tanzania tutathaminiana endapo tutashirikiana kutokomeza hii hali ambayo ilishaonekana ni kawaida huko ccm.

Mimi ninajiuliza lakini sipati jibu hawa chadema walijua je kuwa kuna mtu anatoa mabango usiku huo wa saa 5 usiku, na kwa nini wasingefanya hiyo kazi mchana watu wakamwona. Nisingependa kumsema huyu kijana lakini majibu ya hawa watu wa ccm ndio yanafanya mpaka watu wanatoa lugha ambazo hatarajii.
 
Moderators wa JF, Max na wenzako acheni kuihujumu CCM kwa kupotosha suala la tindikali. sisi tukiweka ushahidi humu au post zinazoeleza ukweli moderator hazipandishi. Na huu ni mkakati wa CDM kutengeneza hizi video na sehemu wanayotengenezea ni kwenye guest moja inaitwa MISANA LODGE. mtaumbuka siku si nyingi.

Peleka ushahidi wako polisi!! wewe ndugu Unaishi Nchi Gani? Hujui taratibu za kisheria?Au Feleshi anasubiri huo ushahidi wako
 
Moderators wa JF, Max na wenzako acheni kuihujumu CCM kwa kupotosha suala la tindikali. sisi tukiweka ushahidi humu au post zinazoeleza ukweli moderator hazipandishi. Na huu ni mkakati wa CDM kutengeneza hizi video na sehemu wanayotengenezea ni kwenye guest moja inaitwa MISANA LODGE. mtaumbuka siku si nyingi.
Nepi acha kulialia umeyataka mwenyewe ngoja unyolewe hivi ukijua guest wanayotengenezea ndiyo utafanyaje.
 
Kiukwaeli hali ya Igunga bado ni tete na bado ipo kwenye mabano, but natoa ushauri kwa vyama vya upinzani kuwa wawe makini saaaaana na zile kura za MOTO, zilizoiangusha iliyokuwa ikijulikana kama ngome ya CUF hapo TEMEKE miaka ya hivi karibunI iiliyopita na kutaka kumfanya mwenyekiti wao kwenda Misri na South Africa kuzifanyia utafiti but ghafla bin vuuuu kapewa shavu na sersikali iliyokuwa madarakani kisha kasau wajibu wake yeye kama mwenyekiti wa chama.
 
[h=1]UCHAGUZI IGUNGA:[/h]


