Uchaguzi wa Spika huenda usifanyike, kesi ya Mbatia juu ya ukiukwaji wa Katiba katika kupatikana Spika mpya inaanza kusikilizwa

Uchaguzi wa Spika huenda usifanyike, kesi ya Mbatia juu ya ukiukwaji wa Katiba katika kupatikana Spika mpya inaanza kusikilizwa

Katiba inasema vyote viwili sura 148(1) inasema barua iandikwe na isaniniwe kwa mkono wa mhusika. Baadaye kipengele (c) inasema hiyo taarifa (iliyo katika barua) ipelekwe bungeni!! Ndugai hakufanya hivyo!!
Wakati katibu wa Bunge amethibitisha kuipokea barua? Au ilikuwa lazima aambatane na kila mmoja wetu kama uthibitisho wa kufanya hivyo?
 
Nchi hii kila kitu kinawezekana hususan kama mhimili uliojichimbia chin zaid ukiwa na maslah
Ndivyo watakavyojibu. Japo kwa mujibu wa Katiba ya JMT, mhimili wa mahakama, ndio the custodian wa Katiba. Bunge lilitunga sheria
batili ya kipengele cha mgombea uongozi kudhaminiwa na chama cha siasa, Mtikila akafungua kesi Mahakama Kuu kupinga kipengele hicho, akashinda, Mahakama Kuu ikatoa uamuzi kipengele hicho ni batili kwasababu kinakwenda kinyume cha katiba. Serikali ikakata rufaa, ikashindwa.

Ili kumkomoa Mtikila na kuidharau mahakama, Serikali ikapeleka bungeni sheria ya mabadiliko ya katiba kwa hati ya dharura na kukichomeka kipengele hicho batili ndani ya katiba, ili kuhalalisha sasa kiko kikatiba. Mtikila akapinga tena na akashinda tena kwa mahakama kutamka mabadiliko hayo ya katiba ni mabadiliko batili.

Serikali ikakata rufaa na mahakama ya rufaa Tanzania ikafikia uamuzi wa ajabu kuwahi kutokea Tanzania, ikatamka Mahakama haina uwezo wa kuliingilia Bunge na
kupinga kipengele chochote Bunge lilichokiingiza kwenye ndani ya katiba!.
P
 
Mkuu Consultant, nchi inaendeshwa kwa mujibu wa Katiba, sheria, taratibu na kanuni. Kilichofanyika katika uteuzi wa Dr. Tulia Akson ni utaratibu tuu ndani ya CCM. Baada ya utaratibu wa CCM kufuatwa, kila chama kitaleta mgombea wake aliyepatikana kwa mujibu wa taratibu za vyama na kumleta Bungeni ambapo sasa kanuni za Bunge kumchagua Spika lazima zifuatwe na Spika kuchaguliwa na hivyo Spika kuapa mbele ya Bunge na kuwa amepatikana kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni.
Japo baada ya uteuzi wa CCM, huyo ndiye Spika, kinachofanyika ni maigizo tuu ya kukamilisha tuu taratibu za uchaguzi wa Spika wa Bunge kwa mujibu wa sheria na kanuni.
P
Pascal Mayalla unatukosea sana sisi wafuasi kindakindani wa Sisiemu. Inakuaje ^maigizo^ wakati tumefuata taratibu zote kama chama? Maigizo, by definition, ni kitu ama jambo lisilo halisi. See?
 
Hakika muhimili mmoja umejichimbia chini zaidi, Magufuli was very right, open and straightforward person.
Bunge ni mhimili, kufuatia kutokuwepo checks and balance, mahakamani yetu sio tuu haita entertain hiyo kesi, bali haita thubutu hata to summon the legistlature with a court summons, hata Bunge livunje vipi katiba!.
Hivyo mchakato wa kukamilisha tuu taratibu za kumthibitisha Spika Tulia utaendelea as if nothing happened.

