UmkhontoweSizwe
Platinum Member
- Dec 19, 2008
- 9,454
- 8,894
Kwa hili nakubaliana na huu unabii. Na hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kujiunga kwenye chadema hii ya sasa ili agombee urais!4. Kwa mujibu wa unabii huu, CHADEMA hawana mtu ambaye ana kibali cha Mungu - Yehova kugombea kiti cha u - Rais mwaka 2025 aliye ndani ya chama chao..
ChaiNB:
Naomba moderators tafadhali ruhusuni mada hii ijadiliwe. Msiogope, haina madhara yoyote kwenu na JF kwa sbb hii ni kitu halisi na mtu aliyetoa unabii huu yupo na anaweza kuulizwa na kuthibitisha haya
la Mungu (Biblia...)
3. Je, wewe unasemaje? Toa maoni yako...
Nimesikiliza na kusikiza kwa makini. Sijaisikia neno Wagalatia Wala habari za msichana wa miaka 17.Msikilize Nabii feki, utapata majibu yote ya maswali yako.
Kama huna GB za kutosha, siwezi kukusaidia, kwani ukitaka kuifaidi hii mada ni lazima usikilize video hiyo. Vinginevyo utakuwa umekurupuka tu.
Nimecheka kijinga sana system ipo kazini ,chadema haitafanya makosaKama anagombea agombee lakini msimshirikishe Mungu kwenye mambo yenu ya kitapeli. Nwajiboy muongo muongo, asiyekuwa na msimamo, opportunist ni afadhali Samia mara 10,000.
Ngwaji Boy ni msanii sana ila Tanzania sijui kwanini watu huwa wanawaamini wasanii sana.
Imani yangu ya Kikristo imekuwa diluted na manabii wa uongo na tabiri fake kila mtu nabii mazafanta
Hili nalo linawezekana..Kwa jicho jingine... Je Kama ni watu wa CCM wasiomtaka mama, wanamtisha ili asigombee, ili wao wachukue hio nafasi Wala sio Gwajima, kwamba hapa wanatumia jina la Gwaji Kama skape goat ya timu flani ndani ya chama?
Huu ushuzi unatoka huko huko CCM na utawavuruga kwelikweli mpaka kusudi la Mungu litimie.CHADEMA NA MAUJINGA YAO!.......
Ushuzi huu.
Nakukumbusha tu,Hili nalo linawezekana..
Na kusema kweli, kwa haraka haraka hata mimi nimeiona hii picha, kwamba, a smart political game is being played here..
Na hawa jamaa wanaocheza mchezo huu kwa jinsi walivyo wajinga wakidhani watu hawataajua, wanaonesha kuwa hawamtaki huyu mwanamke wao huko CCM lakini at the same time ndani ya CHADEMA wanajua kwa hakika kuwa mtu hatari na sumu kwa CCM wakati wowote ni Tundu Antipasy Mughway Lissu.
Kwa hiyo wanacheza mchezo wao kotekote kuhakikisha, huyu mama hatoboi huko CCM na wakati huohuo kujaribu kupanda mgogoro CHADEMA ili mradi mwiba wa CCM, mwanasheria, mwanaharakati na mwanasiasa nguli na machachari Tundu Lissu hapati nafasi kupambana na yeyote atakayesimama CCM mwaka kesho - 2025..
Na ukiachilia mbali hiki kinachoitwa "unabii", the fact is that, huyu mama majority ya wana CCM huko ndani mwao ukiachilia mbali sisi wananchi tusio wanaCCM hawamkubali..
Vigezo vikuu vya kutokukubalika ni vitatu hivi;
1. Si Mtanganyika, ni Mzanzibari (nchi na taifa jingine akitawala nchi nyingine ya Tanganyika)
2. Ni mwanamke. Taifa hili ni gumu, mwanamke hawezi kuliongoza. Huyu mwanamke amethibitisha hili. Na by the way this is nature. A woman can never be a head of the family unless it is by default..
3. Hatukumchagua. She is just there by constitutional default. in 2020 she was just a side chick wa John P. Magufuli. Mtu ambaye hakuchaguliwa hawezi kuwa na vision ktk uongozi wake. Siku zote uongozi wake utakuwa vogue.
Mimi namwita Lucas Mwashambwa aje huku aseme neno. Yuko kimya sana kwenye hili. Au umepigwa na kitu kizito kichwani boss na umezirai huko uliko??
Ndoto za mchana hizo kakojoe kwanza usije ukashusha "kimba"
Tujadliane wote..Kama una kumbukumbu za kutosha utakumbuka kuhusu unabii wa nabii TB Joshua alipotangaza hadharani kuhusu Edward Lowassa kwamba huyo ndiye rais wa 5 Tanzania, na Mungu ndiye aliyemfunulia hayo.
