Uchambuzi Fikilishi Kuhusu Majibu ya Hospitali ya Mlonganzila Kufuatana na Tuhuma ya Huduma za Hospitali Hiyo ya Taifa Muhimbili-Mlonganzila

Uchambuzi Fikilishi Kuhusu Majibu ya Hospitali ya Mlonganzila Kufuatana na Tuhuma ya Huduma za Hospitali Hiyo ya Taifa Muhimbili-Mlonganzila

the power

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
407
Reaction score
799
aada ya Wanachama wa JamiiForums.com kuandika hoja zinazoitaja Hospitali ya Muhimbili - Mlonganzila kuwa na gharama kubwa na changamoto nyingine za kiutendaji, taasisi hiyo imetoa ufafanuzi. Kusoka hoja za Wadau bofya hapa chini:

~ DOKEZO: Serikali iimulike hospitali ya Mloganzila, Huduma zake ni janga kwa wagonjwa na ndugu wanaouguza pale

~ Gharama za Kujifungua Hospital ta Taifa Muhimbili MNH (Mloganzila) ni kufuru

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MLOGANZILA_page-0001 (1).jpg


Nimesoma kwa makini tuhuma za huduma za Hospitali ya Taifa ya Muhimbili-Mlonganzila kama zilivyotolewa na Mleta mada "DOKEZO: Serikali iimulike hospitali ya Mloganzila, Huduma zake ni janga kwa wagonjwa na ndugu wanaouguza pale" na lingine "Gharama za Kujifungua Hospital ta Taifa Muhimbili MNH (Mloganzila) ni kufuru" .Kwa kweli nimesikitishwa sana na majibu yaliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma Bwana Aminiel Bubera Alogaesha;Soma majibu yake hapo juu, kwa kweli hajaitendea haki fani yake, ni bora angenyamaza.

Swali la kujiuliza ni hili hivi huyu mkuu kweli kajiridhisha na majibu yake kama msomi mbobezi wa fani ya mawasiliano, je wakati anasoma chuo na wakati akijiendeleza hakuna sehemu alijifunza sanaa ya kujibu tuhuma dhidi ya Kampuni au mtu binafsi(the art of respsonding to the public critics in a firm or as an individual). Nimesema "the art " kwa sababu hiyo ni fani ya sanaa na majibidhano ni sanaa inayohitaji facts na relevant data lakini lugha fulani ya kisanii.

Nilitegemea bwana Aminiel asome tuhuma hizo kwa kutulia, bila mihemuko, bila kupanik, halafu arejee hoja za mtoha tuhuma,

Nilitegemea afunge safari ahende Mloganzila kama yeye yuko compass ya muhimbili (main quarter), afanye mrejeo wa ghalama halisi za huduma Mloganzira, afanye mrejeo wa wa nyuma wa wastani wa vifo (retrospective death statistical review for the past at least 6 months), achambue kwenye jedwali average deaths per month, per week and per day , afafanue the peak average deaths per month, weeks and per day, zaidi apite kwenye vitengo vyote anonymously na kutafiti responses ya watoa huduma (systematically), afanye random post-service interviews ya wateja kuhusu suala la huduma stahiki (respective care) ikijumuhisha majibu na maelekezo wanayopewa wateja na watoa huduma.

Baada ya hapo kabla ya kujibu ahorodheshe zile tuhuma moja baada ya nyingine, halafu aanze kuzijibu logically and systematically supported by data and research information kama alivyozichambua mtoa tuhuma, huku akivunja hoja za mtoa tuhumama kwa kutumia takwimu sahihi za hospitali akiambatanisha na sample za malipo au copy ya ghalama za hospitali pamoja na kutumia majibu ya utafiti wake na observation yake kuhusu huduma stahiki (respective care). Ni lazima aeleze amepata wapi hizo takwimu na taarifa na kwa njia ipi? (the where and how) , ningependa atumie njia ya Kisayansi tajwa hapo juu. Hapo ndipo angekuwa amejibu hoja kama msomi, kama msemaji wa institution kubwa kama Muhimbili. Kwa jinsi alivyojibu hana tofauti na majibu ambayo yangetolewa na mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa mass communicatioon SAUTI, kumbuka tumezoea kutoa majibu ya kisiasa kwenye mambo makubwa ya kisayansi (we have reached a turning point of politicizing mod of our serious matters as if we are politicians and not scientists).

Lalamiko la msingi na kubwa la mtoa tuhuma ilikuwa ni ghalama kubwa ya laki moja ya kitanda kwa siku tena kwa mtoto na mama yake separately hapo hujaweka vipimo na madawa (ingawa tulihaminishwa watoto chini ya miaka 5 na mama wajawazito huduma zao ni bure, sijui policy inasemaje kwenye tertially refferal hospitals)). Bwana Aminiel Buberwa angeonyesha je kwa sasa ghalama halisi ni kiasi gani? na je mama analipa separately na mtoto? kama ndivyo kwa nini? je hiyo ghalama ni inclusive ya madawa na vipimo au ni kwa kitanda tu? kama ni inclusive ina-make a lot of sense kwani vipimo na dawa ni ghalama sana lazima wafanye resonable and affordable ecost -sharing. Kumbuka hakuna mtu aliyemuomba msomi mbobezi Aminiel takwimu za misamaa, amejibu contraly to the issues raised, very irrelevant responses kama vile hakuwa amelisoma andiko la tuhuma. Kwa sababu amekwepa lalamiko la msingi, kwa sisi tuliosma Cuba tunaweza kusema mtoa tuhuma yuko sahihi, huduma ya kitanda tu ni shilingi laki moja kila mmoja tofauti mama na mtoto ,ina maana laki mbili (200,000/Tsh) kwa siku bila ghalama za matibabu na vipimo unless stated differently with cristal clear supporting evidences.

Lalamiko la pili la msingi la mtoa tuhuma ni ongezeko la vifo , mtoa tuhuma kasema vifo ni average ya ishirini (20) kwa siku, cha kushangaza Msomi mbobezi Aminiel Buberwa kasema ni vifo vinne (4) mpaka sita (6) kwa siku (Mimi sihamini kabisa takwimu zake). Sasa sisi consumer wa information hizi tumuamini nani? hajasema source yake na methodology aliyotumia, kibaya statistically hajasema variation (mean, average, peak ) ya vifo kwani kuna cation) ni nini na kibaya hajasema ni vifo vya mama wajawazito na watoto tu au ni vifo vyote kwa ujumla (adult and childrens).

Ametoa hoja nzuri kuhusu idadi kubwa ya wagonjwa ila ameshindwa kuitetea kisomi (failure to make a strong case/linking variables/show association between contradicting urgument), Labda ndugu msomaji wa jamii forum, kwa taarifa yako, indisputable multiple peers review journals zimeconclude "kuwepo kwa uhusiano mkubwa sana kati ya idadi ya clients na severity of illness ya clients admitted ukilinganisha na ongezeko la vifo vya clients hao (There is a statistical significant association between number of clients admitted and the severity of their illness with increasing number of their deaths /likel-hood to die). Sasa ameshindwa kujenga hoja na kuvunja tuhuma za mtoa mada, strategic response of critics is an art, angeongezea pia kumbuka Mlongaznila ni tertially referral hospital, tunategemea terminally ill patients wawe wengi ambao wamekuwa reffered from regional na district hospitals, kwa hiyo ongezeko la idadi ya vifo si jambo la kushtusha sana. Hivyo ndivyo watu wataalamu wanavunja hoja kisayansi na ndio maana strategy ya kitaifa ni kuboresha capacity na huduma za afya kwenye lower health facilities-kwenye health center, districts na regional hospitals ili ku-decongest referral hospitals kama mloganzila.

Tuhuma ya tatu ilikuwa ni lugha hisiyo staha kwa clients na kutopatikana kwa maelezo ya kutosha. Sasa msomi na mkuu wa Kitengo cha mawasiliano na mahusiano ya umma Muhimbili Bwana aminiel kamute kabisa /hajajibu as if hii hahikuwa hoja ya msingi. Labda nimueleweshe kama hajui respective care services ni sehemu muhimu kwenye huduma ya tiba kama zilivyo huduma za vipimo na madawa. Angechukua muda na kufanya utafiti wa Kisayansi elekezwa hapo juu na kuja na majibu yaliyokuwa supported na utafiti (evidence-based\0, hata kama yangenatana na tuhuma, muhungwana hujutama, angesema , uongozi wa hospitali utalichukulia suala hili kwa uzito mkubwa na kuhakikisha hali inabadilika;huo ndio usomi.

Kwa kumalizia msomi Aminiel Buberwa alijua kuwa anajibu tuhuma zilizochapishwa kenye jamii forum, forum kubwa chambuzi na yakinifu nchini, iliyojaa vichwa, alitakiwa afanye due diligence kabla kubandika andiko lake likijibu vitu tofauti na mtoa tuhuma na kuacha baadhi ya tuhuma muhimu. Naweza kusema tunahitaji arejee tuhuma tajwa mara ya pili na kujibu tuhuma hizo one by one. Kwa Ku summarize " his current responses did not at all systematically addresses the critics /issues raised, thus we consumers deserve another critical, well thought, investigative analytical responses. Au comsumers wenzangu mnasemaje? toa maoni yako hapa chini kuhusu mkwamo huu...
 
Gharama za MNH-Upanga ndo zile zile za MNH-Mloganzila.

Gharama ya kitanda hailipwi kwa siku, inalipwa mara moja mpaka mgonjwa atakaporuhusiwa, hata kama akikaa miezi ama mwaka. Na hiyo gharama ni 50k tu.

Hii 50k nyingine inayoongezeka ni kwa ajili ya zile huduma za mwanzo mwanzo mgonjwa akifika wodini. Hata kama mgonjwa akiruhusiwa kesho yake na hiyo 50k ikawa haijatumika basi unarudishiwa.

Huu ni utaratibu wa hospitali nyingi tu hasa private, mgonjwa akishalazwa anatakiwa a-deposit kiasi kadhaa cha kuanzia huduma, ni utaratibu wa kawaida sana wala hauna maajabu yoyote.

Mgonjwa akiwa hana, sio kizuizi cha yeye kulazwa pia, kuna utaratibu wa kujaza form maalum kupitia maafisa ustawi.
 
Gharama za MNH-Upanga ndo zile zile za MNH-Mloganzila.

Gharama ya kitanda hailipwi kwa siku, inalipwa mara moja mpaka mgonjwa atakaporuhusiwa, hata kama akikaa miezi ama mwaka. Na hiyo gharama ni 50k tu.

Hii 50k nyingine inayoongezeka ni kwa ajili ya zile huduma za mwanzo mwanzo mgonjwa akifika wodini. Hata kama mgonjwa akiruhusiwa kesho yake na hiyo 50k ikawa haijatumika basi unarudishiwa.

Huu ni utaratibu wa hospitali nyingi tu hasa private, mgonjwa akishalazwa anatakiwa a-deposit kiasi kadhaa cha kuanzia huduma, ni utaratibu wa kawaida sana wala hauna maajabu yoyote.

Mgonjwa akiwa hana, sio kizuizi cha yeye kulazwa pia, kuna utaratibu wa kujaza form maalum kupitia maafisa ustawi.
Umejibu vizuri kabisa na Haya ndiyo msjibu msomi mbobezi Aminiel Buberwa alitakiwa kuyatoa kwa ufafanuzi mahili kama ulivyosema. Kumbuka hoja ya andiko hili ni kucritics majibu ya Afisa mawasiliano ya umma kwamba yanapwaya na hayako exhostive na some are irrelevant. Andiko halijaribu kusupport na kupinga uwepo wa tuhuma hizi, Aksante sana mwana jamii kwa ufafanuzi
 
Back
Top Bottom