Rejea
P,
 
Pascal Mayalla unatukusea sana sisi wafuasi kindakindani wa Sisiemu. Inakuaje ^maigizo^ wakati tumefuata taratibu zote kama chama? Maigizo, by definition, ni kitu ama jambo lisilo halisi. See?
Mkuu Jasmoni Tegga , ninawakoseaje CCM wakati mimi mwenyewe ni kada wa CCM?. Kosa langu ni kuwa ukweli daima, mimi ni CCM Nyerere type, kinataka viongozi wachaguliwe kwa ushindani wa haki based on merits na sio mgombea kubebwa kwa karata ya gender!. Tulitaka spika bora na sio bora Spika, Dr. Tulia Akson ni Bora Spika, but she has a chance to be Spika Bora na hili nimelisema hapa Je, Wajua, Naibu Spika, Chini ya "Bora Spika", Anaweza Kuwa "Spika Bora?". Dr. Tulia, "Ukitulia, Una Fursa ya Kuwa Spika Bora Sana!" Hongera Sana!
P
 
Ndungai ataambiwa aandike barua nyingine kimyakimya alitaarifu bunge, arudishe nyuma tarehe ya barua. Nawaza kwa sauti
 
Wadau na wanabodi, nchi kama nchi yaweza kuwa katika katiba tuna vipengere vizuri sana vinavyosimama kulipeleka mbele taifa ila sasa jinsi vinavyosimamiwa na wasimamizi wa sheria ndiyo tatizo lipo hapo.

Kiufupi sisi kama taifa kufuata katiba na kuionea haibu ni bado sana, kama mahakama yenyewe inagwaya mbele ya serikali unategema mahakama hiyo hiyo itoe tamko gani lenye haibu kwa katiba?.

Issue ya JN ndo imepita hivyo na huyo Mbatia anaenda kuweka kumbukumbu tu za kimahakama kuwa huko nyuma iliwahi tokea hivi but kwa kesi hii majibu yapo wazi.

Tuendelee kujadili mambo ya taifa letu but deep issues hatuwezi kupata mabadiriko yoyote as tunachoweza kuona toka kwa majirani zetu ex, Kenya.
 
Mkuu Consultant, nchi inaendeshwa kwa mujibu wa Katiba, sheria, taratibu na kanuni. Kilichofanyika katika uteuzi wa Dr. Tulia Akson ni utaratibu tuu ndani ya CCM. Baada ya utaratibu wa CCM kufuatwa, kila chama kitaleta mgombea wake aliyepatikana kwa mujibu wa taratibu za vyama na kumleta Bungeni ambapo sasa kanuni za Bunge kumchagua Spika lazima zifuatwe na Spika kuchaguliwa na hivyo Spika kuapa mbele ya Bunge na kuwa amepatikana kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni.
Japo baada ya uteuzi wa CCM, huyo ndiye Spika, kinachofanyika ni maigizo tuu ya kukamilisha tuu taratibu za uchaguzi wa Spika wa Bunge kwa mujibu wa sheria na kanuni.
P

Mayalla, paragraph yako ya mwisho ndiyo pekee uliyohitaji kuandika hapa. Zingine zote hazina tija yoyote katika context ya mchakato halisi unaotumiwa kumpata Speaker!
 
Mkuu Consultant, nchi inaendeshwa kwa mujibu wa Katiba, sheria, taratibu na kanuni. Kilichofanyika katika uteuzi wa Dr. Tulia Akson ni utaratibu tuu ndani ya CCM.
Basi utaratibu wa CCM ni wa kibabe sana. Wabunge wa CCM bado watapaswa kufanya igizo la kupiga kura kuchagua kati ya Tulia na kivuli cha Tulia? Madness!

Mama sasa ateue tu naibu speaker na kumsimika. Nadhani Zanzibar hawajawahi kutupa naibu speaker. Hii iwe zamu yao.
 
Soma muktadha/context vizuri. Anaposema TAARIFA HIYO YA KUJIUDHURU ana-refer taarifa iliyoandikwa na kuwekwa sahihi kwa mkono wa spika!! Lazima hi hk kifungu cha 149 (1) c kisomwe chote kwa pamoja ili kupata muktadha vizuri!!
Kama nisingesoma chote, basi ningeandika tu kifungu kidogo "c" kinasemaje lakini nimeanzia palipoandikwa "Mtu yeyote mwenye dhamana ya kazi yoyote iliyoanzishwa na Katiba hii.....ndipo nikaja ku-drop kifungu c: iwapo mtu huyo ni Spika au Naibu wa Spika wa Bunge, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu ataiwasilisha kwenye Bunge;,

That's one but two, wakati mwingine kusoma katiba peke yake inakuwa haitoshi bila kupata sheria zilizotungwa na bunge (kama zipo) kuhusiana na ibara husika!

Kwa muktadha huu, mtu inabidi apate Sheria ya 1980 #1 Ibara ya16; na marekebisho yake ya 1984, #15 Ibara ya 52 na Sheria ya 1992, #4 Ibara ya 37.

Binafsi nimehangaika sana kutafuta hizi sheria lakini nimezikosa!!!

Kwa bahati mbaya sana, watu huwa tuna-conclude kupitia Ibara za Katiba peke yake lakini huwa haiendi hivyo!! Karibu kila ibara ya katiba huwa inatungiwa sheria na bunge, kwahiyo complete package ya Ibara husika inapatikana kwa kusoma Ibara mbalimbali za Katiba, na katika mazingira mengine, unatakiwa kwenda kwenye sheria!!
 
Kama ikithibitika hakufuata sheria zakujiuzuru huoni atakayechsguliwa automatic atakuwa batili?
Uchaguzi wa Spika utafanyika kwa sababu kesi aliyopeleka mahakamani Mh. Mbatia , ni ya kumtaka Spika aliyepita ajiuzulu kkwa utaratibu. Mh, Mbatia si kwamba anahitaji Spika aliyepita arudi madarakani, hapana bali anamtaka ajiuzulu kwa kufuata utaratibu kama ambavyo Mh. Mbatia anavyodhani kuwa ni sahihi. Sasa hapa kuna hoja gani ya kuzuia uchaguzi usifanyike?

Mh. Mbatia hajapeleka mahakamani shauri la kuzuia uchaguzi wa Spika usifanyike na hivyo uchaguzi utafanyika kama ilivyopangwa.
 
Kama ikithibitika hakufuata sheria zakujiuzuru huoni atakayechsguliwa automatic atakuwa batili?
Assuming angekuwa ameamua kuacha kazi na asiandike barua ya kuacha kazi, Spika asingechaguliwa? Kama kweli angekuwa hakujiuzulu kwa kufauata utaratibu, basi ingeweza hata kuchukuliwa kuwa amefukuzwa kazi halafu mambo mengine yanaendelea. Kutokufuatwa utaratibu na aliyejiuzulu, kwa namna yoyote ile haku-compromise nafasi ya mwingine anayetakiwa kuchukua nafasi yake.
Mwenye nia na kesi hii anatakiwa akazuie mchakato wa kuchaguliwa spika mpya, na si kuhangaika na yule aliyejiuzulu
 
Hivi mgombea mteule wa kiti cha spika si ni nguli wa sheria mwenye phd ya sheria, hakuiona kasoro hiyo mpaka akajitosa kuwania nafasi hiyo? Kama kweli kuna kosa lilifanyika kwa mujibu wa katiba bila shaka kuna pa kutokea. Siamini kama wote waliojitosa kuwania kiti hicho akiwemo "mtemi" walifungwa macho hawakuiona kasoro hiyo. Ngoja tusubiri mahakama itasema nini.
 
Back
Top Bottom