Uchaguzi S/Mitaa 2019: Wagombea wa Upinzani asilimia kubwa wameenguliwa kugombea, CCM wengi wapitishwa

Uchaguzi S/Mitaa 2019: Wagombea wa Upinzani asilimia kubwa wameenguliwa kugombea, CCM wengi wapitishwa

Katika majina ya wagombea wote waliokosa vigezo vya kugombea uenyekiti SM wametoka upinzani, je upande ule wao wote wako timilifu yaani hakuna hata mmoja wao aliyekosea japo kidogo iwe kujaza fomu au kukosa vigezo?
 
Serikali hii inatuchukulia sisi raia ni maboya kweli, yani kuna uongo wanaongea "BILA KUPEPESA MACHO" hata kwenye kichwa cha mwendawazimu hauaminiki.

Huyu Dr. Abbas ameongea leo kama mtoto wa chekechea. Ni aibu kubwa katika sekta ya elimu ya "PhD HOLDERS" kua na kiumbe kilaza kama huyu.
 
Wakati mwingine ujanja ujanja hufanyika kwa mahesabu, lakini safari hii in hatari! Hebu fikiria karibu nchi nzima kosa la upinzani linafanana, kujaza form vibaya! Ukienda Kagera, Kigoma, Mwanza, Arusha, Kilimanjaro! Hii inakuwaje kama siyo maagizo yakutoka juu ya namna ya kudeal na form za wapinzani! Unapokula Na kipofu angalia usimguse mkonp
 
Hao ndio walioruhusiwa na watendaji kuchukua, baada ya hao wawili kuchukua waliokusudiwa na watendaji kwa mjibu ya maelekezo waliopewa na CCM, milango ilitiwa lock na watendaji walitimua mbio kama vifaru vya Iddi amini vilivyokoswakoswa na makombora ya Nyerere.
 
k
Kwenye kata yangu kwa siku 7 zote wagombea wa CHADEMA walifanya kila waliwezalo kupewa fomu za kugombea na ikashindikana!! Hakuna anayelalamika bali watu wanaelezea hali halisi ilivyokuwa!!
kata gani?
 
Wakati mwingine ujanja ujanja hufanyika kwa mahesabu, lakini safari hii in hatari! Hebu fikiria karibu nchi nzima kosa la upinzani linafanana, kujaza form vibaya! Ukienda Kagera, Kigoma, Mwanza, Arusha, Kilimanjaro! Hii inakuwaje kama siyo maagizo yakutoka juu ya namna ya kudeal na form za wapinzani! Unapokula Na kipofu angalia usimguse mkonp
Labda Mwenyekiti wa Chadema aliagiza wakosee who knows?
 
Hao ndio walioruhusiwa na watendaji kuchukua, baada ya hao wawili kuchukua waliokusudiwa na watendaji kwa mjibu ya maelekezo waliopewa na CCM, milango ilitiwa lock na watendaji walitimua mbio kama vifaru vya Iddi amini vilivyokoswakoswa na makombora ya Nyerere.
umewasiliana na mwenyekiti wa chadema longido?
 
Labda Mwenyekiti wa Chadema aliagiza wakosee who knows?
Kwa nini unadhani ni maagizo ya Mwenyekiti na siyo katibu ambaye ndiye mtendaji? Hata nikikutajia ni kata gani hutaelewa. Barua yangu iko mezani kwa Jafo na haijafanyiwa kazi. Ilikuwa ni maelekezo!!
 
Mkuu chama chetu pendwa ccm kimevamiwa na watu wenye roho mabaya sana za kikatili.
 
Mke wangu Nilimwambia mapema kabisa kabla hawajaapishwa asishiriki hii dhuluma ya kuonea na kutotenda haki. Bahati nzuri alitoa sababu ya hudhuru na akatolewa.