Kura zikipigwa leo
*CCM kupata asilimia 39
*CHADEMA asilimia 37
*CUF kupata asilimia 18
*Vyama vingine asilimia 6
Na Waandishi Wetu, Igunga na Dar
Katika utafiti huo ambao umefanyika katika kata 20 za jimbo hilo, wastani wa watu 50 wenye umri kati ya miaka 20 hadi 50 walihojiwa katika kila kata na kutoa maoni yao.
Matokeo ya utafiti huo yameonesha kuwa, kama uchaguzi huo ungefanyika wiki hii, basi matokeo yangekuwa kwamba CCM ingepata asilimia 39, CHADEMA asilimia 37, CUF asilimia 18 huku vyama vingine vilivyosalia vikigawana asilimia sita.
Kata zilizohusika kwenye utafiti huo ni Igunga, Itumbi, Bukoko, Isakamalwa, Nyandekwa, Mbutu, Kining’ila, Mwamashinga, Choma, Kinungu, Ntobo, Igurubi, Hundwa, Mwashiku, Ziba, Ndembezi, Nkinga, Ngulu, Sungwi na Mwisi.
Wagombea katika uchaguzi huo ni Mwalimu Joseph Kashindye (CHADEMA), Dk. Peter Kafumu (CCM), Leopold Mahona (CUF), Hemed Dedu (UPDP), Said Cheni (DP), John Maguna (SAU) na Stephen Makingi (AFP).
Utafiti huo umeonesha kuwa wanaokiunga mkono CCM wanajivunia mtandao wa wanachama wake katika maeneo mbalimbali jimboni, ingawaje wanakiri moja kwa moja kuwapo kwa mgawanyiko na kuwapo kwa makundi.
“Sisi wana-CCM tunao uwezo wa kuwakabili vilivyo wapinzani wetu, kwa sababu watu tunao, sera zetu zinaeleweka, lakini tatizo letu ni kutoelewana wenyewe kwa wenyewe, hili linaweza kutuangusha.
“Sasa hivi baadhi yetu wanawaona viongozi wa kitaifa kama wasaliti na watu wasiolitakia mema jimbo letu, hasa baada ya aliyekuwa Mbunge wetu Rostam Aziz kujiuzulu kutokana na siasa chafu ndani ya chama.
“Tatizo ni kubwa zaidi, kwa sababu baadhi ya wenzetu wameshasema wazi kuwa hawatapiga kura, na kuna uwezekano wengine wakawapigia wapinzani ili kulikomoa kundi au watu fulani, hii hali si nzuri kwa chama chetu,” alisema Mwenyekiti wa moja ya matawi maarufu ya CCM Igunga Mjini.
Kwa upande wa CHADEMA, utafiti umebaini kuwa kinaungwa mkono na makundi ya vijana na wafanyabiashara, makundi ambayo yanaonekana kuwa na kiu ya manadiliko.
Kutokana na ukweli huo, chama hicho ambacho kinatarajiwa kutoa upinzani mkubwa kwa CCM na CUF, kinatarajia kupata kura nyingi katika maeneo ya mjini, ambako umaarufu wake umekuwa ukikua kwa kasi tangu kuanza kwa vuguvugu la uchaguzi ambao unatarajiwa kufanyika Oktoba 2, mwaka huu.
Pia wananchi wengi ambao walihojiwa na kuonekana kukiunga mkono CHADEMA, ni wale ambao wanakabiliwa ugumu wa maisha unaotokana na kupanda kwa bei za bidhaa muhimu kwa ajili ya matumizi ya kila siku.
Kundi hili linaonekana kufurahishwa na sera ya chama hicho (CHADEMA) ya kupambana na umasikini kwa kuhakikisha rasilimali za nchi zinanufaisha wananchi husika, pamoja na kupigania bei bora za mazao ya biashara, ikiwamo pamba inayolimwa kwa wingi jimboni huo.
Kwa upande wa CUF, wananchi wengi waliohojiwa ambao wanaonekana kukiunga mkono wanaweka karata yao zaidi kwenye idadi ya kura 11,000 alizopata mgombea wao katika Uchaguzi Mkuu uliopita.
“Sisi tayari tuna kura zetu zaidi 10,000i, kwa hiyo tunahitaji kuweka nguvu zaidi kuziongeza, sera zetu zinafahamika Igunga, mgombea wetu ni mtoto wa hapa hapa, kwa hiyo tunachosubiri ni ushindi wa kishindo, labda tuhujumiwe,” alisema mfanyabiashara mmoja katika soko la Igunga, aliyejitambulisha kwa jina la Doto Maganga.
Matatizo ya wananchi wa Igunga
Wakati kampeni zikiingia siku ya pili leo, uchunguzi umebaini matatizo kadha wa kadha yanayowakabili wapigakura wa Igunga, matatizo ambayo wanatarajia Mbunge wao mpya atayapatia ufumbuzi.

Miongoni mwa matatizo hayo ni uhaba wa chakula unaolikabili jimbo hilo kutokana na uhaba wa mvua, tatizo ambalo kwa kiasi kikubwa limeathiri shughuli za maendeleo hasa maeneo ya vijijini.

Aidha, kuna hali ya umasikini wa kutisha kama ilivyo kawaida katika sehemu nyingi nchini ikichochewa na mfumuko wa bei, kupanda na kushuka kwa bei za mafuta na kudorora kwa shughuli za uchumi kama vile biashara na kilimo.

Vile vile kuna kuporomoka kwa bei ya pamba, zao kuu la biashara kwa wakazi wa jimbo hilo kumezidisha ukali wa maisha, ingawaje kumekuwapo juhudi za kuhakikisha wakulima wanapata bei nzuri sokoni.

Jimbo la Igunga pia linakabiliwa na tatizo sugu la miundombinu ya barabara, tatizo ambalo kwa kiasi kikubwa limeathiri mawasiliano kati ya sehemu moja hadi nyingine.

Taarifa zaidi zimesema kuwa, pamoja na Mbunge aliyejiuzulu kujitahidi kutatua matatizo yaliyopo kwenye sekta za afya na maji, bado nguvu kubwa inahitajika kukidhi mahitaji wa wana-Igunga.

Wagombea wa CCM, CHADEMA, CUF wanavyotazamwa
Mgombea wa CCM, Dk. Peter Kafumu, amewahi kugombea mara kadhaa, ambapo mara ya mwisho alianguka kwenye kura za maoni, wakati Mbunge aliyejiuzulu, Rostam Aziz, akiibuka mshindi.

Kwa sasa yeye ni Kamishna wa Madini katika Wizara ya Nishati na Madini, na ni msomi aliyebobea katika masuala ya madini akiwa na Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Madini.

Lakini uchunguzi umebaini kuwa, kwa wakazi wengi wa Igunga, Dk. Kafumu anaonekana si mwanasiasa, si mkazi wa Igunga na pia ni mtu ambaye ni vigumu kujichanganya na watu, ingawaje anatajwa kuwa anaweza kuukwaa uwaziri kama atashinda, ikiwa yatafanyika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri.

