Uchaguzi S/Mitaa 2019: Wagombea wa Upinzani asilimia kubwa wameenguliwa kugombea, CCM wengi wapitishwa

Uchaguzi S/Mitaa 2019: Wagombea wa Upinzani asilimia kubwa wameenguliwa kugombea, CCM wengi wapitishwa

[emoji30][emoji30][emoji30]
Screenshot_20191016-224559-picsay.jpeg
 
Mgombea akikosea kujaza kwani hakuna anayehakiki?

Kwani ni mtihani huo kwamba mtu akikosea ndio ishatoka hiyo?

Hii sababu ya fomu kukosewa kujazwa ni sababu moja ya kipuuzi sana kwenye nchi inayofuata mfumo wa "demokrasia"
Uko sahihi mkuu, yaani mtu apite bila kupingwa kisa kaandika Sheli badala ya Shely?
 
Wanajitekenya wenyewe wanakenua wenyewe. Watanzania sio mazuzu kama wanavyotaka tuonekane
 
Kwa tuliofanya kazi na wanakijiji hii siishangai ni kawaida kabisa kukosea kuandika. Sasa kwakua hii ni vita ya kisiasa ukiona mtu kakosea kuandika unamuacha hivo hivo na ukilaza wake ili akaenguliwe mbele huko. Pia hawa vilaza ukiwasaidia kurekebisha walipokosea baadae huwa wasumbufu sana maana kuandika hawajui ila mdomoni wanaongea sana kama wake wenza.
CCM woooote hawajakosea ila upinzani tuuuu???jiulize kidogo mkuu fikirisha ubongo hapo ndo kwenye hoja
 
Hapa dawa ni kuingia kitaa tu basi.
Ila kuja hapa JF sijui Twitter hakuna msaada wowote.
Makonda ataendelea kujazia hips zake hadi 2025
 
Katiba Mpya ni muhimu ili kumaliza huu upuuzi unaoendelea.
 
Hiyo hapo chini ni form ya mgombea wa CHADEMA lakini baada ya kukata imekutwa imeongezwa kwenye mwaka 1979, wao wameongeza '0' na kwenye jina la Hamimu ,wameongeza 'u'. Huku wengine wameombiwa form zao zimekata kwa sababu awana namba ya anuwani .ila mchezo mlioucheza auchezeki

Watendaji wa kata kumbukeni amtoweza kuinyamazisha sauti yenye machozi ata siku moja iyo amri mliyopewa atoweza kuzaa matunda

View attachment 1255416
Nadhani huyu alikuwa na kopi take ni vizuri akakate rufaa
 
Wasalaam,

Ukifatilia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utagundua makosa yote katika fomu za wagombea yamelenga wagombea wa upinzani tu. Mbona hakuna mgombea hata mmoja wa CCM aliekatwa? Ina maana wagombea wa CCM ni malaika na hawana walilokosea?

Ukitafakari kwa kina utagundua hawa watendaji wa kata walipokea maelekezo maalum kutoka juu wawapitishe bila kupingwa wagombea wa CCM na kuwakata wale wa upinzani, kwa muktadha huu sioni sababu kwa nini vyama vya upinzani vishiriki uchaguzi huu wa kibedui wakati hata wakishinda hawatatangazwa.

Mwisho, ni vema vyama vya upinzani wasisikilize propaganda za Waziri Jaffo kwamba wakate rufaa badala yake kwa umoja wao wakae pembeni na wasishiriki uchaguzi huo wawaachie CCM na umafia wao wajikite kudai 'Tume Huru ya Uchaguzi', na kama watashiriki wasilalamike wameporwa ushindi - tutawachoka na kuwaona mamluki wa CCM.

Ova.
 
Yule muuza bar kama wewe ndio mnajiita upinzani,bado sana

State agent
Halafu kiazi kama ww ndio unacopy post za my son drink water kisha unajifanya unaweza kumjua user! Hizo siasa za kihanithi ndio zitaua chama kama cdm?
 
Kosa ni la nani kwani?
Kwa nini wapinzani wache kupambana?
 
kufeli sio kufeli shule,
Kufeli ni kufeli maisha.
Kushinda si kuwa na wafuasi wengi,
Kushinda ni kuwa na Mbinu nyingi.
ccm ni watu si malaika,
Sisi ni watu kama wao,tumeshindwaje?
Kimenukaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Mgombea akikosea kujaza kwani hakuna anayehakiki?

Kwani ni mtihani huo kwamba mtu akikosea ndio ishatoka hiyo?

Hii sababu ya fomu kukosewa kujazwa ni sababu moja ya kipuuzi sana kwenye nchi inayofuata mfumo wa "demokrasia"
Mtu anajaza asione kakosea mwaka au jina lake?[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Yaani ukiangalia unaona tofauti ya aina ya peni na uandishi. Hata mtoto wa primary haezi fanya ujinga kama huo kwenye ripoti akifeli.
 
Inaonekana waadilifu ndani ya nchi yetu wamebaki wachache sana. Hofu ya Mungu haipo kabisa. Niombe tu wenye msituhofu binadamu wenzenu wr have nothing to do for you but fear the Heaven God.
 
Kimsingi wagombea wa CCM,wana akili sanaaa, hawawezi kukosea kujaza forms.
ukitaka ucheke upasuke,chukua mgombea wa ccm hapa upinzani pale wape kitabu wasome ama wape imla (drs la 3b iyo ) alafu toa matokeo 90% ya ccm ni ujinga mtupu huku 90% ya upinzani watafanya vzr

ila leo ccm wote wamegeuka ma prof. hatar sana hii
 
Kwa tuliofanya kazi na wanakijiji hii siishangai ni kawaida kabisa kukosea kuandika. Sasa kwakua hii ni vita ya kisiasa ukiona mtu kakosea kuandika unamuacha hivo hivo na ukilaza wake ili akaenguliwe mbele huko. Pia hawa vilaza ukiwasaidia kurekebisha walipokosea baadae huwa wasumbufu sana maana kuandika hawajui ila mdomoni wanaongea sana kama wake wenza.
Hakuna makosa hapo, wamechukua peni wakaongeza herufi na namba hizo.. we huoni kama ni mchezo huo unachezwa.
 
Watendaji wa serikali na CCM wamewaachia kila kata mpinzani mmoja agombee na kuwakata wasigombee katika mitaa mingine ni la kimkakati zaidi.

Yaani wamepanga mtaa huo mmoja utakafanya uchaguzi waushambulie kwa wapiga kura hewa toka mitaa mbalimbali wakisindikizwa na polisi washinde kiurahisi. Hiyo ndio mbinu ilioundwa magogoni wakati wa kikao kile
 
Back
Top Bottom