Kwangu sitaki dhuluma na wala sikulele kwa dhuluma; eti pesa nikamwambia ukifanya kazi ya uandikishaji basi elewa umekeuka amri yangu. Aniletee mabalaa kwangu.
 
umewasiliana na mwenyekiti wa chadema longido?

Ushenzi wote kwa muongozo wa jiwe unaeleweka wala hauhitaji kuwasiliana na mtu yoyote. Wala usipoteze muda wako kutaka kujikosha. Hata wananchi wajinga kwenye hiki kinachoendelea wamejua jiwe ni mshenzi fulani.
 
Kumbe Ni JingaLao!!. Basi Acha Tu Niendelee Na Mambo Mengine.
 
Ndungu zangu watanzania tangu Magufuli aingia madarakani ccm imekuwa ikipoteza ushawishi siku hadi siku. Na mpaka sasa ccm haina hata mkoa mmoja ambao inaushawishi wa kiongozi. Yaani hapa nataka kwanza tuelewe tafauti ya kuongoza na kutawala.

Kuogoza ni ile hali ya kushawishi watu kwa govu ya hoja na kuwafanya mshirikiane kwa pamoja kufanikisha mambo yenu. Kutawala ni hali ya kuzibiti kitu au watu kwa kutumia nguvu na kuwafanya watu wafanye unavyo taka wewe kwafaida yako, bila kujari kama wanataka au la.

Serikari au mtu unapo fikia kutawala badala ya kuongoza huwa mwisho wako sio mzuri hata kama unafanya mazuri kiasi gani. Mifano ya watu na serikali zilizo tawala badala ya kuongoza ni kama serikali ya Libya chini ya Gaddafi, Iraqi China ya Sadam, Zimbabwe chini ya Mugabe, na sasa chini mwanagagwa.

Kwa Africa na Asia mifano ni mingi sana ya serikali za kiutawala na miisho yake ya kusikitisha. Ila jaajabu wafirika ni wagumu sana kujifuza kupitia makosa ya wezao. Yaani ni jambo la kawaida kwenye jamii nyingi za kiafirika kukuta watu warudia makosa mwaka hadi mwaka bila hata kushituka.

Kwa mfano tuchukulie ajari za barabarani hasa za bodaboda vijana wengi wamepoteza maisha kwa kuto fuwata tahadhari za vyombo hivo lakini bado unakuta vijana wengi wanaendesha badoboda bila hata kuvaa helmets au wanavaa kwa kuhofia police tu.

Mfano mwingine ni utawala mbovu ambao huperekea maafa makubwa kama yale ya Rwanda na Burundi lakini bado nchi hizo jirani zake bado zinafanya makosa ya watangulizi wao. sasa ngoja ni rudi kuzungumuzia CCM inakopeleka nchi na iliko fikia.

Kwa sasa CCM imefika wakati wa kutawala kwa asilimia mia chini ya Magufuli, marais wengine kabla ya Magufuli walikuwa wanatawala asilimia hamusini,hamsini nyingine wanaongoza. sasa Serikali yoyote inapo fikia aslimia mia kutawala mwisho wake sio mzuri na huwa hauko mbali.

Kwanini nasema hivi ni kwamba ukisha anza kutawala badala ya kuongoza ni kwamba unakuwa umeziba masikio. Husikii tena kelele za unao watawala na unao watawala nao wanaamuwa kuziba mdomo, watawala wanabaki wanabaki kuongea wenyewe kwa wenyewe.

Na watawaliwa wanatafuta namna nyingine ya kuongea wenyewe kwa wenyewe bila kutowa sauti. nchi inakuwa na makundi mawili ya watawala na watawaliwa.

Watawala wanalindwa na majeshi na mitutu na watawaliwa wanabaki wakinamisha vichwa vyao huko wakitafuta sauti ya kuwaamurisha kupambana na watawala. Hapo ndio ccm ilipo fikisha taifa ndani ya miaka minne ya Magufuli.
 
Back
Top Bottom