Kwa upande wake, mgombea wa CHADEMA, Mwalimu Joseph Kashindye, yeye ni Mkaguzi wa Elimu wa Wilaya ya Igunga, pia ana historia ndefu katika Sekta ya Elimu.

Alianza kazi ya ualimu akiwa kama Mwalimu wa UPE, lakini amekuwa na bidii kubwa katika kujiendeleza, na hivi sasa ni mwanafunzi wa Shahada ya Uzamili katika masuala ya elimu.

Kwa wakazi wengi wa Igunga, anaonekana kuwa ni mkazi mwenzao, anafahamu matatizo ya siku hadi siku ya Igunga, pamoja na yale yanayowakabili walimu na wanafunzi.

Kuhusu mgombe wa CUF, Leopold Mahoma, Rai haikuweza kupata taarifa zake kwa kina, lakini kama alivyo mgombea wa CHADEMA, yeye pia ni mkazi wa Igunga, na katika Uchaguzi Mkuu uliopita, alishika nafasi ya pili nyuma ya mgombea wa CCM, ambapo alipata kura 11,000.
 
MONDAY, 12 SEPTEMBER 2011 19:45 NEWSROOM


* Wakaleta tena balaa za Tarime na Arusha
KATIKA mjadala na vimbwanga vya siasa vilivyo katika chati, watu wanasema &#8216;mambo yote yako Igunga." Ni harakati za kumsaka mrithi wa Rostam Aziz, aliyekuwa mbunge wa Igunga kwa tiketi ya CCM na baadaye akajiuzulu.

CCM imeshapiga kambi ya uhakika huko, ikiwania kukirejesha kiti hicho katika imani kwamba &#8216;kiti ni chetu.' Ilitarajiwa kwamba siasa na kampeni zingenoga sana Igunga, sera za kukosoana majukwaani ndio zingetawala, lakini kwa siasa za Chadema huko Igunga, imedihirisha si utaratibu wao. Wamekuwa mstari wa mbele kutoa maneno mengi, kashfa na propaganda nyingi.

Wamekuwa wakitafuta ushindi kupitia propaganda za majukwaa ya kisiasa. Kama alivyonena Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga, kwamba &#8216;hivi karubuni, siku zote mbwa anayebweka sana, huwa haumi,' hivyo hilo limekuwa haliumizi kichwa CCM ambayo imeenda katika matendo zaidi.


Ushuhuda wa &#8216;matendo zaidi' ya CCM dhidi ya &#8216;wabwekaji' ni umati uliofurika katika Uwanja wa Sokoine, kumsikiliza Mwenyekiti mstaafu Mzeee Benjamin Mkapa, alipozindua kampeni za mgombea wake Dk. Peter Kafumu, msomi wa madini mwenye shahada nne na stashahada mbili za uzamili mbili.


Si kwamba hayo yameanzia huko, bali killa wanakopita mambo ni hayo hayo. Siasa za chama hicho ni lazima ziwe na &#8216;harufu za damu.' Tukumbuke kilichojiri Arusha na Mwanza.


Kampeni zinaporuhusiwa rasmi, ni jambo la kawaida wanasiasa na wafuasi wao wakazunguka sehemu mbalimbali kulingana na ratiba walizopangiwa.

Pia, mazingira ya kampeni hutawaliwa na mengi katika propaganda zake, picha za wagombea kubandikwa katika maeneo ya umma, muziki kupigwa na vibweka vya namna mbalimbali, ili mradi ni matendo yaliyovunja sheria.

Uchaguzi, pia maana yake ni mtu anajitolea kupeperusha bendera ya chama fulani, kuhakikisha anasimamia sera zake kuwaletea maendeleo wananchi husika, huku wananchi wakiendelea kuishi kwa amani na utulivu. Kinyume na hicho, mhusika hafai kugombea nafasi hiyo.


Chadema kwa kuendelea kudhihirisha ni watu wa fujo, makada wao wanaonekana kutumwa na mtandao wa mamlaka ya chama, walimvamia na kumpiga kisha kumwagia tindikali kada wa CCM.


Kisa, ni kwamba alikuwa anabandika picha za mgombea wake, Dk.Kafumu, jambo ambalo ni haki yake ya kisiasa na kisheria, kwani kampeni zilisharuhusiwa.

Simulizi za tukio na namna walivyoathirika wahusika, kilimshitua karibu kila mtu nchini na nje ya nchi, mpenzi wa siasa na asiyependa siasa.

Ni kitendo ambacho daima si ubinadamu hata kidogo. Sijui inajenga picha gani, jumuia ya kimataifa na jamii ya wageni waishio nchini? Watakaa wajiulize, hizi ndizo siasa zetu ?


