Elections 2010 Uchakachuaji HAUPO! - NYARAKA HIZI HAPA NI FAKE

Elections 2010 Uchakachuaji HAUPO! - NYARAKA HIZI HAPA NI FAKE

Status
Not open for further replies.
With all due respect to you Invisible.

Nina kila sababu za kuamini kuwa hii barua ni feki. Naomba wanaharakati muwe makini sana kwenye kutumia hii barua kama uthibitisho wa wizi wa kura.

Bandiko langu hili sio la kumuandama Invisible (a friend and a guy I respect) BUT ni kumu-alert kuwa inawezekana amelishwa kasa.

Uchunguzi uendelee ili kuthibitisha authenticity ya hiyo barua.

Ila kwa sasa, wapiganaji wote tuelekeze nguvu zetu kwenye kuhakikisha kuwa vijana wote wanafika kwenye vituo vya kupiga kura na wanapiga kura kwa wingi sana. Kwa pamoja tutaweza kubadilisha uongozi wa nchi yetu na kuwaondoa hawa majambazi waliopora maliasili zetu zote kwa manufaa yao binafsi na familia zao.

Najua nitaumiza baadhi ya ego for this BUT I had to do this today.

Sasa kwa nini usituwekee hizo sababu hapa?? Hivi kweli mlitegemea baada ya mkutano huo, huyo Kabwe angeanza series nyingine ya mikutano kupeleka ujumbe?? Hivi unafikiri nani angemuamini zaidi ya kutumia nafasi na madaraka yake ya kiofisi?? Tushaona skendo kibao duniani ambazo ni nyeti kuliko hii lakini kunakuwa na nyaraka au memo uchunguzi unapokuja kufanyika baadaye.
 
Huwezi kusema ni feki tu bila uthibitisho. Maana kila kitu kinachokuja usivyotaka utakataa ndio maana kuna mahakama. Kazi yake sio kusikiliza tu watu wanachosema bali kukithibitisha kwa ushahidi, na wewe fanya hivyo pia maana hatufanyi mashairi bali tunaweka hoja za msingi hapa.

sina uthibitisho mkuu na samahani kwa hilo, nimetoa tu mawazo yangu kwenye hili.
 
Tuwe makini katika kipondi cha lalasalama. Kinachofanyika sasa hivi ni kujaribu kukatisha tamaa watu wanaounga mkono opposition wasiende kupiga kura. Njia mojawapo ni kuonyesha kuwa uchaguzi umeshaibwa ili watu waone kwamba hakuna haja ya kwenda kupiga kura. Ikitokea hivyo watakaoenda vituoni ni wana ccm pekee. Barua hii ni sehemu ya hiyo mikakati. Tuikatae mipango hii michafu. Hakuna kura kuibwa. Twendeni tukakpige kura. Cha msingi mawakala wawe imara.

kabisa!
 
Mkuu Invisible, with due respect; Hivi, uliona wapi wafanya magendo au wala rushwa wakapeana risiti? nadhani hiyo barua ndio uchakachuaji wenyewe na aliyeitoa anakusudia kujenga hofu na kuwababaisha watu.
Uzoefu wangu wa rafu za uchaguzi huwa hakuna maandishi labda pale mnapotaka kujenga mazingira ya kufungua kesi kupinga matokeo.

Kwani vile vi-memo vilivyomwangusha Lowassa ilikuwaje?
 
Jamani Inv sio mtu wa Kukurupuka tu, hawezi kuweka kitu humu ndani bila kuwa na Source ya kueleweka, MWAFRIKA, AMA NA BUCKREEF, msipotoshe watu, Hii barua ni ya kweli sijaona mtu wa kunishawishi kuwa hii barua ni FAKE
 
Sasa kwa nini usituwekee hizo sababu hapa?? Hivi kweli mlitegemea baada ya mkutano huo, huyo Kabwe angeanza series nyingine ya mikutano kupeleka ujumbe?? Hivi unafikiri nani angemuamini zaidi ya kutumia nafasi na madaraka yake ya kiofisi?? Tushaona skendo kibao duniani ambazo ni nyeti kuliko hii lakini kunakuwa na nyaraka au memo uchunguzi unapokuja kufanyika baadaye.

Sawa mkuu,

Haya ni mawazo yangu tu ( I will be as polite as I can). Unaweza kuyakubali au kuyakataa.
 
