UCHAMBUZI: Hesabu za Kura 32.7M na Dakika 540 Zinakwama Wapi Kimahesabu?

888I

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
472
Reaction score
581
Wakuu,

Matokeo ya Uchaguzi mkuu yameshatoka na maisha yanaendelea na tumeapishwa. Lakini, kama mdadisi wa mambo, nimekuwa nikicheza na takwimu rasmi za INEC na Sensa yetu ya 2022. Naomba tusaidiane kuzitafakari hizi namba kwa pamoja, maana kwangu kimahesabu picha inagoma kukaa sawa.

Huu si uchambuzi wa nani alishinda, bali ni uchambuzi wa 'process' na uhalisia wa namba zenyewe.

KITENDAWILI CHA 1: Daftari vs. Sensa
Kwanza tuanze na hapa:

1.Watu wenye umri (14+ Miaka) - Sensa 2022: Milioni 35.3
2.Waliojiandikisha Kupiga Kura - INEC 2025: Milioni 37.7

Swali: Tumepata wapi watu Milioni 2.4 wa ziada waliojiandikisha (37.7M) kuliko watu waliopo wenye umri wa miaka 14+ (35.3M)?

-Au Sensa ya 2022 ilikosea na Watanzania tuko wengi kuliko walivyotuhesabu?😃
-Au, Daftari la Kudumu halijahuishwa kwa muda mrefu? Hizi Milioni 2.4 ni "majina hewa" (watu waliofariki, waliohama, waliojiandikisha mara mbili)?🤦
-Kama ni "majina hewa," je, yanaweza kupiga kura? Na kama yanaweza, yalipiga?🙂‍↕️

KITENDAWILI CHA 2: Kura 32.7M vs. Muda (The 540 Minute Puzzle)

Hapa ndipo mambo yanapopata utamu zaidi. Twende na namba rasmi:

1.Jumla ya Kura Zilizopigwa: Milioni 32.7
2.Jumla ya Vituo vya Kura: 99,895
3.Muda Rasmi wa Kura: Saa 1:00 Asubuhi - 10:00 Jioni (Jumla Saa 9 au Dakika 540)

Hesabu Rahisi:

-Wastani wa Kura kwa Kituo: 32.7M Kura / 99,895 Vituo = Wapiga Kura 327 (kwa kila kituo).

-Muda wa Mpiga Kura: Tukichukulia kwa uchache (optimistic) kwamba mpiga kura anatumia Dakika 2 tu (kuingia, kutambuliwa, kupewa karatasi, kupiga kura, kukunja, kutumbukiza).

HESABU SASA:
-Muda Uliohitajika Kituoni: 327 Watu × Dakika 2 = Dakika 654

-Muda Uliokuwepo Kituoni: Dakika 540 (Saa 9)
Utata Upo Hapa: Kimahesabu, kila kituo kilihitaji Wastani wa Dakika 654 (Saa 11) kumaliza wapiga kura wake 327.

- Lakini vituo vilifunguliwa kwa Dakika 540 (Saa 9).
Kila kituo kilipungukiwa na Dakika 114 (karibu Saa 2)!

KITENDAWILI CHA 3: Hoja ya Ukosefu wa Foleni (The 'No Queue' Paradox)

Hili ndilo linalonichanganya zaidi, na hapa naomba mliokuwa "ground" mshuhudie.

1.Matokeo ya Kimahesabu: Ili kura 32.7M zipigwe (86.9% Turnout), vituo vilitakiwa kuwa "busy" na kufanya kazi kwa Saa 11 bila kupumzika. Hii ingesababisha FOLENI KUBWA (misururu) kuanzia asubuhi hadi jioni, na watu wengi kuchelewa kumaliza.

2.Hali Halisi (Niliyoshuhudia na Niliyosikia): Vituo vingi vilikuwa "vimepooza". Hakukuwa na msongamano wa kutisha. Uchaguzi ulionekana kuwa na "hamasa ya kawaida," si ya 86.9% turnout.

Swali la Mwisho: Tunazipatanishaje hizi 'Option' mbili?
Option 1 (Super-Voters): Labda Watanzania walikuwa wepesi sana siku hiyo? Na walitumia Sekunde 99 tu (Dakika 1.6) kupiga kura badala ya Dakika 2 ambazo nimeashumu tu? (540 min / 327 kura = 1.65 min/voter).

Je, inawezekana mtu kumaliza mchakato wote kwa sekunde 99?🤔

Option 2: Labda kulikuwa na vituo vingi "visivyo rasmi" vilivyotumika ambavyo haviko kwenye hesabu ya 99,895? (Hii ni 'wild assumption').😱

Option 3 : Au...Hii 'turnout' ya 86.9% haikuwa ya watu halisi waliofika vituoni? Labda masanduku yalipata "msaada" ili kufikisha idadi ya kura 32.7M?

Option 4: Labda namba za INEC (kura zilizopigwa au idadi ya vituo) zina makosa ya kimahesabu?

Wadau,

Nawasilisha hoja hizi kwenu. Hizi namba na uhalisia wa vituoni ninaona vinapingana.

Hizi kura Milioni 32.7 ziliwezekanaje kupigwa ndani ya Dakika 540 bila kuacha foleni ?😎
Karibuni tujadili kwa HOJA.
 
Hayo mambo mbona yako wazi mkuu au unatafuta sababu wakuteke ubakie stori tu?
 
[
Unauliza ujinga tu kujaza server,
Mwaka 2022-2025 hujui km kuna watoto wamekua wakubwa kupiga Natumain hujamwelewa mtoa mada na xwali amelijibu mwanzon mwa uzi tu yaaaaan kachukua xenxa ya 2022 wale ambao ilipofika 2025 watakuwa tyr wamekidhi vigezo vya kupga kura amejumlixha pia idad yao hapo rudia tena uzi bob
 
usitufokee kwa kutumia x kwenye s halafu mbona hata Gen Z hawatumii hizi siku hizi wewe generation ipi?
 
Anaforce kesi ya uhaini.

Tukiacha utani nchi yetu ina shida kubwa sana, maana hata kudanganya hatuwezi.
Nchi ya mazombie! Unajua 'mama' alidhani watu wangetoka kweli kwenda kutiki akapika matokeo kabla. Ila kusema kweli hawakwenda. Kama kuna mtu ana picha yoyote inayoonesha foleni ya wapiga kura ya 2025 aitume humu
 
Wakuu,

Matokeo ya Uchaguzi mkuu yameshatoka na maisha yanaendelea na tumeapishwa. Lakini, kama mdadisi wa mambo, nimekuwa nikicheza na takwimu rasmi za INEC na Sensa yetu ya 2022. Naomba tusaidiane kuzitafakari hizi namba kwa pamoja, maana kwangu kimahesabu picha inagoma kukaa sawa.

Huu si uchambuzi wa nani alishinda, bali ni uchambuzi wa 'process' na uhalisia wa namba zenyewe.

KITENDAWILI CHA 1: Daftari vs. Sensa
Kwanza tuanze na hapa:

1.Watu wenye umri (14+ Miaka) - Sensa 2022: Milioni 35.3
2.Waliojiandikisha Kupiga Kura - INEC 2025: Milioni 37.7

Swali: Tumepata wapi watu Milioni 2.4 wa ziada waliojiandikisha (37.7M) kuliko watu waliopo wenye umri wa miaka 14+ (35.3M)?

-Au Sensa ya 2022 ilikosea na Watanzania tuko wengi kuliko walivyotuhesabu?😃
-Au, Daftari la Kudumu halijahuishwa kwa muda mrefu? Hizi Milioni 2.4 ni "majina hewa" (watu waliofariki, waliohama, waliojiandikisha mara mbili)?🤦
-Kama ni "majina hewa," je, yanaweza kupiga kura? Na kama yanaweza, yalipiga?🙂‍↕️

KITENDAWILI CHA 2: Kura 32.7M vs. Muda (The 540 Minute Puzzle)

Hapa ndipo mambo yanapopata utamu zaidi. Twende na namba rasmi:

1.Jumla ya Kura Zilizopigwa: Milioni 32.7
2.Jumla ya Vituo vya Kura: 99,895
3.Muda Rasmi wa Kura: Saa 1:00 Asubuhi - 10:00 Jioni (Jumla Saa 9 au Dakika 540)

Hesabu Rahisi:

-Wastani wa Kura kwa Kituo: 32.7M Kura / 99,895 Vituo = Wapiga Kura 327 (kwa kila kituo).

-Muda wa Mpiga Kura: Tukichukulia kwa uchache (optimistic) kwamba mpiga kura anatumia Dakika 2 tu (kuingia, kutambuliwa, kupewa karatasi, kupiga kura, kukunja, kutumbukiza).

HESABU SASA:
-Muda Uliohitajika Kituoni: 327 Watu × Dakika 2 = Dakika 654

-Muda Uliokuwepo Kituoni: Dakika 540 (Saa 9)
Utata Upo Hapa: Kimahesabu, kila kituo kilihitaji Wastani wa Dakika 654 (Saa 11) kumaliza wapiga kura wake 327.

- Lakini vituo vilifunguliwa kwa Dakika 540 (Saa 9).
Kila kituo kilipungukiwa na Dakika 114 (karibu Saa 2)!

KITENDAWILI CHA 3: Hoja ya Ukosefu wa Foleni (The 'No Queue' Paradox)

Hili ndilo linalonichanganya zaidi, na hapa naomba mliokuwa "ground" mshuhudie.

1.Matokeo ya Kimahesabu: Ili kura 32.7M zipigwe (86.9% Turnout), vituo vilitakiwa kuwa "busy" na kufanya kazi kwa Saa 11 bila kupumzika. Hii ingesababisha FOLENI KUBWA (misururu) kuanzia asubuhi hadi jioni, na watu wengi kuchelewa kumaliza.

2.Hali Halisi (Niliyoshuhudia na Niliyosikia): Vituo vingi vilikuwa "vimepooza". Hakukuwa na msongamano wa kutisha. Uchaguzi ulionekana kuwa na "hamasa ya kawaida," si ya 86.9% turnout.

Swali la Mwisho: Tunazipatanishaje hizi 'Option' mbili?
Option 1 (Super-Voters): Labda Watanzania walikuwa wepesi sana siku hiyo? Na walitumia Sekunde 99 tu (Dakika 1.6) kupiga kura badala ya Dakika 2 ambazo nimeashumu tu? (540 min / 327 kura = 1.65 min/voter).

Je, inawezekana mtu kumaliza mchakato wote kwa sekunde 99?🤔

Option 2: Labda kulikuwa na vituo vingi "visivyo rasmi" vilivyotumika ambavyo haviko kwenye hesabu ya 99,895? (Hii ni 'wild assumption').😱

Option 3 : Au...Hii 'turnout' ya 86.9% haikuwa ya watu halisi waliofika vituoni? Labda masanduku yalipata "msaada" ili kufikisha idadi ya kura 32.7M?

Option 4: Labda namba za INEC (kura zilizopigwa au idadi ya vituo) zina makosa ya kimahesabu?

Wadau,

Nawasilisha hoja hizi kwenu. Hizi namba na uhalisia wa vituoni ninaona vinapingana.

Hizi kura Milioni 32.7 ziliwezekanaje kupigwa ndani ya Dakika 540 bila kuacha foleni ?😎
Karibuni tujadili kwa HOJA.
Taifa limekosa WAZALENDO KABISAA ila angalau tuna watu wenye akili kama wewe.
 
Hoja ya msingi hapo ni moja tu, hakukuwa na foleni isingewezekana hizo kura nyingi zipigwe bila foleni kuwepo. kila mtu anajua hizo kura hazikupigwa.

Kuhusu muda wa kupiga kura, hapa watu onatakiwa waeleweshwe kura zinaweza kupigwa hadi usiku ilimradi watu hao walifika kituoni kabla ya saa kumi. ni kama benki vile muda wa kufunga unafika watu waliopo wanahudumiwa. Kama hili lingetokea basi zingeonekana foleni ndefu ila hakukuwa na foleni sababu watu hawakwenda kupiga kura.

Kuhusu numbers kwenye daftari la mpigakura na takwimu za Sensa kupishana jibu lake ni simple majamaa yameandikisha wanafunzi wenye miaka 14, 15, 16, 17 nchi nzima. kipindi wanaandikisa walikuwa hawajui kama kuna sensa ilifanyika 2022 tutaangalia walio na umri wa miaka 14+ ndo watakuwa na sifa za kuandikishwa.

Tukiachana na hayo yote, haiwezekani eti sensa iwe na big error yaani eti watu million 2.4 hawakuhesabiwa hii namba ni kibwa sana.
 
🙏🙏 Kwa maoni Mazuri mno...hii turnout ni balaa ilinitetemesha
 
Hayo mambo mbona yako wazi mkuu au unatafuta sababu wakuteke ubakie stori tu?
Nisamehe Mimi😃😃 ,,,wasiniteke nilikuwa nataka tuzungumze tu kwanini tunadanganyana hivi wakati ni sisi ndiyo tunaoishi Wala hatumpelekei mtu mwingine majibu kwamba atusahihishie atuone tumefaulu 🤦
 
Hapo kimsingi tunasema kitaalaam zaidi ni kwamba Matokeo haya kuwa na "VALIDITY" yaani result haiakisi uhalisia. So Probably ni business as usual Matokeo ya kupika aka cooked results 😂
 
Sema nini tunakoelekea mkuu ndio itakua kama ulivyofafanua hapo kwenye UZI wako yaani itafik mahali Matokeo yatadadavuliwa kwa kufuata vipengele kama hivyo hapo juu ili kujiridhisha kuna udanganyifu au hakuna. Itachukua muda lakini tutafika tu huko. Lazima tuendane na kasi ya dunia haiwezekani duniani kuna hadi teknolojia ya AI lakini sisi tubakie gizani kudanganyana hivi Hapana Aisee Big No!
 
Back
Top Bottom