Uchaguzi KKKT: Askofu Malasusa achaguliwa kuwa Askofu Mkuu wa KKKT kuchukua nafasi ya Dkt. Fredrick Shoo

Uchaguzi KKKT: Askofu Malasusa achaguliwa kuwa Askofu Mkuu wa KKKT kuchukua nafasi ya Dkt. Fredrick Shoo

Malasusa amepata kura 167 ambazo ni asilimia 64 ya kura zote zilizopigwa

Askofu malasusa alikuwa anagombea dhidi ya askofu Abednego Keshomshahara wa Dayosisi ya Bukoba aliyepata kura 73 na Askofu Dr George Fihavango wa Dayosisi ya Njombe aliyeshindwa katika duru ya kwanza.

Hii itaakuwa ni mara ya pili kwa Askofu malasusa kuwa mkuu wa kanisa la Kiinjili la Kiliteri Tanzania (KKKT) tangu alipochaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2007, hadi mwaka 2015 ambapo alimuachia kijiti askofu Fredrick shoo ambaye ameongoza kwa kipindi cha miaka nane.

Hongera Askofu Malasusa, Hongera KKKT.
---

Mkutano Mkuu wa 21 wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) umemchagua Askofu Alex Malasusa kuwa mkuu mteule wa KKKT.

Askofu Malasusa wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani anachukua nafasi ya Askofu Fredrick Shoo aliyemaliza muda wake wa uongozo wa awamu mbili.

Anarejea tena kwenye nafasi hiyo aliyoihudumu kuanzia 2007-2015 alipomaliza na nafasi yake ikiongozwa na Askofu Shoo.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo mwenyekiti wa uchaguzi huo,Askofu Amon Mwenda,amesema kura zilizopigwa zilikuwa 241 ambapo kati ya hizo Malasusa amepata kura 167 sawa na asilimia 69.3 huku Askofu Abednego Kesho Mshahara akipata kura 73 sawa na asilimia 30.3

Askofu Malasusa alizaliwa Aprili 18, 1961; katika kijiji cha Kiwira Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya.

Ni mtoto wa pili katika familia ya watoto nane ya Marehemu Mchungaji Gehaz Japhet Malasusa na Subilaga Timoth Malasusa.

Askofu Malasusa amewahi kuwa Mkuu wa Kanisa kwa miaka 8 tangu 2007 hadi 2016 na Mkuu wa Chuo Kikuu Tumaini Makumira kwa kipindi chote.

Mstari wa Biblia anaoupenda ni Yohana 3:30 ‘’Basi hii furaha yangu imetimia. Yeye hana budi kuzidi, bali mimi kupungua.’’
Hi hbr siyo nzuri Sana kwa mchungaji eliona kimaro siyo nzuri kabsa
 
Malasusa? Hakuna kitu pale, yule ni mwanasiasa tu kama wanasiasa wengine ni sawa na bagonza tu tofauti yao ya wazi ni ukada wa vyama mwingine chadema mwingine ccm, but all in all wale ni kitu kimoja katika utumishi wao katika kutekeleza majukumu ya kazi zao
poor analysis. Bagonza anapingana na udhalimu, wizi, dhambi ya wanasiasa. Huyu mwingine anaunga mkno dhuluma za ccm... vitu viwili tofauti kabisa.
na wewe hutaki udhulumiwe, Am I right?
 
poor analysis. Bagonza anapingana na udhalimu, wizi, dhambi ya wanasiasa. Huyu mwingine anaunga mkno dhuluma za ccm... vitu viwili tofauti kabisa.
na wewe hutaki udhulumiwe, Am I right?
still hao wote ni maaskofu wa KKKT
 
poor analysis. Bagonza anapingana na udhalimu, wizi, dhambi ya wanasiasa. Huyu mwingine anaunga mkno dhuluma za ccm... vitu viwili tofauti kabisa.
na wewe hutaki udhulumiwe, Am I right?
Yako ndo very poor analysis maana at the end comparison yao ni kuwa wote ni wanasiasa wenye mlengo tofauti unaoshahibiana na baadhi ya vyama vya kisiasa.
 
Malasusa hana jipya na hatakuwa na jipya zaidi ya kuendeleza abrakadabra za kisiasa ndani ya KKKT. Bora wangemchagua Keshomshahara ambaye hajulikani sana mrengo wake wa kisiasa kama ni mhafidhina au mliberali
Huyo keshomshahara nae ni puppet wa Bagonza na ndo maana hashindi, since 2015 anagombea na hashindi. It's time aseme imetosha.
 
Kanisa hili la KKKT huko juu kuanzia level za uchungaji wa kanisa kubwa, mpaka uaskofu mkuu ni mwendo wa kupiga pesa tu.
Mungu nisamehe
Ndio maana Rushwa na uchawi vinatawala.. Hawako ktk kutafuta Roho zilizopotea... Wapo kupiga hela na kulinda mapato yasio halali ili vizazi navyo vifaidi dhambi zao😭😭
 
Unaweza kuta rushwa zinatumika kwenye kuchagua wa Askofu. Hapo ndio naonaga bora nipige bia tu.
 
Huko kote sijasoma, nimesoma jina tu keshomshahara ni mhaya aisee
 
Back
Top Bottom