Uchaguzi Nigeria: Naona safari hii wameamua kuongonzwa na vibabu vilivyokula chumvi nyingi

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2020
Posts
7,799
Reaction score
14,215
Habari zenu wana JF wenzangu, ama baada ya salam ningependa sasa nijielekeze kwenye mada husika.

Kwa wasiofahamu, ni kwamba Nigeria inakwenda kufanya uchaguzi wake mkuu wa uraisi miezi mitatu ijayo.

Katika uchaguzi huo mkuu, mchuano mkali utakuwa kati ya vikongwe wawili wa nchi hiyo mh Bola Ahmed Tinubu mwenye umri wa miaka 70, huyu atapeperusha bendera ya chama tawala cha APC.

Na mgombea mungine anaitwa mh Atiku Abubakar mwenye miaka 75, ambae atapeperusha bendera ya chama cha upinzani cha PDP.

Ukiangalia umri na muonekano wao wote wanaonekana ni wazee, lkn ndo hivyo mfumo umeona hao ndio wanaofaa zaidi kuongoza taifa hilo linaloongoza kuwa na watu wengi Afrika, na pia ndio nchi inayoongoza kuwa na wasomi wengi vijana.
Sasa vijana sijui tunakwama wapi hadi kutokupewa nafasi kubwa kubwa kugombea.

Hata Marekani waliona wazee ndio wanaofaa safari hii kuwaongoza baada ya bwana mdogo Obama kumaliza muda wake.

Picha ya juu ni mzee Bola Ahmed Tinubu, na ya chini ni mzee Atiku Abubakar.

 
Kama wananchi wamewaamini hakuna tatizo kabisa.Ni sawa tu na tanzania awamu ya sita inaongozwa na vijana wengi lakini kwa mambo ya hovyo yanayofanywa utatamani bora tungeongozwa na wazee wa kuanzia miaka 90.
 
Mbona wataalam wa mambo wanasema peter obi wa LP he’s likely to take it?
Ni ngumu kuvhukua kwasababu ni Igbo. Hatapata kura kutoka kwa Yoruba ambao ni wengi na kaskazin Waislamu ambao wote kwa pamoja hawawapendi Igbo.

Kumbuka Igbo wenyewe sasa hivi wanajitambulisha Biafra siyo wa Nigeria. Wanataka kujitenga.

Ahmed Tinubu ni myoruba na mwislamu ambaye si mdini ana support ya pia ya wakristo na Waislamu wa kaskazin.

Atiku Abubakar ni Hausa mwislamu hana support kubwa ya wakristo pia Waislamu wamegawanyika.

Tinubu atashinda.
 
Safari hii Rais hatakuwa Mkristu toka kusini maana ndiyo umekuwa utamaduni wao
 
Safari hii Rais hatakuwa Mkristu toka kusini maana ndiyo umekuwa utamaduni wao
Ila wakristo wengi wanampenda Tinubu. Yani ni kama muislamu jina. Uzuri wa Waislamu wa kusini waoruba Uislamu ni jina wengi wao wanafuata dini za asili na ndugu zao wengi wakristo. Abiola alijuwa muislamu Yorubo hata tapeli Hushpupy ni muislamu Yoruba. Olesegun Obasanjo mkristo Yoruba.
 
Thanks for enlightening me,siasa za naija sizijui kabisa.πŸ™πŸΏ
 
Kama wananchi wamewaamini hakuna tatizo kabisa.Ni sawa tu na tanzania awamu ya sita inaongozwa na vijana wengi lakini kwa mambo ya hovyo yanayofanywa utatamani bora tungeongozwa na wazee wa kuanzia miaka 90.
Naona nchi nyingi zitaanza kurudisha pasi kwa wazee ambao ndio wafungaji wazuri wa ahadi zao.

Vijana madoido mengi lkn vitendo ni zero. Ofisini wanawaza girlfriend zao na mipango yao tu basi.
 
Uchambuzi wako ni mzuri na bora kabisa hapa jukwaani.

Wape salam wazee wa Copenhage, nasikia ndipo yalipo makazi ya mzee wa ubwabwa Gen Hashim Rungwe πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Safari hii Rais hatakuwa Mkristu toka kusini maana ndiyo umekuwa utamaduni wao
Ila hapo mchuano mkuu ni wa hao wawili ambao nafikiri ni waislam. Japo inawezekana jina likawa sio kigezo husika cha dini ya mtu.
 
Mkuu kumbe kwa namna fulan uko vizuri. Nilitegemea wew ni mjuzi wa yale mambo yetu ya uvunguni tu peke yake πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…