Uchaguzi Ukraine ni mwakani, Zelensky atawaambia nini wapiga kura wake?

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Uchaguzi mwengine mkuu wa Ukraine unatarajiwa kufanyika mwakani 2024.

Kipi kinatarajiwa kufanyika kwenye uchaguzi huo. Je, utasitishwa kutokana na vita vinavyoendelea.Na jee katika inaruhusu udhuru huo.

Na kama uchaguzi utafanyika raisi wa sasa, Zelenksy naye atagombea. Na kama akigombea atanadi sera gani kwa wapiga kura wake?.
 
Sijui kama itatosha kuwaambia wapiga kura kuwa kesho itakuwa siku ya furaha sana.
Wakulima wa ngano sijui watasemaje.Na wamiliki wa viwanda vya madawa na chuma nao sijui kama watamuelewa.
Kwa nini wao raia hawaono
 
Atawaambia amewaletea zawadi ya vita.
 
Shitholes mnakera sana! Mambele huko is quietly different!
 
Sijui kama itatosha kuwaambia wapiga kura kuwa kesho itakuwa siku ya furaha sana.
Wakulima wa ngano sijui watasemaje.Na wamiliki wa viwanda vya madawa na chuma nao sijui kama watamuelewa.
Hahitaji kuwaambia chochote, wanapaswa kumshukuru kwa kuzuia mashamba na viwanda vyao kutekwa na Urusi.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Kwa changamoto anayopitia, hiyo ndio sehemu pekee ya kung'atuka bila lawama, ashiriki kwenye uchaguzi ila ajiwekee mazingira ya kushindwa; baada yahapo akapumzike ugenini.
Ata ningekuwa mimi, ningeitisha uchaguzi kama kawaida, na ningejiwekea mazingira ya kushindwa ili nipumzike.
Kuruhusu watu waingie kwenye vita na kufa si kazi rahisi; nchi inaweza ikakunyonga kwa maamuzi mabaya.​
 
Unafanya transition ya uongozi huku mabomu yanarindima? Wewe unaona nani atataka kukalia kiti ktk mazingira kama hayo?
 
Hakuna nchi inakuwa na vita dhidi ya taifa lingine vinaendelea alafu ikafanya uchaguzi
 
Ikitokea wanachi wakitaka uchaguzi?
Mfano inawezaje kutokea wananchi wa Tanzania wakataka uchaguzi mwaka 2023 au 2024 au ule wa mwaka 2025 wasiutake?

Uchaguzi sio suala la ombi ni suala la kikatiba. Katiba ya Ukraine hairuhusu uchaguzi mkiwa vitani, na sijawahi sikia nchi inayoruhusu uchaguzi mkuu ikiwa vitani. Rais akifariki au akajiuzulu bado hawafanyi uchaguzi mkuu
 
Back
Top Bottom