Uchaguzi Zimbabwe, upinzani Tanzania bado hatujifunzi?

Uchaguzi Zimbabwe, upinzani Tanzania bado hatujifunzi?

Uchaguzi wa karibuni kwenye mazingira kama yetu, ni huu wa juzi Zimbabwe.

Waangalizi mbali mbali mbali wakiwamo SADC, Carter Center na wengine, wamelazimika kuuita kwa majina lake. Yaani kwa ufupi, wameuona siyo uchaguzi bali ni wizi wa mchana kweupe.

Hapa chini ni sampuli za yale matokeo pendwa ya zile tume zetu za kizalendo kutokea vyama tawala kama yanavyoendelea kutolewa:

View attachment 2729187

View attachment 2729188

Hiyo CHADEMA ya huko (CCC) ndipo Sasa watajua kumbe walikuwa hawajui.

Kibaka ni kibaka tu.

Ajabu na kweli hiki chama cha upinzani, CCC kilikwenda kufanya nini kwenye uchaguzi wa namna hii? Kwa hiyo sasa ndiyo waanze kulalamika siyo? Kwamba walikuwa wamesahau nini?

Haya si ndiyo ya kwetu CHADEMA, ACT na wenye kujinasibu kusaka ukombozi wa nchi hii watakayokuja kuyalalamikia 2024 na baadaye 2025?

Hivi kweli hiyo itakuwa ni akili, au matope?

Kwani hata haya 2020 hatukuyasikia?

View attachment 2729204

Au ni kuchagua kuwa kama mang'ombe tu?

Enyi ndugu mnaojielekeza kwenye kushiriki uchaguzi mkuu 2024/25 bila shaka kwa msukumo wa njaa zenu binafsi, siyo siri kuwa mnaturudisha nyuma sana kwenye ukombozi wa nchi hii.

Ama kwa hakika mkisikia tunawaita ni wasaliti bila kujali nyadhifa zenu au historia, wala msishangae.

Si mkajiunge hata na kina Makhtoum kwenye biashara za bandari huko kama taabu yenu kumbe ni njaa za matumbo yenu na familia zenu tu?

Ifahamike hatuujui msimamo mwingine baina yetu zaidi ya huu:

Uchaguzi bila katiba mpya wa nini?
Una hoja nzito sana
 
Kwa ukweli bila Katba mpya ni Bora kususia tu uchaguzi.
Kwa hiyo katiba mmpat ndio itawapitia wanachama wapya au? Nyie endeleeni tu kidanganywa na mchezo disco kuwa tatizo ni katiba.SAD
 
Una hoja nzito sana

Tokea juu hadi chini tunapaswa kuamua kusuka au kunyoa. Si kulaumiana. Kama vipi tunawahitaji kina Mwabukusi juu kuliko wakati mwingine, vinginevyo bado tupo tupo sana.
 
Back
Top Bottom