Hivi umewahi kujiuliza kwa nini Edward Lowassa hakutimiza huo unabii? Mie naamini kuwa nabii TB Joshua alifunuliwa na mungu yule yule aliyemfunulia huyo nabii wa Arusha. Kinachonipa shida ni hiki.. Mungu alimuondoa duniani nabii TB Joshua, baadae akamuondoa na Edward Lowassa.
Mpaka leo Sijajua mwenye shida ni nani kati ya hawa watatu..
1. Mungu aliyemfunulia TB Joshua
2. TB Joshua aliyefunuliwa na huyo Mungu.
3. Edward Lowassa aliyetabiriwa kuwa ndiye rais wa awamu ya tano Tanzania.
Kumbuka TB Joshua na Edward Lowassa sasa.
Hebu nitatulie hiyo shida Ila nipate kuamini pia kuhusu Gwaji boy ndiye rais aliyetabiriwa
Watu wajinga kama wewe huangalia mazuri machache aliyofanya mtu pasipo kujali pale aliishia, vitabu vya Mungu vinasema bora mwisho mwema kuliko mwanzo mwema..Magufuli alianza vyema badae aliharibu na matokeo yake alipata alichostahili..hata kama alifanya mazuri kiasi gani hapo mwanzo, mwisho ndio unasema kwa sauti kubwa kuliko mwanzo wake, hayo mazuri aliyofanya ni sawa na bure, Mungu alituma watu kumwambia..acha hii mambo, akakaza shingo na kiburi cha madaraka, ndio ikaishia hapo, binadamu ana uamuzi kusikia anachoambiwa bila kujali nani anasema, maskini au tajiri, mkubwa au mdogo, muislamu au mkristo au mpagani...SIKILIZA! ukikaza shingo itabaki historia!Chadema ni chama kikuu cha upinzani hili halina ubishi. Tatizo la chadema kwa sasa imepoteza viongozi wenye mvuto japo hawataki kukubali. Wao wamejikita na chuki dhidi ya JPM wanadhani hichi kitawasaidia kumbe ndio kinawauwa kabisa. JPM bado anaishi kwenye mioyo ya watu wengi pamoja na makosa yake ya kibinadamu bado anakumbukwa sana kwa kazi na hulka yake na yeyote atakaye mzungumzia vizuri ananafasi kubwa ya kupenya kisiasa, hivyo basi ili imani ya watanzania kwa chadema irudi inahitaji watu watayeweza kutembelea nyota ya JPM hata kama viongozi wa juu hawataki nao hao watu wengi wao wapo nje ya chadema. Huu ni ushauri wangu.
Ikiwa unaanza na herufi kubwa baada ya nukta hapo ndipo nilipogundua hakuna unachoelewa.Watu wajinga kama wewe huangalia mazuri machache aliyofanya mtu pasipo kujali pale aliishia, vitabu vya Mungu vinasema bora mwisho mwema kuliko mwanzo mwema..Magufuli alianza vyema badae aliharibu na matokeo yake alipata alichostahili..hata kama alifanya mazuri kiasi gani hapo mwanzo, mwisho ndio unasema kwa sauti kubwa kuliko mwanzo wake, hayo mazuri aliyofanya ni sawa na bure, Mungu alituma watu kumwambia..acha hii mambo, akakaza shingo na kiburi cha madaraka, ndio ikaishia hapo, binadamu ana uamuzi kusikia anachoambiwa bila kujali nani anasema, maskini au tajiri, mkubwa au mdogo, muislamu au mkristo au mpagani...SIKILIZA! ukikaza shingo itabaki historia!
Lissu anafaa sana kuwa waziri wa Sheria na Katiba.Mpeni Lisu kiti 2025 tunatoboa wallah, wapinzani wengi wana sifa chafu ila si huyu Mwana.
Marais wote ni chaguo la MunguNi ujinga kiasi gani hata wakimpokea? Tambua Gwajima ni CCM then aende kugombea kule sio rahisi ,ishu ya Lowasa bado inawagawa wao kwa wao mpaka leo.
Kama kweli ni Mpango wa Mungu ,yule shekhe yahya yupo correct 💯 kwa sababu alitabiri mpaka kifo cha Magufuli mda mrefu sana ....Uhalisia ni kwamba Mama samia ni chaguo la Mungu.
Marais wengi dunian ni wana-sheriaLissu anafaa sana kuwa waziri wa Sheria na Katiba.
Na siku zote Mungu hujibu maombi ya watu wake ktk njia tofauti kabisa na tunavyodhani sisi kama asemavyo katika Neno lake;Ondoa wazo la kurogwa..
Mungu akiamua iwe hivyo, basi itakuwa hivyo. Hakuna wa kupinga..
Na siku zote Mungu hujibu maombi ya watu wake ktk njia tofauti kabisa na tunavyodhani sisi kama asemavyo katika Neno lake;
Isaya 55:8-9 SUV
".....Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.."
Kwa Mungu yote yanawrzekana. Hata yule usiyemdhani na hujawahi kumweka katika akili na mawazo yako, anaweza kufanywa Rais wa nchi hii..!