mchambuzi umekosea mwanza.... mwanza ni blue kabisa... ni kati ya ngome kubwa ya chadema na kura nyingi zilitoka mwanza za chadema.. hapo panahitajika kurekebishwa..
ni vyema ukianzisha mjadala kama poll ila utawekaje hiyo poll?wazo zuri; sasa tunafanyeje, nianzishe mjadala mpya as a poll?
Sawa sawa, ngoja niziweke sawa then nitazipandisha;You're welcome mkuu.
Kuhusu takwimu ambazo wanachadema wanazikataa,je ni zile zenye kuonyesha idadi ya waliovipigia kura vyama?Kama zilichakachuliwa,je kuna ambazo huwa wanazitumia?
Mkuu nadhani unaweza tu kuziweka hapa halafu kama kuna watakaoweza kuongezea kutokana na wanavyoona,ama kama wanazo takwimu za tofauti basi wataziweka.Cha muhimu ni kuona ni wananchi kiasi gani waliowapigia kura chama flani kwenye hizo ngome zao.Hata kama zimechakachuliwa,bado tutakuwa na uwezo wa kuona ni wananchi wangapi kati ya waliojiandikisha kupiga kura na wakafanya hivyo wakati wa uchaguzi.
Tunafanyeje hapo mkuu, maana kuna Mkoa wa Katavi na pia wa njombe; lakini kwa takwimu za sasa, geita ipo kwenye takwimu za Mwanza, kama ilivyokuwa katavi rukwa na njombe iringa;
Kuna saa naona kama vichwa venu haviko sawa.Hivi kweli Chadema mnawaza Kushika nchi hii.Hizo ni ndoto za alinacha
kwa sasa mikoa mingine imeanzishwa mipya. hukuijumuisha. hata hivyo na hiyo kama dsm kusema ni ngomehakika ya CDM, kwa takwimu za mwaka gani? ukiangalia kati ya chadema ina jimbo la kawe & ubungo (2) . CCM inamajimbo (6) ya kinondoni, ilala,ukonga,segerea,kigamboni,temeke nk. hivyo kusema dsm ni ngome ya uhakika Chadema, kwa kutumia tafiti zipi ?
the same to maeneo mengine ya mikoa mingine. uchambuzi huu hauko realistic.
Nilidhania Mwanza Blue ila sikuwa na uhakika sana niiweke wapi; Lakini nadhani upo sahihi; ngoja tuone wadau wengine wanasemaje, ila ningependa ufafanue kidogo kwanini unadhani mwanza ni blue, nafanya hivyo ili kuepuka wajinga wa CCM wakija humu waanze kutaja tu fulani kijani kwa hoja za ovyo; Kuhusu Kigoma, pia nakubaliana na wewe, lakini kati ya nyekundu na blue for NCCR, imelalia zaidi wapi kwa mtazamo wako?
Vigezo gani mnatumia kupanga mikoa? Hili ndio jambo la kwanza. Maana naona mnachangia tu bila kujua vigezo. Inawezekanaje Kigoma ikawa kijani na Kilimanjaro blue? Kigoma ilitoa Kura Kwa chadema kwenye Urais 45% Mara mbili ya national avarage. Arusha? Kilimanjaro? Dar ES Salaam?Mwanza ni buluu kutokana na yaliyomkumba Tony na Lau licha ya mamlaka yao ya kidola n.k.
Kigoma imelalia bluu zaidi kama tunajumuisha bluu ya NCCR na upinzani katika ujumla wake
Mkuu nakubaliana na wewe'unafikiri nini kifanyike ili tuweze kuharibu huo mpango mpya wa ccm?
.....
Vigezo gani mnatumia kupanga mikoa? Hili ndio jambo la kwanza. Maana naona mnachangia tu bila kujua vigezo. Inawezekanaje Kigoma ikawa kijani na Kilimanjaro blue? Kigoma ilitoa Kura Kwa chadema kwenye Urais 45% Mara mbili ya national avarage. Arusha? Kilimanjaro? Dar ES Salaam?
Kigoma ina majimbo 8, majimbo 5 yapo upinzani na 3 CCM. Hawa NCCR wote isipokuwa mmoja Ni CDM rebels tu na watu wa Kigoma walichagua watu hao Kwa hasira na sio NCCR iliyochaguliwa na ndio maana CDM ilipata Kura nyingi za Urais na madiwani wengi sana mkoa Mzima.
Wekeni vigezo vya kisayansi na sio hisia tu. companero wewe mwanasayansi, saidia kuweka vigezo ili mjadala uwe na maana.
Kigoma has never been CCM toka mfumo wa vyama vingi uanze and it will never been CCM. Unawezaje kuweka Iringa blue na Kigoma au Kagera kijani?.......