Mbali na hilo, viongozi wa Chama wanajitosa kutumia dhana ya ajabu, ikiwemo
madai ya &#8216;nguvu za giza' kitu kinachoshangaza, baadhi yao ni wasomi waliobobea na wana historia ya kutumikia dini, lakini si chochote, wanatumia siasa za ajabu tena zenye utashi wa kudhuru watu.


Hii si mara ya kwanza, kwani kwa mwenendo huo huo haujapita muda mrefu huko mjini Arusha, kwamba mwenendo wa Chadema na falsafa yao ya &#8216;nguvu ya umma' walisababisha vifo vya watu kadhaa.


Katika harakati hizo, yalitokea mapambano baina ya Polisi na wana-Chadema waliohamasishwa na viongozi wa juu Chama pamoja na mbunge wao wakitumia &#8216;nguvu ya umma' dhidi ya nguvu halali ya Polisi ikitimza wajibu wa kulinda raia na sheria za nchi.


Ni tukio lililoishia kwa msiba na viongozi wa Chadema kuingia katika lawama za kuwaingiza katika matendo yao kuwashawishi wafuasi wao na hata wakapoteza maisha.


Huko Mwanza, simulizi ni ghasia hizo zinazosababishwa na wafuasi wa Chadema zimeishia katika kujenga hali tete jijini humo na hata jina la chama hicho kuwa baya kwa wakazi wote jijini.


Falsafa ya &#8216;nguvu za umma' mara zote hutekelezwa kwa matukio ya ghasia na uvunjaji wa sheria za nchi pasipo sababu za msingi. Ni vigumu kutenganisha propaganda za Chadema na matendo ya ghasia.

Pengine kwa kurejea matukio ya kurupukushani za kisiasa katika kampeni ndogo ya uchaguzi wilayani Tunduru, ilishuhudiwa chama hicho kilivyotumia muda mwingi kutunishiana misuli na fujo za kisiasa katika mitaa ya Tunduru dhidi ya Chama cha CUF.


Ngome hiyo ya upinzani ambazo zilitakiwa kuungana mkono dhidi ya CCM, lakini cha ajabu walitunishiana misuli hata kufikia hatua kwamba mara nusuru wafuasi hao wapigane, jambo lililolainisha kampeni za CCM kwa wananchi kujua pumba na mchele.


Kuna wakati bila Kamanda wa Polisi wa Mkoa bila ya kuingilia kati kuwatawanya wafuasi hao wawe katika pande mbili tofauti, basi kungetokea ghasia nzito ambazo haijulikani nini hasa ingekuwa hatima yake.


Hivi karibuni wilayani Tarime, ghasia za Chadema uanaharakati wa haki za wazwa katika migodi nazo ziliishia katika kusababisha vifo hivi karibuni na baadhi ya Wabunge wa chama hicho sasa wanakabiliwa na mikono ya sheria.


Sura kama hiyo ya ghasia, ndio ilijitokeza katika mazishi ya aliyekuwa mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe, ambapo mazingira ya shari yalitawala wakiamini kifo hicho kina mkono wa viongozi wa juu wa chama.


Kwa ujumla, Chadema muda mwingi imekuwa ikijitapa kwamba wanapambana wakidai haki na demokrasia. Kwa bahati mbaya wadau hao wa demokrasia ndio wamekuwa wavunjaji wakubwa wa demokrasia na haki za binadamu.


Iwapo matendo yao nio hayo, Chadema wanasaka nini katika viti vya uchaguzi, kwa wao kuna na matendo yaliyofanana na matakwa ya demokrasia kitaifa na kimataifa.

Sifa kubwa ya chama cha siasa ni &#8216;kukubalika'. Kwa hayo yanayojitokeza na kudhulumu haki za binadamu ndio kukubalika?
 
Hv hili gazeti la Udaku bado lipo? Mi nafikiri wahariri wake wanatumia miguu katika kufikiri jamani tuwasamehe bure tu.
 
Regardless of the source ya hii habari..inabidi tukubaliane kuwa..chadema wamekuwa chanzo cha vurugu na vifo vingi vya watu wasio na hatia
 
Mod, mmeunganisha thread nyingi mpaka zinaboa kusoma, maana zimejichanganya, hakuna hata mtiririko mzuri.
 
Regardless of the source ya hii habari..inabidi tukubaliane kuwa..chadema wamekuwa chanzo cha vurugu na vifo vingi vya watu wasio na hatia

Vipi biashara yako ya majeneza na sanda inakwendaje i?
 
Hilo gazeti bado linauzwa katika maofisi ya serikali tu. tena wao wanaomba wawasaidie kulinunua ili wapate fedha za kujiendesha.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom