rodrick alexander
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 16,784
- 23,312
Siipendi CCM lakini kwa maslahi ya taifa nitawapa kura ya urais
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pole, PM zilinigomea, sijajua tatizo.Mzee,ujumbe wangu PM huioni.?
Daaah sa nakupataje.?Pole, PM zilinigomea, sijajua tatizo.
P
Lete ushahidi wa sentensi ambayo ni uwongo
Angekuwa amefanya mambo makubwa angepiga magoti Njombe?Rais Magufuli tangu aingie Madarakani amekuwa akifanya baadhi ya Mambo ambayo yanakuwa reflected Kama ya kwake.
thanks leo imefunguka, nimekujibuDaaah sa nakupataje.?
Hekaya za Abunuas wapelekee watoto wanaokaribia kujiunga chekechea, nao sijui kama watafika mwisho wa simulizi kabla hawajauchapa usingizi mzito.Watu gani wanajaa, unajua hii Nchi Ina watu wangapi!? Unajua wapiga kura wako wangapi! Nenda kaangalie mikutano ya Dr.Slaa kipindi hicho halafu ndio utajua. Kura hazipatikani kwa kufanya mikutano na kujaza watu, kura zinapatikana kwa mikakati kabambe, CCM wanatafuta kura kuanzia ngazi ya Nyumba kumi hadi na Taifa. Wakati nyie Lissu anadhurura peke yake, WanaCCM wako busy inchi nzima kila mtaa, kila Kijiji, kila kata, kila tarafa, kila Willya na kila Mkoa na hapa ndipo siku zote Mnapigwa. Mkutano unajaza Bodaboda ambao hata hawakujiandikisha na wale waliojiandikisha tareh. 28 watakuwa busy wakila vichwa kuvipeleka na kuvitoa kwenye maeneo ya kupigia kura. Bodaboda gani atapaki Bodaboda yake akatumie three hrs eti kumchagua Lissu eti kisa wakati wa Kampeni alimjazia wese.
Poti unamsikia huyu......ha haaaaa...mtoa ujumbe noma.Acha uK wewe nyau pasco.
Na hiyo ndio aina ya demokrasia ccm mko nayo bure kabisa! NktSasa si mvichukue na nyingi Kama mna uwezo huo!
Matusi hayasaidii kijana kuwa na heshimaAcha uK wewe nyau pasco.
Mbona waongea kama mgeni/mpya. Hivi hizo TV umeanza kuangalia karibuni. Pole sanaKwani Kuna mtu amewazuia Msichaguliwe. Wanazengo wenyewe ndio wanaamua, na hadi sasa wanaona Chama kiendelee kushika hatamu.
Jana nilikuwa naangalia kipindi kimoja UTV AZAM TV cha Uchaguzi, jamaa alikuwa Jimbo la Ubungo, moja ya swali alilikuwa akiwauliza wanazengo Kama wanawajua wagombea ubunge was Jimbo Hilo, huwezi amini, 40% walikuwa hawajui wagombea, Sasa Hawa ndio CCM wanasanya kura zao na kuwaelekeza sehemu ya kuweka tiki na wakienda kwenye kituo hawarembi, 50% walisema wanamjua mgombea mmoja tu, Kitila Mkumbo na baadhi wakasema hawajawahi kwenda kwenye Kampeni ila wamemuona kwenye Matangazo.
Sasa nyie mnajitekenya humu mnacheka wenyewe eti mtashinda, wakati wanazengo hata hawana tym na nyie!
Kwann kuna mbinu rukuki za wizi, hujuma nkBora sema wewe, tukisema sisi, tutanyooshewa vidole vya Makada!.
P
Mawazo kama haya alikutana nayo Nyerere na Mandela wakat wa kudai uhuruYaani chadema Kama chama kikuu Cha upinzani kimepoteza muelekeo,huwezi kuwaaminisha watu eti utashinda urais na wakati wagombea ubunge na madiwani hawana muelekeo, utashinda vp Kama cibangi hizo? Hata Kama ukishinda bado Hawa wenye wabunge wengi watawapelekesha tuuu kiufupi vyama vya upinzani mnatimiza wajibuu Hapo.
Siyo kazi ya CCM kuleta time huru ya Uchaguzi. So long wanaendelea kutawala, kwao huu ndio mfumo sahihi!CCM wangekuwa wanajiamini wangeleta tume huru, wasingeChakachua wenyeviti Wa mitaa Na vitongoji mwaka Jana, wasingewawelea pingamizi yasiyokuwa na mantiki, ukitaka tuonekane kama wewe Ni great thinker, uone ukweli huu.
Jama wana wasiwasi sana. Pamoja Nakufungia wapinzani midomo miaka 5, pamoja Na kuzuia vyombo vya habari visitangaze habari za upinzani, pamoja Na picha za wagombea Wa upinzani kutotundikwa, pamoja Na mikutano ya CCM kusomba watu kwa maroli, bado CDM inawaogopa wapinzani. Ni kwa nini? Jiulize
Umesahau kuongeza chagua Kichaa😂😂 Eti kuanza keaho tutembee kwa makundi yeye anadhani wote vichaa kama yeye😂😂 Mwanasheria asiyejua kuna sheria ya inayozuzuia mikusanyiko isiyo halali.
Kuna mambo ya Msingi zaidi ya kuangalia Binge liveHatutaki Rais dikteta ,sauti za wananchi kuzizima, bunge letu kuwa kibogoyo, Radio zote kutangaza habari za ccm,magazeti yote kutangaza habari za ccm,watu kupigwa risasi ovyo na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa ,kulagai wakulima kuwa nitanunua mazao lakini ndio kwanza mazao yamekufa, korosho hola, alizeti hola, mpunga hola, kahawa hola biashara nyingi zimefungwa sasa serikali ya namna hii ni ya nini huyu ni Idd Amini wa Tanzania hafai hata kwa kulumagia
Big up, this is the truthKuna watu humu wanajipa moyo eti CHADEMA hii ya Lissu, Mbowe, Mnyika, Heche, Halima, Bulaya Matiko na Wenzake wanaweza kuishinda CCM ya Magufuli, Bashiru Ali, Mangula, na mfumo mzima wa Chama Cha Mapinduzi.
Kama Kuna mtu anawaza hivo na anamanisha na ana amini Mawazo yake hayo yanaweza kuwa uhalisia, basi huyo ana tatizo kubwa sana kifikira.
Uchaguzi huu CDM iliyopalaganyika ikiwa inamtegemea mtu mmoja inakwenda kupambana na:
1. Rais Magufuli
2.Chama Cha Mapinduzi.
3.Watanzania
1.Rais Magufuli
Rais Magufuli tangu aingie Madarakani amekuwa akifanya baadhi ya Mambo ambayo yanakuwa reflected Kama ya kwake.Hali hii imemfanya pengine awe maarufu kuliko hata Chama chake. Magufuli amejijengea ufalme wake ndani ya mioyo ya Watanzania, siyo lazima akubalike na wote na hakuna anayetegemea iwe hivo, lakini ukweli umaarufu wake unamfanya yeye Kama yeye apate kura ambazo atapigiwa yeye Kama Magufuli, na nyingi ni zile za wasio na Chama.
Hizi kelele za mitandaoni dhidi ya JPM ukizifatilia ni za wale wale, hata thread humu ukiangalia wale wale ndio wanakoment, lakini waulize je Mama zao, Dada zao, wajomba zao, shangazi zao, Babu zao na Bibi zao wanaijua Facebook, wanaijua JF, wanaijua tweeter au Instagram. Jibu wanalo, je hoja ya Uhuru na maendeleo ya vitu inaeleweka kwa Hawa watu. Mtu ambaye hakuwahi kuona umeme( sizungumzii Maria Sarungi Wala Fatuma Katume, na Hawa hawafiki hata 5000) leo kauona umeme unaweza kumueleza asimchague Magufuli eti kwakuwa amemnyima Uhuru wakati anaenda kanisani, anapiga simu, anaenda sokoni anaenda shambani Bila wasiwasi akakuelewa?.
2. Chama Cha Mapinduzi
Dubwasha linalotisha, Dude hatari Barani Africa, dude ambalo Lina historia ya kuwaweka viongozi kadhaa wa Afrika Madarakani. Hili dude Lina vichwa, Lina Consultants, lina rasilimali watu na fedha za kutosha, Lina uzoefu wa kutosha katika anga hii ya siasa. Halafu Kuna mtu anawaza linaweza kushindwa na mtu anaitwa Tundu Lissu.
Hebu angalia muundo was CCM kuanzia hapo kwenye mtaa unaoishi, angalia kwa sasa kwenye eneo lako la nyumbani kumi muundo wa CCM, angalia WanaCCM hao katika muundo huo katika eneo Hilo la nyumba kumi walivyojipanga na wanavyoendelea kuzisanya kura kwa ajiri ya CCM. Sasa unaona, Kuna kura za Magufuli ambazo atazipata yeye na kura ambazo Chama Cha Mapinduzi kitazipata. Hali hii iliwahi kutokea mwaka 2005 ambapo Jakaya Mrisho Kikwete yeye Kama yeye alipigiwa kura na CCM nayo ikapata kura zilivyounganishwa mkwere akapiga 80%. Lakini 2010 watu wakawa hawana hamu naye, lakini Chama Cha Mapinduzi kikamtafutia kura. Akapiga 61% Kama sikosei, hizi zilikuwa za Chama.
Najua wengi mmejaa kwenye Social Media, hamupo field, hamuoni huo muundo ulivyo hatari. CDM is no where, katika level hizi, CDM ipo mgongoni kwa Lissu. Upande mwingine Kuna CCM Kuna Magufuli na Kuna CCM.
Sasa ukiangalia hali ilivo Sasa unaona kabisa atapigiwa parefu, lakini bahati mbaya hata upande wa Wabunge Mambo ni magumu mno. Majimbo ambayo siku za nyuma yalikuwa ni hoja isiyobishaniwa Sasa mwaka huu ni hoja nzito, Pale Mbeya Sugu amekamatwa Ke....nde, na Dr. Tulia, Lema ameshikwa Pu....bu, na Gambo, hapo Arusha, Mbowe jasho linatirtika hadi kwenye meno, Mzee wa Kondoo wa bwana anapumulia Kisogo Cha Halima. CDM ni Kama wapo kwenye furushi ambalo tarehe 28 linadondoka.
3. Watanzania
Sisi tunayo Kariba ambayo tumejengewa na Mzee Baba mwenyewe, Mchonga, Baba wa Taifa, Julius Kambarage Nyerere. Ni Kariba ambayo unaweza iita utakavyo kulinga a na muono wako, Njema sana, Mbaya, woga, au uungwana.
Watanzania tunapenda Amani Bila kujali gharama yake, Watanzania ni wavumilivu bila kujali gharama, Watanzania tunapenda uungwana sana, hatupendi Shari, lakini mbaya zaidi tunayo Imani Kali kuwa Mabeberu ni watu hatari, na watu wabaya sana. Lakini sisi ni wanafiki, Watanzania ukiwa na sisi tutakueleza hivi, ukitoka tunafanya tofauti, Tunakutanguliza halafu tunasikilizia, upepo ukibadilika tunaingia mitini!
Watanzania ukishaonyesha dalili za ushari, dalili za kuleta uvunjifu wa Amani au ukajinasibisha na Mababeru, au ukasingiziwa Mambo hayo, basi sisi Watanzania tunachofanya, tunakukwepa.
Tarehe 28 Watanzania bila kujali gharama, bila kujari Lissu anaahidi nini Watamkwepa, watajiepusha naye.
Msisahau hapa sijazungumzia swala la CCM kuwa Chama Dora!!
Nimevaa ngao🤣🤣🤣
Kumbuka: Oktoba 28 kujitokeza kwa wingi kupiga kura. CHADEMA tunaomba umchague;
Rais-Tundu Lissu,
Chagua wagombea Ubunge na Udiwani wa CHADEMA.View attachment 1610830