Uchaguzi wa Spika wa Bunge na uthibitisho wa Waziri Mkuu mpya kufanyika Novemba 11, 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Kufuatia Tangazo la Rais la kuitisha Bunge lililotolewa kwenye Gazeti la Serikali, Toleo Maalum Na. 11 (Special Supplement) la tarehe 4 Novemba, 2025 Tangazo Na. 647A Wabunge Wateule wote wanafahamishwa kwamba shughuli za usajili na taratibu nyingine za kiutawala zitafanyika Ofisi ya Bunge Dodoma kuanzia tarehe 8 hadi 10 Novemba, 2025.

Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa Kwanza wa Bunge la 13 kitafanyika tarehe 11 Novemba, 2025 kama ilivyotamkwa kwenye Tangazo la Rais; na shughuli zitakazofanyika katika Mkutano huo ni pamoja na:-

(a) Kusomwa Tangazo la Rais la kuitisha Bunge;
(b) Uchaguzi wa Spika;
(c) Kiapo cha Uaminifu kwa Wabunge wote;
(d) Kuthibitisha uteuzi wa Waziri Mkuu;
(e) Uchaguzi wa Naibu Spika; na
(f) Ufunguzi rasmi wa Bunge Jipya utakaofanywa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Utaratibu wa uchaguzi utakaotumika kujaza nafasi ya Spika na Naibu Spika umetangazwa katika Tangazo Na. 14824A na Na. 14824B kwenye Gazeti la Serikali Toleo Maalum Na. 11 (Special Supplement) la tarehe 4 Novemba, 2025.

Aidha, inasisitizwa kwamba Wabunge Wateule wote wafike wakiwa wamevaa mavazi rasmi kwa ajili ya zoezi la usaili na upigaji picha pamoja na nyaraka zifuatazo:-

(a) Hati ya Kuchaguliwa/Kuteuliwa kwa Mbunge;
(b) Kitambulisho cha Taifa na nakala yake;
(c) Kadi ya Benki yenye Namba ya Akaunti ya Mbunge;
(d) Cheti halisi cha Ndoa kinachotambuliwa na Serikali (kwa wenye Ndoa) na nakala yake;
(e) Vyeti halisi vya kuzaliwa vya watoto wenye umri chini ya miaka 21 (kwa wenye watoto/wasiozidi wanne) na nakala;
(f) Vyeti halisi vya Elimu/Taaluma vyenye ithibati ya taasisi husika na nakala zake;
(g) Wasifu wa Mbunge (Curriculum Vitae).

1762325855129.png
 
Msajili wa vyama vya siasa chadema hakistahili kuwa chama ndani ya nchi hii,kifutie usajili.
 
Nani anamjua mwenyekiti wake wa mtaa,diwani na mbunge wake ?
 
Matokeo ya wabunge yame tangazwa yote kweli au wanaend akama wame itwa shule kwa kua walikua wame jisajiri team ya ushindi tayari
Kama unaishi kenye huwezi kujua kama matokeo yalibendikwa kwenye maeneo yetu
 
Kufuatia Tangazo la Rais la kuitisha Bunge lililotolewa kwenye Gazeti la Serikali, Toleo Maalum Na. 11 (Special Supplement) la tarehe 4 Novemba, 2025 Tangazo Na. 647A Wabunge Wateule wote wanafahamishwa kwamba shughuli za usajili na taratibu nyingine za kiutawala zitafanyika Ofisi ya Bunge Dodoma kuanzia tarehe 8 hadi 10 Novemba, 2025.

Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa Kwanza wa Bunge la 13 kitafanyika tarehe 11 Novemba, 2025 kama ilivyotamkwa kwenye Tangazo la Rais; na shughuli zitakazofanyika katika Mkutano huo ni pamoja na:-

(a) Kusomwa Tangazo la Rais la kuitisha Bunge;
(b) Uchaguzi wa Spika;
(c) Kiapo cha Uaminifu kwa Wabunge wote;
(d) Kuthibitisha uteuzi wa Waziri Mkuu;
(e) Uchaguzi wa Naibu Spika; na
(f) Ufunguzi rasmi wa Bunge Jipya utakaofanywa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Utaratibu wa uchaguzi utakaotumika kujaza nafasi ya Spika na Naibu Spika umetangazwa katika Tangazo Na. 14824A na Na. 14824B kwenye Gazeti la Serikali Toleo Maalum Na. 11 (Special Supplement) la tarehe 4 Novemba, 2025.

Aidha, inasisitizwa kwamba Wabunge Wateule wote wafike wakiwa wamevaa mavazi rasmi kwa ajili ya zoezi la usaili na upigaji picha pamoja na nyaraka zifuatazo:-

(a) Hati ya Kuchaguliwa/Kuteuliwa kwa Mbunge;
(b) Kitambulisho cha Taifa na nakala yake;
(c) Kadi ya Benki yenye Namba ya Akaunti ya Mbunge;
(d) Cheti halisi cha Ndoa kinachotambuliwa na Serikali (kwa wenye Ndoa) na nakala yake;
(e) Vyeti halisi vya kuzaliwa vya watoto wenye umri chini ya miaka 21 (kwa wenye watoto/wasiozidi wanne) na nakala;
(f) Vyeti halisi vya Elimu/Taaluma vyenye ithibati ya taasisi husika na nakala zake;
(g) Wasifu wa Mbunge (Curriculum Vitae).

Mtasababisha watu fulani walale kwa Wganga week nzima.
 
Msajili wa vyama vya siasa chadema hakistahili kuwa chama ndani ya nchi hii,kifutie usajili.
Chadema sio chama hata wakifuta ni spirit waliyonayo watu ni kubwa mno Chadema hata ikifa mkuu sasa hivi hata mtu mmoja anaweza kuitisha bila Chama pata Lissu hana chama akiitisha maandamano itakuaje maana atakusanaya watu wote wa vyama vyote na ambao hawana vyama maana yeye hana chama LISSU chama ni rahisi sana kuliko Lissu hana chama
 
Msajili wa vyama vya siasa chadema hakistahili kuwa chama ndani ya nchi hii,kifutie usajili.

We shetani mwendawazimu utapiga kelele sana dhidi ya CHADEMA, lakini kwa sababu CHADEMA inatetea haki, kamwe hakitakufa. Utakufa wewe na ushetani wako, utaiacha CHADEMA inaendelea. CHADEMA itakufa endapo tu itaungana na ninyi mashetani kudhulumu haki.
 
Kumbe wabunge wa viti maalum huwa hawachagui Spika,Okay.

Halafu mbona INEC huwa hawaweki matokeo ya ubunge ya majimbo yote katika website yao.

Kweli wale hawajui wanachokifanya ndio maana tunakuwa na chaguzi za namna hii.
 
Back
Top Bottom