Elections 2010 Uchakachuaji HAUPO! - NYARAKA HIZI HAPA NI FAKE

Status
Not open for further replies.

Sasa kwa nini usituwekee hizo sababu hapa?? Hivi kweli mlitegemea baada ya mkutano huo, huyo Kabwe angeanza series nyingine ya mikutano kupeleka ujumbe?? Hivi unafikiri nani angemuamini zaidi ya kutumia nafasi na madaraka yake ya kiofisi?? Tushaona skendo kibao duniani ambazo ni nyeti kuliko hii lakini kunakuwa na nyaraka au memo uchunguzi unapokuja kufanyika baadaye.
 
sina uthibitisho mkuu na samahani kwa hilo, nimetoa tu mawazo yangu kwenye hili.
 
kabisa!
 
Kwani vile vi-memo vilivyomwangusha Lowassa ilikuwaje?
 
Jamani Inv sio mtu wa Kukurupuka tu, hawezi kuweka kitu humu ndani bila kuwa na Source ya kueleweka, MWAFRIKA, AMA NA BUCKREEF, msipotoshe watu, Hii barua ni ya kweli sijaona mtu wa kunishawishi kuwa hii barua ni FAKE
 
Sawa mkuu,

Haya ni mawazo yangu tu ( I will be as polite as I can). Unaweza kuyakubali au kuyakataa.
 
Acha fix, hii kitu siyo mpya hapa, imeanza kujadiliwa hapa na mifano toka juzi, acha kudesa.

Tundika hapa zile karatasi mlizo kamata kule mpakani.

nimekupigia senksi mkuuu.
Kasema anabandika karatasi ... kaingia mitini. Angekuwa mkweli angejibu yale yote aliyoulizwa kwenye ile thread ya Tunduma au angeomba samahani kwa kushindwa kuieweka.
Alidanganya watu siku ya kwanza lakini ameshashtukiwa.
 
We jamaa zero... Scientifically unaposimama hadharani kusema ni feki unatakiwa kuonyesha original ni ipi na sio kubwabwaja tu, heri ungekaa kimya na imani yako kuwa feki kuliko kupost thread bila kuonyesha original yake. Heri yenu msioamini kila kitu maana hamtaamini pia kama ccm inaanguka mwaka huu.
 
Jamani Inv sio mtu wa Kukurupuka tu, hawezi kuweka kitu humu ndani bila kuwa na Source ya kueleweka, MWAFRIKA, AMA NA BUCKREEF, msipotoshe watu, Hii barua ni ya kweli sijaona mtu wa kunishawishi kuwa hii barua ni FAKE

we waangalie wamejiunga lini jf sis tunamjua invisible hakurupuki katika post zake na ni mtu muhimu sana humu jf
 
tuko pamoja ! Kitila hakuna shaka kabisa kura kupiga tutakwenda,lakini hii barua si fake! yani labda Invisible hawe mwengine kuwika kitu hapa pasi kuwa na uhakika nacho. kura tutapiga wala mjadala hakuna,lakini hii karatasi si fake.
 
Dar hadi Mza ni saa moja tu, kama JK alikuwa pwani mchana inawezekana kabisa usiku akaenda Mwanza.... We sema unakataa kwa sababu nyingine lakini usijiweke ktk kundi la wapumbavu wanaodhani dar mwanza ni mwezi mzima
 
we waangalie wamejiunga lini jf sis tunamjua invisible hakurupuki katika post zake na ni mtu muhimu sana humu jf

ID ya Edson imesajiliwa March 2009, na ya Kituko imesajiliwa January 2009. Kati ya Edson na Kituko nani mgeni humu JF? Au ulidhani umetumia ID yako ya zamani?
 
napenda kumtahadharisha mleta mada kuwa mkiendelea kuweka makaratasi ya kutunga hapa, mtapata matatizo na wanachama wa JF watakosa mahali pa majadiliano. kuweni waangalifu
 
Nimeweka kwa jina la 'Kura zimeshaibiwa, Kwikwete 80% kaishinda' lakini baada ya dakika 2 imetoweka.
 
Tukubali kulipa gharama ya kulinda amani na utulivu tuliojijengea toka uhuru.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…