Uchaguzi S/Mitaa 2019: Wagombea wa Upinzani asilimia kubwa wameenguliwa kugombea, CCM wengi wapitishwa

Uchaguzi S/Mitaa 2019: Wagombea wa Upinzani asilimia kubwa wameenguliwa kugombea, CCM wengi wapitishwa

@kulumaliyawananch, Serikali yenye vyama Vingi ni serikali legelege na inakuwa haina maamuzi magumu. Piga kazi mzee Baba.
 
Mtoa mada hujielewi, wangechukuaje wakati watendaji walifunga ofisi muda wote,? Rais angekuwa kweli Ni mtetezi Wa wanyonge watendaji wote walipaswa kufukuzwa kazi.
 
Hawa jamaa zangu hawakujiandaa vyema kwani nikichukulia mfano wa wilaya ya longido ni wagombea wawili tu ambao walichukua fomu kupitia chadema kugombea .
Tukisema hawakujipanga mtachukia?
POYOYO
 
Hawa jamaa zangu hawakujiandaa vyema kwani nikichukulia mfano wa wilaya ya longido ni wagombea wawili tu ambao walichukua fomu kupitia chadema kugombea .
Tukisema hawakujipanga mtachukia?
Wewe mjinga umejifungia huko lumumba na basha wako utajuaje ya mtaani??
 
Hawa jamaa zangu hawakujiandaa vyema kwani nikichukulia mfano wa wilaya ya longido ni wagombea wawili tu ambao walichukua fomu kupitia chadema kugombea .
Tukisema hawakujipanga mtachukia?
Mtahadaa sana watu ila maelekezo waliyopewa na mashinikizo yote wametueleza hao watendaji.. Na wengine walijutia sana hizo nafasi japo hawakuwa na jinsi.. Mfano walipotoka ikulu walitueleza kila kilichosemwa na miongozo waliyopewa na vikao vilivyofanyika baadae wakiwa na kamati za siasa za wilaya na kata, na nadhibitisha hili kwa Kigoma wilaya ya Kasulu, utaniluta mtaa wa Muilamvia..
 
1.Huna shughuli ya kueleweka
2.Haujulikani unakaa wapi
3.Sehemu ya makazi unayoishi haijasomeka vizuri
4.Chama chako hakijasajiliwa
5.Muhuri wa Chama chako haueleweki
6Uraia wako tunamashaka nao
7.Umejaza fomu vibaya
8 Ati zenu zinafanana
9 Kwenye R umeweka L
10 Hii picha ya lini?
11.Ni mlevi
12. Unakesi polisi
13. Ofisi imefungwa kwa wiki nzima

Naomba uniongezee sababu nyingine zilizotajwa kuwaengua wagombea Kwenye uchaguzi huu wa Serikali za mitaa.
FB_IMG_1573098533293.jpg
 
Ccm tumezoea ushindi wa goli la mkono. Mambo ya kushindana sio utamaduni wetu
 
P
Mshauri wake mkuu Daud Bashite hana vyeti na yeye mwenyewe PhD yake ni ya utata na kibaya zaidi washauri wa Naibu Rais Daud Bashite ni akina cyprian Musiba , Le mutuz na Joseph yona, ebu cheki huu mtiririko ndipo utabaini kuwa ipo shida kubwa kwenye mfumo wa utawala awamu hii ya tano
Pumbavu
 
WALE WANAOLALAMIKA WAMEONEWA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA WAMEZINGATIA HAYA?
1 . Kama majina yake yatatofautiana kati ya majina aliyojaza kwenye fomu na majina aliyojiandikisha kwenye daftari. Angalia kanuni ya 13 (e) Uk. 152

2. Endapo mdhamini hataandika majina matatu na cheo ktk vyama. Angalia mwongozo wa uchaguzi kipengele cha 14.2 (d) Uk. 10-11

3. Jina alilojaza wakati anachukua fomu lifanane na lililopo kwenye fomu ( dispatch book vs forms). Angalia kanuni ya 17 (1) Uk. 153

4. Mgombea arejeshe fomu mwenyewe na kusaini. Angalia kanuni ya 17 (2) Uk. 153

5. Majina ya mdhaminiwa yafanane na ya mgombea yaliyojazwa kwenye fomu. Angalia mwongozo wa uchaguzi kipengele cha 14.2 (a-d) Uk. 10-11

6. Fomu ya kiapo iwe halisi iliyotolewa na msimamizi msaidizi na ishuhudiwe na msimamizi msaidizi ngaz husuka. Angalia kanuni ya 16 (e) Uk. 152

7. Fomu zijazwe na mhusika lazima ziwe zimesainiwa. Angalia mwongozo wa uchaguzi kipengele cha 14.2 (e&f) Uk. 10-11

8. Fomu zishuhudiwe na ngazi ya chini ya chama itakayobainishwa na chama. Angalia mwongozo wa uchaguzi kipengele cha 14.1 & 14.2 (a) Uk. 10-11

9. Ambaye hajajiandikisha hana sifa ya kuwa mgombea. Angalia kanuni ya 13 (e)Uk. 152, ilinganishe na Kanuni ya 16 (d) Uk. 152 na Kanuni ya 14 (a) Uk. 152

10. Aliyejiandikisha mara mbili atakuwa amepoteza sifa ya kugombea au kupiga kura. Angalia kanuni ya 14 (b)Uk. 152
11. Lazima aeleze shughuli halali inayomwingizia kipato na endapo atabainika kudanganya atakuwa amepoteza sifa. Angalia kanuni ya 15 (d)Uk. 152
12. Atakayeomba nafasi zaidi ya moja kwenye fomu moja atakuwa amepoteza sifa. Angalia kanuni ya 17 (1) & (5) Uk. 152-153
13. Nafasi anayoomba ionekane mpaka kwenye fomu ya kiapo. Angalia kanuni ya 17 (1)Uk. 153 isome sambamba na Kanuni ya 16 (e) Uk. 153
14. Fomu zijazwe kwa ukamilifu. Angalia kanuni ya 17 (2) Uk. 153
15. Eneo la uraia ajaze uraia siyo nchi mfano: Mtanzania na siyo Tanzania. Angalia kanuni ya 17 (1-5) Uk. 153-154
16. Usahihi wa maeneo kwa mujibu wa GN mfano chankobe akiandika chakobe atakuwa amepoteza sifa maana eneo hilo litakuwa halipo ktk GN. Angalia kanuni ya 15 (e) Uk. 152 & Kanuni ya 17 (1-5) Uk. 153-154.

17. Mwombaji aeleze anaomba nafasi ipi na wapi mfano nafasi anayoomba mwenyekiti wa Kijiji cha Kagera vinginevyo atakuwa amepoteza sifa. Angalia kanuni ya 15 (e) Uk. 152

18. Fomu ijazwe taarifa inayohitajika tu, kuwepo kwa maandishi au michoro isiyohitajika hilo ni kosa. Angalia kanuni ya 17 (5) Uk. 154

19. Mgombea arejeshe fomu zote mbili kinyume na hapo hana sifa. Angalia kanuni ya 17 (2), (3) na (4) Uk. 153-154

20. Kama mgombea ameomba nafasi mbili unaweza kumteua nafasi moja. Angalia kanuni ya 17 (1)& (5) Uk. 153-154

21. Mgombea akiwa na ajira, wadhifa au uteuzi wowote katika mihimili ya Serikali atakuwa amepoteza sifa za kuchaguliwa. Anagalia kanuni ya 16 (f)Uk. 153

22. Ikiwa Mgombea alichukua fomu na hakurejesha atakuwa amepoteza sifa za kuchaguliwa. Angalia Kanuni ya 17 (2), (3) na (4)

23. Mgombea ambaye hatadhaminiwa na ngazi ya chini ya Chama chakeatakuwa amepoteza sifa za kuchaguliwa. Angalia mwongozo wa uchaguzi sehemu 14.1 na 14.2 (a)

Kabla ya kulalamika kukatwa majina,Jiridhisheni kwa kila hatua kama mmekidhi vigezo na masharti sio kulalama...
 
Mtahadaa sana watu ila maelekezo waliyopewa na mashinikizo yote wametueleza hao watendaji.. Na wengine walijutia sana hizo nafasi japo hawakuwa na jinsi.. Mfano walipotoka ikulu walitueleza kila kilichosemwa na miongozo waliyopewa na vikao vilivyofanyika baadae wakiwa na kamati za siasa za wilaya na kata, na nadhibitisha hili kwa Kigoma wilaya ya Kasulu, utaniluta mtaa wa Muilamvia..
Maajabu katika pita pita zangu kule Mabibo Maziwa- kuna ofisi ya Chama Na. 8, majira jioni vijana walikuwa kwenye mazoezi kama yale ya mchakachaka, wakiimba kwa hamasa wakati wanafanya vile kama wanajiandaa kwenda kwenye paredi za matamasha! Natumaini sio matayarisho ya kupambana na vyama vya upinzani hio tarehe ya uchaguzi!
 
Back
Top Bottom