Acha fix, hii kitu siyo mpya hapa, imeanza kujadiliwa hapa na mifano toka juzi, acha kudesa.

Tundika hapa zile karatasi mlizo kamata kule mpakani.

nimekupigia senksi mkuuu.
Kasema anabandika karatasi ... kaingia mitini. Angekuwa mkweli angejibu yale yote aliyoulizwa kwenye ile thread ya Tunduma au angeomba samahani kwa kushindwa kuieweka.
Alidanganya watu siku ya kwanza lakini ameshashtukiwa.
 
We jamaa zero... Scientifically unaposimama hadharani kusema ni feki unatakiwa kuonyesha original ni ipi na sio kubwabwaja tu, heri ungekaa kimya na imani yako kuwa feki kuliko kupost thread bila kuonyesha original yake. Heri yenu msioamini kila kitu maana hamtaamini pia kama ccm inaanguka mwaka huu.
 
Jamani Inv sio mtu wa Kukurupuka tu, hawezi kuweka kitu humu ndani bila kuwa na Source ya kueleweka, MWAFRIKA, AMA NA BUCKREEF, msipotoshe watu, Hii barua ni ya kweli sijaona mtu wa kunishawishi kuwa hii barua ni FAKE

we waangalie wamejiunga lini jf sis tunamjua invisible hakurupuki katika post zake na ni mtu muhimu sana humu jf
 
Jamani Inv sio mtu wa Kukurupuka tu, hawezi kuweka kitu humu ndani bila kuwa na Source ya kueleweka, MWAFRIKA, AMA NA BUCKREEF, msipotoshe watu, Hii barua ni ya kweli sijaona mtu wa kunishawishi kuwa hii barua ni FAKE

tuko pamoja ! Kitila hakuna shaka kabisa kura kupiga tutakwenda,lakini hii barua si fake! yani labda Invisible hawe mwengine kuwika kitu hapa pasi kuwa na uhakika nacho. kura tutapiga wala mjadala hakuna,lakini hii karatasi si fake.
 
With due respect. Invisible nakuaminia na nimekuwa napenda post zako. Kwa hili nasita kuamini. Kwanza kwa wale wenye kumbukumbu tarehe 16.10.2010 Kikwete alikuwa Mkoa wa Pwani ziara aliyoanza tarehe 15.10.10. Tarehe 17.10.10 alikuwa Mkoa wa Dar. Yaani hata hao walioandika barua ya magizo je hawakujua ratiba hiyo? Barua inaonesha mwandishi hajui kanuni za kuandika barua. Kwanza haina Kumbukumbu. Barua kama hizi lazima zipigwe muhuri wa "SIRI" au "Confidentail". Kichwa cha barua yenyewe kinatia mashaka. Na mwandishi anaonekana kukosa weledi wa kuandika barua za Kiserikali. Kwa mimi naona barua hiyo si barua ya kweli. Ebu rejea source ya barua hiyo na ujiridhishe kama ni credible.

Dar hadi Mza ni saa moja tu, kama JK alikuwa pwani mchana inawezekana kabisa usiku akaenda Mwanza.... We sema unakataa kwa sababu nyingine lakini usijiweke ktk kundi la wapumbavu wanaodhani dar mwanza ni mwezi mzima
 
we waangalie wamejiunga lini jf sis tunamjua invisible hakurupuki katika post zake na ni mtu muhimu sana humu jf

ID ya Edson imesajiliwa March 2009, na ya Kituko imesajiliwa January 2009. Kati ya Edson na Kituko nani mgeni humu JF? Au ulidhani umetumia ID yako ya zamani?
 
napenda kumtahadharisha mleta mada kuwa mkiendelea kuweka makaratasi ya kutunga hapa, mtapata matatizo na wanachama wa JF watakosa mahali pa majadiliano. kuweni waangalifu
 
mkuu,
hii analysis yako ndio haswaa watakachofanya.
Please nakuomba sana - hili bandiko lako lianzishie thread ya peke yake.
Kuliacha Ktk hii thread litazikwa na kusahaulika, watu wengi hawataliona na utakuwa hujaifanyia justice post yako na members.
Please just do it. It's extremely important.
Asante.

Nimeweka kwa jina la 'Kura zimeshaibiwa, Kwikwete 80% kaishinda' lakini baada ya dakika 2 imetoweka.
 
Tukubali kulipa gharama ya kulinda amani na utulivu tuliojijengea toka uhuru.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom