Elections 2010 Uchaguzi wa Spika wa bunge la 10 la Tanzania

Elections 2010 Uchaguzi wa Spika wa bunge la 10 la Tanzania

Tangu Nyerere aseme hivyo hilo lilishatekelezwa? Wengine hatutaki / hatuwezi kugombea uongozi kwa mengi tu.

dah sasa talent yako inapotea hivi hivi..tuangalia utaratibu ambao ni more inclusive ....hivi Kingunge anaapiaga nn?


Mh Regia Anaapa sasa.....LIVE on Star TV....
 
Regia Mtema ndo anakula kiapo cha kuwa mwaminifu kwa jamhuri na katiba
 


MATOKEO:

Kura zilizopigwa jumla ni 327
Zilizoharibika ni kura 9 -

Anna...kura 265....SPIKA 74.2%

Marando.....kura 53
[/QUOTE]

Hivi katika hizo kura 9 zilizoharibika ni za wabunge waliochaguliwa na wananchi ??? Kwa maana hao wanatakiwa wawe mstari wa mbele kuelimisha wapigaji kura jinsi ya kupiga kura kwa usahihi !!! kama ni wao na wanakosea kwa chaguzi zenye pembe mbili tuu !!!!
 
Anna Makinda kura 265

Mabere Marando kura 53

Kura zilizoharibika 9
Hii ina maana kwamba Marando amepata kura za kambi ya upinzani tu na Makinda kura za CCM.
Tuombe Mungu kwamba katika uhai wa Bunge hili CCM watabadilika na hawatazingatia mwelekeo wa chama kwa ya hofu ya kulipizwa kisasi na chama chao kama ilivyofanyika kwa Sitta.
Ni wazi CCM wamepata walichokuwa wakikitaka, yaani kumpata Spika mwenye msimamo laini na wanayeweza kumdhibiti kwa "remote control" ingawa wasipokuwa makini jambo hili linaweza kuwa mwanzo wa anguko kuu kwa CCM mwaka 2015.
 
anna makinda kura 265

mabere marando kura 53

kura zilizoharibika 9

duh chadema ndio mjue sasa kuwa siasa ni kwenu tu yaani umoja wa upinzani nao umewaangusha hata kura za uspika.kweli nyota njema uonekana asubuhi.yaanai hadi wale wanaojiiita wapambanaji wa ufisadi wamempa kura anna makinda?mh kweli siasa is a zero game...
 
hata cifa za kuwa kiongozi huna

Moja, hunijui na hivyo huwezi kujua hilo, unless unataka kuwa mpayukaji tu.

Mbili, hata kama hilo lingekuwa kweli, you are missing the point. This is not about me, it is about a whole section of the Tanzanian population who do not believe in god.

But I know you will never get that through your head, it is probably 100 years too advanced for you, maybe your grandchildren will get it.
 
Amepata kura za chadema pekeyake, sasa hapa kazi ipo na cjui huo upinzani ndani ya bunge kama kutakuwa na upinzani wa nguvu kwa chama tawala,
Chadema peke yao wapo 45 na yeye amepata kura 53 nadhani reale2m hauko sahihi tupunguze ushabiki jamani...japokuwa Cuf sidhani km wamepa kura hata moja cause jamaa wana ubia na CCM na wamegoma hata kuunganisha nguvu na kuwa na kambi moja ya upinzani kaaazi kwelkweli
 
Ulikuwa hujui??

CCM is under trap.

Tutawaeleza wananchi why Chadema and not those idiot puppets?
 
Makinda anayokazi ya kuhimili nguvu ya wapiganaji wa CHADEMA. Hawa wengine sijui CUF hana shida nao kwakuwa ni 2nd CCM.
 
Kifo cha nyani miti yote hutereza mpendwa, huwezi zuia riziki ya mtu sana sana utaichelewesha tu but mwisho wa siku lazima ataipata. Na ndivyo nyie mafisadi mlivyofanya kuziba riziki ya wananchi kupata maisha bora kwa kumchagua Rais bora na makini mwenye uzalendo na nchi yake then mkawaibia kura zao wananchi na kumpa yule wasiyemtaka kwa ubinafsi wenu na wa watoto wenu, hakina laana zote zi juu yenu.
 
Halafu hii habari ya kila mbunge kuapa pekee inapoteza muda tu, wangeapishwa wote kwa mpigo, ukiwa bungeni na hujakataa iwe binding. Sio watu wanatumia kikao kizima kuapishana tu, wanaongeza gharama tu bila ufanisi.
 
Mh Sitta ndo anaenda kuapa sasa...anashangiliwa na wabunge hapa....what aturn over anaapishwa na aliyekuwa naibu wake! maisha lazima yaendelee...
 
inaonyesha 6 bado ni chaguo la wengi, mbona kapigiwa makofi???!!!!
 
Hii ni rough estimate ya jinsi Spika wa Bunge alivyochaguliwa leo na Wabunge:

Jumla ya wabunge waliopiga kura = 327

Kura zilizoharibika = 9

Anne Makinda = 265 (74%)

Mabere Marando = 53 (16%)

Wabunge wa CCM = 251

Wabunge wa Chadema = 45

Wabunge wa CUF = 32

TLP = 1

UDP = 1

NCCR = 4

Ukiangalia idadi ya wabunge hapo juu inadhihirisha kuwa Marando kapigiwa na wabunge wa Chadema, TLP, UDP na NCCR tu.

Wabunge wa CUF wameungana na wabunge wa CCM kumpigia kura Makinda.

Kuna tetesi kuwa wabunge wa CUF walipata maelekezo kutoka kwa Rostam Aziz kupitia kwa Jussa kumpigia kura Anne Makinda.
 
hongera kwake,ila tunachotaka ni utendaji wala sio ubabe
 
Halafu hii habari ya kila mbunge kuapa pekee inapoteza muda tu, wangeapishwa wote kwa mpigo, ukiwa bungeni na hujakataa iwe binding. Sio watu wanatumia kikao kizima kuapishana tu, wanaongeza gharama tu bila ufanisi.

Hapa nakubaliana na wewe..imagien TV stations kubwa zote zinaonyesha hii kitu live.....wangeapa kwa mpigo bana....
 
Anna makinda nasikia kapita ila sijafahamu kwa kura ngapi
Na pia MARANDO sijafahamu kapata kura ngapi
 
Back
Top Bottom