Elections 2010 Uchaguzi wa Spika wa bunge la 10 la Tanzania

Elections 2010 Uchaguzi wa Spika wa bunge la 10 la Tanzania

Hii ni Aibu kama wapinzani wengine kura zao zimeenda kwa huyu mama ndo watajua ujeuri na ukorofi wake wakati wa kuchangia hoja :nono:
 
Kama ilivyokuwa kwenye uchaguzi wa RAIS, ni wazi kwamba Dk SLAA angekuwa rais bora zaidi kuliko huyu aliyechaguliwa na NEC, JAKAYA KIKWETE, ndivyo ilivyotokea kwenye uchaguzi wa Spika. MABERE MARANDO angekuwa Spika bora zaidi kuliko huyu mwanamama ANNE MAKINDA aliyechaguliwa na MAFISADI. Inabidi sasa wananchi tuwe makini zaidi katika kuchagua wawakilishi wetu bungeni. Hii sasa inaonyesha picha halisi ya jinsi Bunge hili litakavyokuwa -- ni kutetea ufisadi tu.
 
''juock ping'' namwaminia

tendaaa muujiza..... baba tendaaaa muujuzaaaaa

usituache mwaka huu upite bila marando kuwa spika... tendaaa muujiza
Nawe humjui Marando, mpaka unahitaji miujiza kwa Marando, na iishie huko.
 
Yaani i don't belive kama CUF wamempigia kura Anna makinda??? duuu

Jamani tusianze kuhukumu. Kura zilikuwa za siri kwa hiyo nani kamchagua nani siyo la msingi kwa sasa maana hatuna uhakika. Tugange yajayo. Life goes on.
 
I think Sitta ndio katoa hio kura moja nje ya CHADEMA. Yani CUF wameonyesha rangi zao. :nono:
 
and i am afraid kama 2015 akisimamishwa mwanamke kugomnea urais kwa tiketi ya CCM atashinda. Wanawake huwa wanapepa sijui hisia ya huruma, CCM wajanja hamjui? kivyovyote kama angesimama mwanaume uspika angepata Marando.
habari ndo hiyo jamani. Go back to work na kujipanga. there is no chama cha upinzani apart from CHADEMA.
 
CCM kumchagua Marando ni miujiza ya ajabu manake watakuwa wameruhusu uwazi ambao haujawahi kutokea na walivyochafuka duh watajutia,hivyo kulinda maovu yao CCM watakimbilia kwa Makinda si kwa qualifications but kukingiiana kifua tulikokuzoea.
 
Inaonyesha wazi kuwa wapinzani bado wana beef wao kwa wao, na hii ni dalili mbaya sana kwa wapinzani. Chadema wapo kama 45 inamaanisha 45+8 ndo 53. Vyama vya upinzani vimesalitiana kiuwaziwazi!
 
The person you can easily change is yourself, CUF ni chama kingine na si lazima mitazamo yao iendane na nyie. Kwa ubinafsi walioonyesha Chadema wa kuchagua kiongozi wa upinzani bungeni bora wabaki peke yao.
 
People's power will sustain. Ni fundisho la awali kwa wabunge wa Chadema kwamba wako pekeyao kwenye upinzani.
 
Anne Makinda – 265 (74%)
Marando – 53 (16%)
Zilizoharibika – 9

Jumla ya kura - 327
 
Hakuna wa kumpa changamoto ambayo hataiweza.


Kishongo we vipi? Huyu mwanamke alishindwa mikikimikiki ya Wangwe moja tu. Sasa tuna akina wangwe kibao ndani ya bunge nakuambia atakoma.
 
Ameapa mwanasheria mkuu Werema, anafuata Anna Abdalla
 
Jambo moja ambalo CCM wanashindwa kulielewa ni ile kanuni ya maisha kwamba kila kitu kina climax yake na ikifika hapo basi kinachofuata ni kuporomoka. Zimepita dola nyingi tu dunia, wanahistoria watatusaidia lakini za karibuni ni ile ya Warumi, Wajerumani, Waingereza na sasa Wamarekani ambao nao tayari wameanza kuwahofia Wachina.

Kwa kanuni hiyo ni wazi CCM itaanguka tu, na tayari dalili zimeanza kuonekana, na hata wakilazimisha vipi haitawezekana kuzuia mabadiliko. Wametumia sana usanii katika miaka ya karibuni, bado hali sio nzuri kwao kinachokuja ni kuporomoka hata watumie risasi, wakati ukifika watatoka tu.
 
Back
Top Bottom