Nakubaliana na wewe. Kinachonishangaza sijui watanzania elimu yetu ni ya namna gani...mimi ni mfanyakazi mbali ya Basic Salary yangu kuna sitahiki zingine kama house rent allowance nk. vinaunganishwa na mshahara wangu na kukatwa kodi. Kwahiyo Mhe. Jerry Silaa ana hoja ya msingi kwamba zile posho wanazopata wabunge nje ya mshahara wao zijumuishwe na kukatwa kodi kama wafanyakazi wengine wa umma na binafsi. Jiulize, kama mbunge anapewa posho kwa ajili mishahara ya wasaidizi wake je, akishawalipa PAYE yao anaipeleka TRA au inakuwaje?
PAYE, short for Pay-As-Your-Earn, is a Tanzanian withholding tax applied on taxable incomes of applicable employees. Every employer in Tanzania is required, by law, to deduct the tax from an employee's taxable salaries or wages and submit such deductions to the Tanzania Revenue Authority
Ndio maana Basic Salary na sitahiki zote ni mapato kutoka kwa mwajiri wako ni lazima yakatwe kodi. Kinachonisikitisha sheria zipo lakini watanzania wengi hawajui hii PAYE inapatikaje, Pathetic. Hivyo basi kama hizo posho zingine za wabunge hazikatwi kodi basi ni wakati mwafaka kubadili sheria iliyopo na kuanza kukatwa kodi kama wafanyakazi wanavyokatwa posho za mafuta ya gari na posho ya kwa ajili ya pango (rent).